Acheni upumbavu hakuna anaye pinga watu kupewa chanjo ,ARV wa kindomu bure watu wanacho pinga ni hii misaada kwa sababu inatudumaza akili.
Haiwezekani pesa za kufanyia mambo ya kipumbavu zimejaa lakini linapo kuja pesa za kuhudumia raia basi hizo hazipo bali mnategemea misaada ya taifa lingine.
Mkaguzi wa serikali kwenye ripoti ya mwaka juzi 2023 alisema kuwa Tz kwa mwaka inapoteza zaidi ya $bilion 1.5 kwa sababu ya ufisadi na ukwepaji wa kodi. Hapo bado hatuweka pesa zakuhonga makanisa na kununulia mashekhe magari, kununua magoli, kuhonga wapinzani ili waunge juhudi, kulipa machawa akina mwijaku waxunguke dunia nzima kumtangaza ,mtumizi ya viongozi kujifaharisha kwa mpaka mkuu wa wilaya ana msafara.
Hayo yote ukiyaunganisha unaweza kuta Tz ina poteza zaidi ya $bilion 2 na ushenzi kwa mwaka ambazo ni sawa na tuirion karibia 5,alafu leo unalilia dora milion 500 za msaada wa Marekani.
Yaani kiongozi wa nchi anaenda kanisani kutoa sadaka ya milion 100 lakini milion 20 za kujenga vyoo kwenye shule fulani hizo hazipo mpaka Japan aje kutoa msaada wa kukujengea hivyo vyoo.