Wapinga muundo wa serikali tatu

Wapinga muundo wa serikali tatu

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Waryoba.jpeg

Jaji Warioba

Mchakato wa kujadili rasimu ya mapendekezo ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umechukua sura mpya baada ya baadhi ya wajumbe kueleza kuwa mfumo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Rais ni sawa na kuunda Taifa jipya na si kufanya marekebisho ya Katiba.
Hali hiyo imejitokeza kwenye kikao cha Baraza la Katiba wakatiwajumbe wakichangia rasimu ya mabadiliko ya katiba katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Mkokotoni Mkoani Kaskazini Unguja kilichokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Kamishna Awadhi Ali Said akisaidiwa na Waziri Mkuu mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim.
Mjumbe kutoka shehia ya Zingwezingwe Abdallah Kombo Baraka (54) alisema mfumo uliopendekezwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba wa serikali tatu unakwenda kinyume na makubaliano ya mkataba wa Tanganyika na Zanzibar ya Aprili 26, 1964.
“Kubali kuwapo kwa serikali tatu ni sawa na kuunda Taifa jipya na kukiuka makubaliano yanayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, kiti cha Tanganyika na Zanzibar ni kimoja chini ya makubaliano yanayotambuliwa na sheria ya kimataifa, serikali ya tatu hilo ni Taifa jingine ndani ya Muungano," alisema.
Alipendekeza kuwa kifungu cha 57(1) kifutwe kwa vile kinakwenda kinyume na kukiuka makubaliano ya msingi ya Muungano.
Mjumbe Furaha Khamis Mshenga toka shehia ya Bumbwini Makobaalisema suala la serikali tatu linazingwa na utata na kwamba linaweza kuibua mgogoro unaoweza kuliyumbisha Taifa na kulisambaratisha.
Mshinfa alisema ikiwa Rais wa Tanganyika atatoka chama 'A', Rais wa Zanzibar chama 'B' na Rais wa Muungano akatoka chama 'C', huo utakuwa ni mwanzo wa mpasuko na mtikisiko lakini pia utii wa vyombo vya ulinzi na usalama utakosa nguvu.
“Amir Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama atakuwa nani katika mfumo wa serikali tatu, Rais wa Zanzibar, Tanganyika au Muungano, nafikiri hata msukomo wa kisera na uendeshaji wa nchi utakumbwa na urasimu," alisema.
Aidha wajumbe wengine waliopata nafasi ya kutetea mfumo wa muungano walisema baada ya Watanganyika na Wazanzibari kuunganisha damu kwa miaka 49 ni vigumu kuwatenganisha chini ya serikali tatu.

CHANZO: NIPASHE
 
basi ziwe mbili lakini muungano ufilie mbali.
 
huku wataka kule wata, chako changu, changu changu hiyo ndio Zanzibar serikali yao wanayo, lakini hawataki wengine wao na yao
 
Back
Top Bottom