Wapinzani Chukueni Tahadhari, Njama Walizopanga CCM Kuelekea Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa 2019

Anabadilika kama kinyonga
Leo karopoka mambo ya ajabu, kaacha kuongelea chama chake ameongelea vyama vya upinzani mwanzo wa speech mpaka mwisho, sijui atafanyaje uenezi wa vyama vya upinzani.
 
Hii ni ramli chonganishi si kila kitu unachoamka nacho muda wowote ukilete hapa, ukiambiwa thibitisha ulichokisema unaanza kuhangaika, tatizo watu mnakuwa na ujasiri mnapokuwa nyuma ya keyboard
 
Hii ni ramli chonganishi si kila kitu unachoamka nacho muda wowote ukilete hapa, ukiambiwa thibitisha ulichokisema unaanza kuhangaika, tatizo watu mnakuwa na ujasiri mnapokuwa nyuma ya keyboard
Pimbi wenu wa Wilaya ya Hai hujaona vituko anavyofanya.
 
Mkuu ahsante sana kwa taarifa hizo za huko JIKONI. Nina amini Vyama husika watazifanyia kazi, ili hawa MABEBERU WA AFRIKA waendelee kudhibitiwa ipasavyo.
Yes opposition must take precaution against Satan and his evil plan.
 
Nyinyi hamuishi mbinguni, narudia ccm hawaishi mbinguni wanaishi na watu sio kila anayewaona mnafanya maovu anawafurahia. Sasa wasiofurahia uovu wenu ndio wanaovujisha mipango yenu miovu.
 
Mtoa mada umedhihirisha una "mardhi ya moyo kuhusu" Prof. Lipumba na chama cha CUF. Unalazimisha kupandikiza kwenye vichwa vya watu kuwa
1. Chama cha CUF "cha sasa" ni kidogo mno na hakina nguvu ukilinganisha na ACT.
2. Katika nchi hii wapinzani wa kweli ni ACT na CHADEMA tu.
3. CUF sio wahanga wa hujuma za serikali/CCM kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa na kwamba hawakustahili kulalamika na kujitoa kama walivyojitoa "wapinzani"

Bila shaka matamanio yako ni kuona CUF kimekufa na badala yake iwe ACT. Zaidi, ulitarajia kuona "CUF ya Lipumba" kinaendelea kushiriki uchaguzi huu ndipo "nafsi yako" ingetulia katika fikra na mtazamo wako juu ya chama hicho kuwa kipo pale kama mamluki wa CCM.

Kwa bahati mbaya sana chama hicho kimeenda kinyume na fikra na matarajio yako na matokeo yake sasa unatapatapa kulazimisha unachokitaka kiwe.

Bali maamuzi ya chama hicho kujitoa yamekupa "mardh ya moyo" ambayo yamesababisha kuwe na "logical discontinuity" katika mada yako. Mathalani, umeishia kutoa tahadhari tu bila kuonesha ni jinsi gani kujiondoa kwa CUF kunainufaisha CCM dhidi ya hao wapinzani au wapinzani wangenufaikaje dhidi ya CCM endapo CUF kingeendelea na uchaguzi. Zaidi umeshindwa kuonesha njia kwa wapinzani ya kudhiti hujuma za CCM dhidi yao kwa kuitumia CUF.

Kwa dalili ulizozidhihirisha katika mada hii nachelea kusema usingekosa "kuchonga" kuwa "CUF ya Lipumba" kinaunga mkono hujuma za CCM dhidi ya "wapinzani" endapo kingeendelea kubariki na kishiriki uchaguzi.

Unajaribu kulazimisha akili za watu ziamini unachokiamini kuhusu CUF. Kuna wakati yakupasa utambue kuwa si kila mtu kwenye jukwaa hili anaweza kushikiliwa akili iwe kishabiki, kimahaba wala kwa chuki bali wako walio huru na wenye uwezo wa kuyaona mambo kwa kutumia akili zao wenyewe.
 
Kitu gani hakieleweki? Chama cha kijani ccm hesabu zao za ushindi wa asilimia 95 zimefeli kwa kuwa Chadema na Act Wazalendo na vyama vingine vimejitoa, lengo la ccm ni kuionyesha nchi na ulimwengu kuwa wamekishinda chama kikuu cha upinzani nchini Chadema. Sasa kwa kuwa kimeondoa na vingine vikafuatia, ccm wamelazimika kuvitoa vyama vyake mamluki viifuate Chadema na baadaye virudi kwenye uchaguzi kama vitakavyoelekezwa na ccm ili kuuhalalisha uchaguzi ionekane upinzani umeshiriki, pamoja na Chadema na Act Wazalendo kujitoa, hivyo kutafuta uhalali wa uchaguzi kwa jumuiya ya kimataifa na wafadhili, huulewi nini sasa?
 
Novemba 24 sio mbali Mungu akipenda tutaona hivyo vyama mamluki vikishiriki uchaguzi. Hapo ndipo maradhi yako yatakapopanda zaidi kuona dhana, hisisia, mtizamo na fikra zako juu ya vyama vingine hazitimii na mimi nitakukumbusha urekebishe huu uzi wako.
 
 
Soma hii barua ili ukazie hoja yako kuhusu Lipumba na CUF yake.
 

Attachments

  • FB_IMG_15738311348070857.jpg
    38.8 KB · Views: 2
humu nimegundua watu bado hawajawa makini . mleta uzi ametoa kama angalizo , dokezo , siri, sasa wale wanaopewa siri, eti hawataki... ndugu tunashukuru kwa maelezo yako ....yatasaidia kwa walengwa .achana na wavuruga mada .
 
NAIAMINI TAARIFA HII
 
We ccm au mpinzani??? Mana km sio ccm umezipata wap taarifa
 
Leo ni Novemba 25, ni siku moja tu baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Je, unaweza kutuonesha "ukibaraka" wa CUF ya Lipumba katika kususia uchaguzi? Je, kuna mtaa, kijiji au kitongoji chochote ambako CUF wameshiriki uchaguzi kama ulivyowapa tahadhali wapinzani wa kweli?
 
Taarifa ya matokeo ya uchaguzi leo yanaonyesha CUF wamepata kijiji kimoja mitaa 3 na nafasi mchanganyiko 19. Kujibu hoja yako ni kwamba taarifa zinazoletwa humu hulenga kuvujisha mipango ovu, ili waovu wasiitekeleze. Umeshawaambia majambazi kuwa umeshajua siku fulani watakuja hivi wewe unafikiri wao wajinga waje siku hiyohiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…