MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimesoma sehemu mbalimbali kwamba inasemekana mojawapo ya sehemu ya maridhiano ni wapinzani kuachiwa majimbo kadhaa ya uchaguzi.
Baada ya kutafakari sana kisha ku-connect dots na haya matusi ya viongozi waandamizi wa upinzani dhidi ya bodaboda na makundi mengine ya kimkakati nikahisi inaweza kuwa kweli.
Naona kama vile wapinzani wamejiwekea hayo matumaini ndo maana wanaishia kutukana wapiga kura kwamba kazi zao ni za laana.
Linapokuja suala la uchaguzi ni kwamba CCM huwa haina mzaha kabisa... alishawahi lalamika Zitto Kabwe kwamba kwenye uchaguzi mdogo tu huko jimboni Kigoma, CCM ilipeleka viongozi wake wa kitaifa akiwemo makamu wa Rais kupiga kampeni.
CCM kamwe hawawezi kuachia chama chochote jimbo. Kitu pekee cha kutia moyo ni kwamba 2025 uchaguzi utakuwa huru na wa haki hivyo wapinzani wajipange badala ya kudhani watapewa majimbo kama zawadi.
Sanduku la kura ndo litaamua. CCM haina mjadala wala utani kwenye uchaguzi wa ngazi yoyote ile.