Uchaguzi 2020 Wapinzani hawako tayari kuongoza nchi

Sasa wewe unaangaliaje maneno ya watu wachache na kuyafanya kuwa kweli? Hatahivyo, hao wote wameshaomba msamaha

Kikubwa wewe mwenyewe umeona mzee mambo ametenda. Amethibitisha kuwa anaweza na zaidi ya kuweza
Sasa kama ameweza from zero experience kwann hao wapinzani wenye uzoefu wasemwe kuwa hawawezi?
 
HOTUBA YA TUNDU LISSU ARUSHA:
1. Lissu kazungumzia ugumu wa maisha ya mfanyakazi na jinsi atakavyoyaboresha kwa kulipa malimbikizo yote wanayodai na kuwalipa nyongeza zao za mishahara za kisheria(annual increments)

2. Amezungumzia uonevu wanaofanyiwa wafanyabiashara wetu na kwamba ataundoa

3. Amezungumzia kuhusu elimu bora na siyo bora elimu, amezungumzia kuhusu elimu ya ujuzi wa kazi siyo ya kukariri

4. Amezungumzia kuhusu viwanda na kuvutia mitaji ili kutoa ajira kwa vijana wetu

5. Amzezungumzia kuhusu diplomasia yetu iliyoshuka na jinsi atakavyorudisha mahusiano bora ya kimataifa

6. Amezungumzia bima ya afya kwelikweli siyo hii ambayo wazee wetu wakishastaafu wanaambiwa waongeze hela ili waweze kuwekwa kwenye bima ya magonjwa nyemelezi ya wazee

7. Amezungumzia kuhusu kuirejesha Arusha kuwa kitovu cha utalii

8. Amezungumzia kuhusu katiba mpya, ameonyesha ubovu wa katiba ya sasa ambayo imelinyima hata bunge uwezo wa kuanzisha hoja ya namna ya kutumia pesa za nchi isipokuwa tu kama hoja hiyo imeanzishwa na serikali.

9.Amezungumza kuhusu haki za watu, ametetea masheikh walio jela kinyume cha sheria, kwa mfano amesema Arusha peke yake kuna Masheikh 70 wako jela achilia mbali wale masheikh wa uamsho.

10. Amezungumzia kuvunjia wananchi nyumba kikatili etc

11. Kszungumzia mzigo mzito wa makato ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu na amesema atashusha makato hayo kwa mwezi kutoka 15% hadi 3% ya mshahara kwa mwezi

12. Amezungumzia kuhusu adha za vitambulisho vya kimagumashi vya wamachinga amesema ataondoa mzingo wa shilingi 20000 ya kitambulisho cha wamachinga pesa iliyoanzishwa na Bashite na Magufuli

13. Amesema ataanzisha sheria ya haki ya mlipa kodi "Bill of taxpayers rights" ili waweze kulindwa kisheria badala ya utaratibu wa sasa ambao wafanyabiashara wanaonewa sana na TRA na hawana pa kukimbilia, kila wanapokimbilia wameshafungwa minyororo

14. Amezungumzia kuhusu uhuru wa habari, kuwa ataondoa sheria kandamizi zilizotungwa na Magufuli kumlinda yeye badala ya kusaidia taaluma kukua

15. Amesema ataomesha matumizi ya hovyo ya pesa za serikali, siyo rais akiamka asubuhi anajenga uwanja wa ndege kijijini kwake ambapo ndege inatua mara mbili kwa mwaka siku anayoenda kula Christmass na pasaka

16. Lissu anazungumzia kuhusu UHURU, HAKI, MAENDELEO
 
Maarifa ya kusimamia wanachama wao tu hawana wataweza kuongoza serikali iliyoajili millions of people wenye tabia za kila namna na kujaribu kuwaweka wote kwenye mstari.

Imagine this Mayor Jacob kawekewa pingamizi na mgombea wa ACT viongozi wake hakina Zitto wanadai ni mgogoro binafsi. Hapo hapo huko ndani ya vyama vyao utakuta kuna watu wamepewa titles za whips sasa sijui ana kazi gani iwapo wanachama can do as they wish.

Chama kinaposema tunakwenda hivi kama walivyoamua kushirikiana na CDM ina maana kila mwanachama has to toe with official party lines. Mtu anakiuka agenda za chama halafu mabosi wake wanadai ni ugomvi.

Hivi wanadhani vyama vya siasa vingekuwa vinaruhusu kila mmbunge wake awe na uhuru binafsi, huko bungeni sheria zao au budget zingepita kweli.

Watu wenyewe kuongoza taasisi zao awawezi wanataka nchi pathetic Zitto.
 
Ishu sio kuwa na wish list, ishu kasema atatekelezaje?

Mwenzake huku Dr Magufuli anatekeleza kwa vitendo
 
Sasa kama ameweza from zero experience kwann hao wapinzani wenye uzoefu wasemwe kuwa hawawezi?
Dr Magufuli hakuwa na zero experience, yeye alikuwa n waziri mwandamizi. Kumbuka amekuwa naibu na waziri kamili kwa kipindi cha miaka 20
 
Dr Magufuli hakuwa na zero experience, yeye alikuwa n waziri mwandamizi. Kumbuka amekuwa naibu na waziri kamili kwa kipindi cha miaka 20
Waziri hafanyi kazi za kiutawala ndugu. Unapingana na prof. Mwandosya?
 

Taga katika ubora wako. Ya kuwa wanahitaji kupasishwa na wewe siku sasa wakifuzu?

Kama hizi siyo zile ndoto za Alinacha. Ndoto hizo zitakuwa hazipo tena.

Yote hiyo ni buku 7 ndiyo inayofagiliwa? Heko bro.

Hiiiii bagosha!
 
Waziri hafanyi kazi za kiutawala ndugu. Unapingana na prof. Mwandosya?
Kwani kazi ya waziri ni nn?
Uzoefu unaoongelewa hapa ni upi?
Yeye Prof uzoefu wake ni upi!

Halafu kaa ukijua kuwa Prof Maandosya n binadamu wa kawaida, naye hukosea
 
Taga katika ubora wako. Ya kuwa wanahitaji kupasishwa na wewe siku sasa wakifuzu?

Kama hizi siyo zile ndoto za Alinacha. Ndoto hizo zitakuwa hazipo tena.

Yote hiyo ni buku 7 ndiyo inayofagiliwa? Heko bro.

Hiiiii bagosha!
Kwahiyo tumekubaliana kuwa nyie mkiandika habari za vyama vyenu ni uzalendo ila sisi tukiandika habari za CCM n buku 7
 
Kwahiyo tumekubaliana kuwa nyie mkiandika habari za vyama vyenu ni uzalendo ila sisi tukiandika habari za CCM n buku 7

Kabisa. Uzalendo wa Lissu usipouona wewe ni buku 7. Waulize buku 7 wenzio watakwambia. Hivi wana hofu sana kuwa watakula wapi sasa kwa upepo huu?

Bila angalau ya buku 7 kwa hakika hayupo wa kuandika huu utopolo mnaoandika. Kwa hamasa ipi?
 
Amani Msumari, Ila ccm akili huwa zinaruka mara nyingine, et lijitu linakwambia tumeibiwa sana wakati nyinyi wenyewe ccm ndiwo mlikuwa mnasaini mikataba na mibovu na wakoloni haohao, misaada hampati toka kwa hao wakoloni basi mnawaita mabeberu.
 
Wakati mwingine wengine tubaki wasomaji tu!Sasa hapa haya mashudu kweli yameandikwa na mtu mzima!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wapo kwa ajiri ya ruzuku tu hamna lolote
akuna wapinzani kuna waganga njaa tu.
Ukweli haiwezi kuwa uchafu jombii
Hivi nyie watu mnaokotwa wapi, hata Kiswahili jamani? Mnaishushia hadhi JF yetu, rudini huko huko Lumumba.
Dr Magufuli hakuwa na zero experience, yeye alikuwa n waziri mwandamizi. Kumbuka amekuwa naibu na waziri kamili kwa kipindi cha miaka 20
Kumbe! Kwa hiyo kulalamika na kukurupuka kote kumbe alikuwa ndani ya serikali zilizopita akila nao, akishirikiana nao, akifisadi nao! Halafu leo anadai anainyosha nchi! Kweli wajinga ndio waliwao!
 
TBCCCM sasa ni mali binafsi ya CCM walienda kuhujumu mkutano wa chadema, wanalipwa mishahara kwa kodi za watanzania wote lakini cha ajabu wamekuwa watumwa wa CCM tu, corona ipo chini chini watu wanakufa lakini husingizia ni magonjwa mengine kuogopa kutengwa na jamii lakini ipo, CCM ni chama cha kishetani na hovyo kilichosalia Duniani sasa wamekuja na style haramu ya kupita bila kupingwa ukiwa ni ushetani Hatari tokea Nchi ipate uhuru mwaka 1961
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…