Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa amesema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya Jimbo la Ukonga, vyama vingine kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa 'wametia mpira kwapani' kwenye mitaa 28 ndani ya jimbo hilo na kukubali yaishe, huku kinachosubiriwa ikiwa ni kura ya ndiyo au hapana.
Silaa ameyasema hayo kwenye mkutano wa ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Jimbo la Ukonga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Amos Makalla.