Wapinzani mna la kusema Uchaguzi wa Udiwani?

Wapinzani mna la kusema Uchaguzi wa Udiwani?

CCM yashinda viti vingi vya madiwani wapinzani watamba mijini
Na Waandishi wetu

CHAMA ha Mapinduzi (CCM) kimepata viti vingi vya udiwani kati ya vivyokuwa vinagombewa katika uchanguzi mdogo uliofanyika nchini juzi, huku wapinzani wakitamba kwenye kata za mijini. Mpaka sasa CCM imepata viti vitano na wapinzani viti vinne.

Kutoka Arusha Mussa Juma, anaripoti kuwa Umoja wa Wapinzani, umeibwaga Chama CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sombetini ambao nusura uvurugwe na polisi kufuatia kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliokuwa na jazba wakisubiri matokeo.

Uchaguzi huo uliofanyika baada ya kiti cha udiwani wa kata hiyo kuwa wazi baada

ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Mussa Mkanga (CCM) 'kuenguliwa' kwa madai ya

kuhusika na ugawaji wa kiwanja cha wazi kilichopo eneo la kilombero kwa kampuni

ya EMOIL Marketing Ltd kinyemela mapema mwaka huu.

Katika uchaguzi huo mgombea wa TLP, Alphonce Mawazo Chemu aliibuka mshindi kwa kupata kura 1515 wakati mgombea wa CCM, Fabian Gabriel Mhindi aliambulia kura 1473.

Kabla ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi huo ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata hiyo,

Juma Kitumbo kutangaza matokeo hayo, wafuasi wa vyama vya upinzani walishinikiza

kutangazwa kwa matokeo hayo hasa kutokana na kujua kuwa wameshinda lakini

msimamizi huyo mara zote alikuwa akihaha kutoa majibu huku akipokea simu mbali

mbali.

Hali hiyo ilisababisha kuibuka kwa vurugu zilizosababisha askari polisi kitengo

cha Kuzuia Ghasia (FFU) kutinga katika Ofisi ya Mtendaji eneo la Mbauda, majira ya

saa 12.30 jioni wakiwa na silaha za moto tayari kukabiliana na hali hiyo.

Hata hivyo giza lilivyozidi kutanda, wafuasi hao wakionekana kuwa na furaha

iliyochanganyika na wasiwasi wa kuporwa kura zao, wakiwa nje ya ofisi hiyo

waliendelea kuimba nyimbo za kumshinikiza msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo

kutangaza matokeo hayo, huku viongozi wa vyama vya upinzani wakilinda masanduku ya

kura.

?Hakuna kulala?tunataka matokeo?msije kupora kura zetu kama ilivyokawaida

yenu,? hizo ni sehemu za nyimbo walizokuwa wakiimba wafuasi huo huku mashabiki wa

CCM akionekana kujikusanya vikundi, vikundi wengine wakiwa nje ya Ofisi ya chama

hicho iliyoko karibu na Ofisi ya Kata.

Umati wa wafuasi hao ulizidi kuongezeka kadri saa zilivyozidi na ilipofika saa 1

usiku askari hao walianza kuvurumisha mabomu ya machozi ovyo hali iliyosababisha

watu kukimbia huku na kule kusaka maji ya kuosha macho yao ambapo walilazimika

kunawa miferejini.

Hali hiyo ilidumu kwa saa tatu hadi saa 4.30 licha ya msimamizi wa uchaguzi huo

kutangaza matokeo majira ya saa 2.45 usiku, ambapo viongozi mbalimbali wa vyama

hivyo wakishuhudia akiwemo Msimamizi wa Uchaguzi wilaya, Job Laizer ambaye pia ni

Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha.

Wafuasi hao wa vyama vya upinzani, walitawanyika na kuendelea na shamrashamara za

ushindi huo, ambapo jana mchana walitarajiwa kufanya sherehe katika viwanja vya

Ngusero kushehekea ushindi huo.

Naye Jospeh Senga anaripoti kutoka Songea anaripoti kuwa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda kwa kishido katika Kata ya Majengo katika uchaguzi mdogo uliofanyika jana katika Kata hiyo iliyoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.

Mgombea kwa tiketi ya Chadema Idd Ibrahim aiyekuwa akiungwa mkono na vyama

vya TLP, NCCR-Mageuzi na CUF alipata kura 1,015 kati ya kura halisi 1,569

zilizopigwa na Halfan Kigwenembe wa CCM alipata kura 554. Jumla ya kura

zilizopigwa ni 1,581 na zilizoharibika ni 12.

Kwa matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa

ya Songea, Edigar Berege alimtangaza Idd Ibrahim kuwa mshindi.

Tofauti na chaguzi zingine ambapo wanawake wanakuwa wengi, katika uchaguzi huo idadi kubwa ya wanaume na vijana walijitokeza wingi kupiga kura.

Ulinzi mkali ulikuwepo katika uchaguzi huo,Kamanda wa polosi wa Mkoa wa Ruvuma,Falhum Mshana na Mkuu wake wa polisi wa Wilaya ya Songea walikuwepo kutokana uchaguzi huo kuvuta hisia za watu wengi.

Baada ya kura kuhesabiwa na matokeo kubandikwa kwenye vituo vya kupigia kura

wafuasi wa vyama vya upizani walianza kushabgilia

Kutoka Muheza, Tanga, Steven William anaripoti kuwa,? CCM imeibuka kidedea baada ya kushinda kwa kishindo katika? uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Masuguru baada ya mgombea wake, Dorothi Kihampa kupata kura nyingi.

?

Uchaguzi huo mdogo ulihusisha?wagombea wa?vyama vitano ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, UDP na TLP.

?

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo majira ya saa mbili usiku katika Shule ya Msingi Masuguru ambako kura zilihesabiwa, Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni ?Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza, Ephireem Kalimawendo, alimtangaza Kihapa wa CCM kuwa mshindi kwa kupata kura 720 akifuatiwa na Awadhi Mjenga wa CUF, alipata kura 363,Chombo Ahamedi (Chadema) kura 9, Yusuphu Salimu (UDP) kura saba na Maiko Muhina waTLP aliyeambulia kura 2.

?

Baada ya matokeo hayo kutangazwa na Mkurugenzi huyo sherehe za maandamano ya CCM zilianza kutoka katika Shule ya Msingi Masuguru hadi Ofisi ya CCM Wilaya ya Muheza ambapo kulikuwa na sherehe.

Naye Abdallah Nsabi kutoka Maswa anaripoti kuwa, CCM imeibwaga CUF katika kinyanganyiro cha udiwani wa Kata ya Nguliguli kwa kunyakua kiti hicho.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Maswa, Gabriel Fuime, alimtangaza mgombea wa CCM Petro Mashara kuwa mshindi baada ya kupata kura 2,222 dhidi ya mgombea wa CUF Jibusa Karaja aliyepata kura 828.

Amesema kuwa uchaguzi ulifanyika kwa kufata taratibu zote za uchaguzi na idadi ya

wapiga kura 3117 walijitokeza kupiga kura na kura 67 ziliharibika na kwamba hakuna malalamiko yoyote yaliyojitokeza katika uchaguzi huo na kila chama kilikubaliana na matokeo hayo.

Akizungumzia matokeo hayo, Mwenyekiti wa CCM, Hamis Mgeja alisema ushindi uliopatikana umetokana na mshikamano uliokuwepo kati ya wanachama na viongozi wa achama hicho na kisha kuwapongeza wapinzani wao CUF kukubali matokeo.

Kutoka Sumbawanga mwandishi wetu anaripoti kuwa, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Katazi, Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa kwa tiketi ya Chadema, Anselmo Mzatula ambaye alihamia CCM amechaguliwa tena kushika wadhifa huo kwa tiketi ya chama hicho.

Ushindi huo wa CCM umetokana na kata ya Katazi kuorodheshwa kati ya kata tatu za

mkoa wa Rukwa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani ambazo ziliachwa wa baada ya madiwan wake kufariki dunia.

Mzatula ambaye alijiuzulu uwanachama wa Chadema na kujiunga na CCM mapema mwaka huu ameibuka mshindi kwa kupata kura 1,295 dhidi ya mpinzani wake Aloyce Sokoni wa

Chadema aliyepata kura 324.

Taarifa kutoka wilayani Nkasi zimeeleza kuwa madiwani wa vyama vya upinzani wamepoteza kata moja kati ya mbili zilizokuwa zinaongozwa na madiwani wa vyama hivyo kabla ya uchaguzi huo.

Msimamizi wa jimbo hilo Bi Christina Midelo alisema kuwa Sospeter Kasawanga wa CCM

alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura 2,310 dhidi ya mpinzani wake Pius Mwanisawa aliyepata kura 1, 837.

Alisema katika Kata ya Kabwe, mgombea wa Chadema, Asante Libinsha alipata kura 1,953 na kumshinda mgombea wa CCM, Juma Milumba aliyepata kura 1,713, na kura 84 ziliharibika
 
Mpaka sasa: wapinzani 4, CCM 5.

Hii ni mpya katika medali za kisiasa Tanzania. Nampongeza sana JK maana ni katika utawala wake ambapo upinzani utaimarika bila yeye kupenda. Safi sana!
 
Mpaka sasa: wapinzani 4, CCM 5.

Hii ni mpya katika medali za kisiasa Tanzania. Nampongeza sana JK maana ni katika utawala wake ambapo upinzani utaimarika bila yeye kupenda. Safi sana!

Kitila,

Mbona unasahau vile viti vya bila kupingwa?

Naona mmejitahidi sana, ila mimi nilikuwa nategemea zaidi hasa baada ya hili suala la Zitto. Jana viongozi wote wa upinzani wangejazana huko vijijini ambako ndiko kuna wapiga kura wengi na hawasomi JF, magazeti wala kusikiliza radio. Huko ndiko inatakiwa
kuwa na mikakati ya kuwabadilisha watu.

Mkiendelee kutumia muda mwingi mjini mwaka 2010 mtafungwa magoli mengi tena. Sikusikia vigogo wa CCM wakienda kupiga kampeni, hapo pesa hazijachotwa BOT, lakini 2010 tegemea CCM kutumia kila njia.
 
...kweli inatia moyo,huu ndio mwanzo wa kuyang'oa mafisadi haya
 
Mwiba, Mwalimu wako wa darasa la tatu hakukufunza matumizi ya vituo? Unaumiza macho ya wasomaji wa maandishi yako.
Ipo kazi ,mimi hua siandiki ,nafanya kama nipo nanyi,tunazungumza uso kwa uso,sasa huwa nasikiliza kwa vile mpo hewani napata majawabu yenu kupitia akilini,huwaga naisikiliza akili yangu ikiwasemea,mtajibu nini na baada ya kupata jibu huwa niandikalo ni jawabu,nina uhakika wa kile utakachokuja kukiandika itakuwa umekifikiria mara mbili baada ya kuona tayari umeshajibiwa ,najaribu kuweka diffence na ndio umahiri wa kuandika katika hoja za kuulizana kwa kutumia mtandao.Na tayari nimeshaona wingine wametoshelezeka maana nimewabana na wamebanika,wanabaki kuchomelea tu.Bado mimi ni mgeni hapa najaribu kufuata sheria ambazo naona inatakiwa uwe unaunga mkono tu japo haauungiki,zile zile siasa za CCM oyee,wengi wape au vipi.
 
mhh,

naona kuanza kusherekea ushindi....

ama kweli hii list ya mafisadi italeta wengi mwaka huu
 
Kitila Mkumbo
JF Senior Expert Member

This is bad news;

-----------------------------------------------------------------

CCM unopposed in five wards
DAILY NEWS Reporter
Daily News; Monday,October 29, 2007 @00:04

FIVE CCM candidates sailed through unopposed in by-elections for councilors in 16 wards held throughout the country yesterday, fanning speculation that the ruling party could emerge with massive victory in full results expected today.

Mkuu Kitila,

Huu wako ni mfano wa kuigwa hapa forum, kukubali ukweli kunapokuwa na ukweli, yaani kabla uchaguzi kuanza na kuisha tayari matokeo yalikuwa,

CCM 5, Chadema 0!

Heshima mbele mkuu, kwa kutuhabarisha ubarikiwe tu!
 
Cha kusikitisha hapa ni pamoja na tuhuma mbali mbali za ufisadi, ula rushwa na kujilimbikizia mali bado kuna Watanzania ambao wametia pamba masikioni na kutoona kasoro yoyote ya kuwapigia kura CCM! hili mimi linanisikitisha sana. CCM wafanye kipi kibaya ili hatimaye wananchi wasiwapigie kura!? Halafu wananchi hawa ndio wa kwanza kulalama kwa ukosefu wa ajira, huduma finyu na mazagazaga mengine chungu nzima! Ama kweli wadanganyika wataendelea kudanganyika!
 
Cha kusikitisha hapa ni pamoja na tuhuma mbali mbali za ufisadi, ula rushwa na kujilimbikizia mali bado kuna Watanzania ambao wametia pamba masikioni na kutoona kasoro yoyote ya kuwapigia kura CCM! hili mimi linanisikitisha sana. CCM wafanye kipi kibaya ili hatimaye wananchi wasiwapigie kura!? Halafu wananchi awa hawa ndio wa kwanza kulalama kwa uksefu wa ajira, huduma finyu na mazagazaga mengine chungu nzima! Amwa kweli wadanganyika wataendelea kudanganyika!

...hao ni wale wa madebe ya pombe na makada waizi wa kura,hujiulizi kwanini CCM inashinda vijijini na mijini inapata shida sana,ni kwa sababu kule ndio kuna wenzao ambao wamewafanya maskini na sera zao hata shule hawajaenda na hawajui chochote zaidi ya kidumu fikra za chama
 
Mpaka sasa: wapinzani 4, CCM 5.

Ushirika wa wapinzani waanza kuzaa matunda

na Mwandishi Wetu

MATUNDA ya ushirikiano wa vyama vinne vya upinzani yameanza kujionyesha katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika katika kata 16 maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi, ushirika wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), NCCR - Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na Tanzania Labour (TLP), umewawezesha wapinzani kutwaa viti vinne vya udiwani, idadi ambayo ni robo ya viti vilivyokuwa vikishindaniwa.

Ushirika huo wa wapinzani umewawezesha kutwaa kiti kimoja katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, ambacho mgombea wa CHADEMA aliyekuwa akiungwa mkono na wapinzani wenzake alipita bila kupingwa.

Mbali na hicho, vyama hivyo vinne ambavyo katika miezi ya hivi karibuni vimelitikisa taifa kwa hoja nzito za ubadhirifu ndani ya Benki Kuu na ile ya utata wa mkataba wa Buzwagi, vimetwaa viti vingine vitatu katika kata za Majengo (Songea Mjini), Kabwe (Rukwa) na Sombetini (Arusha).

Pamoja na mafanikio hayo ya ushindi wa asilimia 25, Chama Cha Mapinduzi kikitumia ukongwe wake, kimefanikiwa kujinyakulia ushindi katika kata nyingine 12 zilizokuwa zikigombewa.

Kutoka Songea, Marietha Msembele anaripoti kuwa mgombea wa CHADEMA, Iddi Ibrahim Abdalah, alimshinda mgombea wa CCM, Alfani Kigwenembe katika Kata ya Majengo na hivyo kukipokonya chama hicho tawala eneo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na kada wa CCM, Adam Mwaibabile, aliyefariki dunia mapema mwaka huu.

Akitangaza matokeo juzi majira ya saa 5:00 usiku katika jengo la SACCOS ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, msimamizi wa uchaguzi, Edger Belege, alisema Abdallah alifanikiwa kupata kura 1,015 huku mpinzani wake, Kigwenembe akiambulia kura 554. Kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 3,754.

Akizungumza na waandishi wa habari, Abdalah alisema kuwa, ushindi alioupata ni matokeo ya udhaifu wa CCM, kwani awali aliomba kugombea udiwani kwa tiketi ya CCM na alibwagwa katika kura za maoni wakidai kuwa hauziki.

Kiongozi mwingine wa CHADEMA mkoani Ruvuma, Joseph Fuime, alisema kuwa ushindi huo ni mvua za rasha rasha na kwamba kwa sasa CHADEMA inajipanga kuchukua nafasi nyingine za udiwani katika kata nyingine, pamoja na ubunge wa Jimbo la Songea Mjini.

Hata hivyo, CCM iliibuka na ushindi katika kata za Muwesi na Malumba wilayani Tunduru ambapo katika Kata ya Muwesi, Nurudin Nolela alipata kura 1,140 na Kata ya Malumba, Msenga Saidi alizoa kura 1,557.

Kutoka Arusha, David Frank anaripoti kuwa polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama vya upinzani waliokuwa wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa diwani katika Kata ya Sombetini.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa TLP, Alphonce Mawazo Chemu aliibuka mshindi kwa kupata kura 1,515 wakati mgombea wa CCM, Fabian Gabriel Mhindi aliambulia kura 1,473.

Uchaguzi huo uliofanyika baada ya kiti cha udiwani wa kata hiyo kuwa wazi, baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Mussa Mkanga (CCM), kuenguliwa kwa madai ya kuhusika na ugawaji wa kiwanja kilichopo eneo la Kilombero kinyemela, mapema mwaka huu.

Kabla ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo ambaye ni Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Juma Kitumbo, kutangaza matokeo hayo, wafuasi wa vyama vya upinzani walishinikiza kutangazwa kwa matokeo hayo wakihofu kuwa ucheleweshwaji ulikuwa ni moja ya njama za kuwapora ushindi.

Hali hiyo ilisababisha kuibuka kwa vurugu zilizosababisha askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) kutinga katika Ofisi ya Mtendaji eneo la Mbauda, majira ya saa 12:30 jioni wakiwa na silaha za moto.

Hata hivyo, giza lilivyozidi kutanda, wafuasi hao wakionekana kuwa na furaha iliyochanganyika na wasiwasi wa kuporwa kura zao, wakiwa nje ya ofisi hiyo waliendelea kuimba nyimbo za kumshinikiza msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo kutangaza matokeo hayo huku, viongozi wa vyama vya upinzani wakilinda masanduku ya kura.

Umati wa wafuasi hao ulizidi kuongezeka kadiri saa zilivyozidi na ilipofika saa 1 usiku askari hao walianza kuvurumisha mabomu ya machozi ovyo, hali iliyosababisha watu kukimbia huku na kule kusaka maji ya kuosha macho, huku baaadhi wakitumia maji yaliyooshewa vyombo katika migahawa ya mama lishe.

Hali hiyo ilidumu kwa saa tatu hadi saa 4:30 licha ya msimamizi wa uchaguzi huo kutangaza matokeo majira ya saa 2:45 usiku.

Wafuasi hao wa vyama vya upinzani, walitawanyika na kuendelea na shamrashamara za ushindi huo, ambapo jana mchana walitarajiwa kufanya sherehe katika viwanja vya Ngusero kusherehekea ushindi huo.

Kutoka Sumbawanga, Prisca Ngonyani anaripoti kuwa aliyekuwa diwani wa Kata ya Katazi, Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa kwa tiketi ya CHADEMA, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Anselmo Mzatula, amechaguliwa tena kushika wadhifa huo kwa tiketi ya CCM.

Ushindi huo wa CCM umetokana na kata ya Katazi kuorodheshwa kati ya kata tatu za Mkoa wa Rukwa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 16 nchini mwishoni mwa wiki iliyopita ambazo madiwani wake wamefariki dunia au kujiuzulu vyama vyao vya awali.

Mzatula, ambaye alijiuzulu uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM mapema mwaka huu, aliibuka mshindi kwa kupata kura 1,295 dhidi ya mpinzani wake, Aloyce Sokoni wa CHADEMA, aliyepata kura 324.

Akitingaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi huo, Mussa Zungiza, alisema jumla ya watu 5,310 wa Kata ya Katazi walijiandikisha kwa ajili ya uchaguzi huo lakini waliojitokeza kupiga kura ni 2,219 tu.

Katika Jimbo la uchaguzi la Nkasi imeelezwa kuwa madiwani wa vyama vya upinzani wamepoteza kata moja kwa CCM, kati ya mbili zilizokuwa zinaongozwa na madiwani wa vyama hivyo vya upinzani kabla ya uchaguzi huo.

Msimamizi wa jimbo hilo, Christina Midelo, alisema kuwa Sospeter Kasawanga wa CCM alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura 2,310 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Pius Mwanisawa aliyepata kura 1,837. Jumla ya watu 11,165 walijiandikisha ambapo waliopiga kura ni 4,273 na kura 126 ziliharibika.

Alisema katika Kata ya Kabwe, mgombea wa CHADEMA, Asante Libinsha, alipata kura 1,953 na kumshinda mgombea wa CCM, Juma Milumba, aliyepata kura 1,713. Jumla ya watu waliopiga kura ni 3,614 kati ya 8,300 waliojiandikisha.
 
mwisho wa mechi matokeo yako kama hivi

chama cha mapinduzi (kampunila kijani lisilofilisika) 12

umoja wa upinzani(wasambaza sumu na fitna kwa wananchi dhidi ya serikali) 04
wamejitahidi vyama vinne average kila kimoja wapewe wadi moja.

na hata bado mapovu ya mdomo yatakutokeni mwaka huu.
 
Hivi Mtu ambaye alikuwa akileta breaking news za uchaguzi si alikuwa Mnyika!!! yuko wapi tena jamani?,,, mpaka tunapata habari za magazeti,,, si JF ndio ilikuwa ya kwanza kupata habari...

Anyway,,, kwa vyovyote vile upinzani unaimarika,,, ingawa sio kwa namna ambayo ni ya uhakika, hapana ni kwa namna ya kusema kwa kusema fulani hawezi automatically mimi naweza, yaani kusema fulani fisadi, automatically mio sio na mimi ni mlokole.

Lakini kama tukujumlisha kura zilizozesema CCM "NO" kwa vyovyote zitakuwa nyingi, ukilinganisha na uchaguzi wa 2005 ambayo haukuitendea haki, wabunge bomu waipata kura kwa sababu tu ni CCM.

The big problem hapa, hizi kura hazina tofauti na kura za urais za aliyekuwa Mh. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa vijana ambaye kura zake zilikuwa nyingi 1995 kwa kuwa mabomu yalikuwa mengi, alafu mwaka 2000 zikapungua kwa kuwa mabomu yalipungua...of course kwa sababu pia kaka Ben ali-deliver

Tunaomba sana Upinzani Ujijenge kwa Maslahi ya Nchi yetu,,, Mabomu is very short term strategy but of course necessary,,, we need sustainable strategy guys, we can't afford to wait!!
 
kitilime wapinzani walikuwa na viti sita katika kumi na sita sasa wameshinda vitatu na cha nne wamegaiwa wamepoteza viwili ndio wameimarika? au tfsiri ya kuimarika siku hizi ni kurudi nyuma?
 
kitilime wapinzani walikuwa na viti sita katika kumi na sita sasa wameshinda vitatu na cha nne wamegaiwa wamepoteza viwili ndio wameimarika? au tfsiri ya kuimarika siku hizi ni kurudi nyuma?

Nadhani namaanisha kwenye idadi ya kura (aggregate votes),,, yaani tuchukue kata zote,,, tuhesabu kura za Upinzani, na Za CCM. Lazima kutakuwa na kuimarika kwa kura za Upinzania,,,,

In terms of Viti vingapi, you may be right, lakini namsubiri mtu wa Mrengo mwingine kwanza... and I will comment accordingly.
 
sasa kitilime unazo takwimu zake? au niwekee wazi majina ya wadi zote niende kutafuta za mwaka 2005 kisha tuzitafute na za juzi tulinganishe.

hata hivyo kupoteza viti viwili ambavyo walivishikilia ni kurudi nyuma.

tuwasubiri, maana hii habari waliispin kwa hiyo wanaangalia watoke vipi LUNYUNGU, MKJJ, MNYIKA na kambi yenu njooni mutuwekee hesabu sawa, jee upinzani umeimarika au umeporomoka?
 
tuwasubiri, maana hii habari waliispin kwa hiyo wanaangalia watoke vipi LUNYUNGU, MKJJ, MNYIKA na kambi yenu njooni mutuwekee hesabu sawa, jee upinzani umeimarika au umeporomoka?

Nami nasubiri,

Meantime, Lazima upinzani ufanye kazi ya ziada kuhakikisha tume ya uchaguzi inawapa haki yao waTanzania walioko nje ya nchi ya kupiga kura at least by 2010,,, kuna kura nyingi sana za kina MKJJ, Mwafrika wa Kike, Kichwa Maji etc,,, binafsi nisingependa ziharibike...

Chama Makini lazima kitaleta analysis. give them time...
 
sasa kitilime unazo takwimu zake? au niwekee wazi majina ya wadi zote niende kutafuta za mwaka 2005 kisha tuzitafute na za juzi tulinganishe.

hata hivyo kupoteza viti viwili ambavyo walivishikilia ni kurudi nyuma.

tuwasubiri, maana hii habari waliispin kwa hiyo wanaangalia watoke vipi LUNYUNGU, MKJJ, MNYIKA na kambi yenu njooni mutuwekee hesabu sawa, jee upinzani umeimarika au umeporomoka?

Mtu wa Pwani:

.....chenga twawala!

Kabla ya Mechi(Ushindi wa mezani). Upinzani( TLP, chunya)-1 CCM 5(tulianza kushinda bao la mwanzo mwanzo kabisa, halafu yakatokea ya wapinzani kujitoa kiasi kikubwa wagombea wa CUF). Hapa kuna uzoefu fulani fulani tumeupata kwa chaguzi zijazo).

Mechi ilipoanza mpaka kipindi cha mwisho: Upinzani 3( TLP Sombetini, CHADEMA Songea Mjini na Kabwe) CCM 6( hii ni sawa na asilimia 50%; ni mwanzo mzuri kwamba chama tawala kinaweza kushindwa nusu ya uchaguzi wa moja kwa moja! Tena tukiwashinda mijini!, ni mwanzo mzuri wa ushirikiano).

Uchambuzi huu nimeufanya nikiwa sifahamu matokeo ya kata mbili- moja ni ya Moshi Vijijini(Vunjo) ambao uchaguzi umepangwa novemba. Na moja sifahamu matokeo yamekuwa nini huku kijijini nilipo).

Swala la kupoteza mbili. Ni kweli tunapaswa kuongeza nguvu zaidi katika kulinda goli letu. Lakini tumepoteza mbili, tumeongeza nne. Hivyo ni kama hatujapoteza ila tumeongeza mbili. Kama unatumia kigezo cha kuongeza namba na si kulinda maeneo. Hata hivyo, ni vyema upinzani tukaendelea kulinda kwa nguvu zote maeneo tunayoshinda.

Ila mechi ilikuwa nzuri, ni mwanzo mzuri. CCM ilipeleka mziki mkubwa ikiwemo mawaziri lakini bado wamehema.

Sasa tusubiri uamuzi wa mahakama, uchaguzi ukirudiwa- Mambo yatakuwaje?

Natabaruku, bado niko msamvu

JJ
 
Kilitime na Mtu wa Pwani:

Na haya yametokea chini ya Tume ya Uchaguzi isiyo huru, unajua kuwa uchaguzi wa Udiwani Wasimamizi wakuu wa Uchaguzi ni Wakurugenzi wa Manispaa(ambao ni watendaji wa serikali) na Maafisa watendaji wa Kata(ambao ni makada)?

Ushindi wa upinzani ni mtamu zaidi kwa kuwa ni wa nguvu ya umma. Si wa nguvu ya dola. Ukiona CCM inashindwa katika mazingira haya ujue kazi ilikuwa nzito. Sombeteni FFU ilibidi watawanye watu kwa mabomu, walitaka usiku kutangaza matokeo tofauti. Songea Mjini Nchimbi aliwekwa "mateka" ikabidi FFU watawanye wananchi. Ilikuwa kazi kweli kweli.

Hapa ni kwa wapinzani kujenga tu na kuendeleza ushirikiano; hakuna kulala..

Kata zote zijenge nguvu zaidi ya kisiasa kama walivyofanya Sombetini, Kabwe na Songea Mjini(Tarime style!)

Bado najiuliza ilikuwaje CHADEMA ikashindwa Namanyere..we had all the reasons to win.

I see change, it is just around the corner..

JJ
 
Na haya yametokea chini ya Tume ya Uchaguzi isiyo huru,

Mnyika,,,

Kama unavyofahamu mimi sio pendera fuata upepo,,,sikubali mambo kirahisi rahisi. Hebu naomba definition ya tume huru!!!

NB:
Remember Zanzibar walitafsiri tume huru kwa namna yao,,, Bunge la Jamhuri likatafsiri kwa namna nyingine,,,
 
Back
Top Bottom