PreGE2025 Wapinzani mna watanzania wengi nyuma yenu, changamkeni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sema CDM wenyewe wanakwambia watu wapewe ng'ombe wawili wawili yaan uchumi gan sijui heche anausemea jamaa ana utopian economy alafu anaongea kwa confidence
 

Ukiwa siyo mtu mnafiki, au ukiwa mkweli kabisa kabisa katika nafsi ya moyo wako, utakubaliana na Ukweli mchungu Sana kwamba huyu Mama Kamwe hawezi kupata Kura hata za Asilimia Kumi tu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao endapo kama kutakuwa na Tume ya Uchaguzi iliyo HURU kama ile iliyopo kule nchini Afrika Kusini.

Chini ya Tume ya Uchaguzi iliyo HURU kabisa kiutendaji:-
Kutakuwa na Demokrasia katika Uchaguzi,
Kura Zitapigwa Hadharani kila Mtu akiwa anaona kwa Macho yake yeye mwenyewe, Waandishi wa Habari wanaweza wakarekodi na kurusha mubashara kabisa mchakato wote kabisa wa Uchaguzi pamoja na zoezi zima la Upigaji kura na Uhesabiaji wake,
Wananchi wataweza Kuruhusiwa kuweza kuwepo katika Vituo vya Kupigia Kura ili waweze Kushuhudia kwa macho yao wenyewe jinsi zoezi la upigaji kura linavyoendelea na uhesabiaji wa Kura.

Endapo kama Mazingira ya Kidemokrasia ya namna hii yatakuwepo Kama vile inavyofanyika katika Chaguzi za kisiasa kule Afrika Kusini, basi naamini kwa dhati kabisa kwamba huyu Mama pamoja na Chama chake Kamwe hawataweza kushinda Uchaguzi na wala hawataweza kupata hata Asilimia Kumi tu za Kura kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
 
Kama tutashindwa kutumia nafasi mwaka huu basi inaweza kuchukua miaka 100 kufika katika kilele kama sasa 2015 tulichezea nafasi kwakumchukua fisadi sasa miaka 10 mbele Mungu ametupa nafasi ya pili chini ya Simba TAL kwa uwezo wake anaweza kuongoza hata kondoo naakakupa matokeo wiki moja kanda ya Nyasa milio kila kona 😂😂😂
 
Huwezi kumchagua na genge lake la mafisadi ya mali za umma
 
Vyeo vinapatikana kwa koo, ufisadi na rushwa na siyo uwezo wa mtu, wengine wote ni wasindikizaji, ilitakiwa vyeo vyote ukitoa cha Rais, Makamu na PM wengine wote waombe na kufanyiwa public interview Tanganyika ingekuwa kama Urusi kwa maendeleo
 
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Hata yule Babu anataka tume HURU 😆 Samia na Mchengerwa wamebaki pekeyao.
Your browser is not able to display this video.

NO REFORMS NO ELECTION LINDA DEMOKRASIA
 
Tatizo vyama ni vingi lakini vya upinzani havizidi vinne!
 
Vyeo vinapatikana kwa koo, ufisadi na rushwa na siyo uwezo wa mtu, wengine wote ni wasindikizaji, ilitakiwa vyeo vyote ukitoa cha Rais, Makamu na PM wengine wote waombe na kufanyiwa public interview Tanganyika ingekuwa kama Urusi kwa maendeleo
Alafu maskini ndio machawa wa "Unaupiga mwingi" na miitano Tena, hawajui wanajichimbia kaburi
 
Naam,hiyo ndo jeuri yao hakika, mabadiliko ya tume ni mhimu sana tu.
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka, ulitaka mtoto wa mwanasiasa afanye nini? We pambana hao uliowataja huwa wanagombea na kushinda. Pambana vinginevyo utabaki kulialia mpk unakufa hakuna wa kukuletea uongozi mezani kwako.
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka, ulitaka mtoto wa mwanasiasa afanye nini? We pambana hao uliowataja huwa wanagombea na kushinda. Pambana vinginevyo utabaki kulialia mpk unakufa hakuna wa kukuletea uongozi mezani kwako.
Nguvu ya wananchi inaweza waondoa madarakani. Haki ikiwepo, amani itatawala Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…