Friends and Enemies,
Maisha ya Wilbroad Slaa kisiasa,na kiuzalendo yalifika Kikomo pale ambapo aliwakana wapinzani wenzake enzi za Rais John Magufuli na kukimbilia mkate wa kuwa balozi huko Canada.
Wilbroad Slaa,wakati wapinzani wanapambania demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari na Utawala Bora katika awamu hii iliyopita,yeye aliwageuka na kutugeuka watanzania hadi kufikia hatua ya kusema kwamba hakuna haja ya katiba mpya,Rais JPM aachwe ainyooshe nchi.
Kama hiyo haitoshi, kipindi wenzake wamepewa kesi za kubumba na mwendazake ambapo hata hivyo Mh Rais Samia alikuja kuzifuta yeye aliwasagia kunguni na kusema hao siyo wapinzani,ni wapinga maendeleo.
Leo hii zama zimembadilikia na anaonekana kwenda kuozea selo hakuna hata chama Cha siasa kutoka upinzani kinachohangaika nae, Wilbroad Slaa amepuuzwa kama vile ambavyo yeye aliwapuuza wenzake.
Ama hakika kuimba ni kupokezana,Unafiki,Njaa na Uchu wa madaraka wa Wilbroad Slaa na tamaa zake za fisi zimepelekea awe na mwisho wa fedheha katika siasa za Tanzania...