Wapinzani na Rasimu ya Katiba: Jipangeni kutetea hoja kwa mantiki

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
USULI: Suala la katiba lilitolewa tahadhari nyingi kabla ya kuanza. Tulionya nia mbaya iliyokuwepo tukizingatia CCM haikuwa tayari kwa mabadiliko. Tukaonya hoja kutekwa nyara na serikali, wapinzani kuridhia kwenda Ikulu na miswada bungeni. Taratibu za kuandika katiba hazikufuatwa na hilo lilipaswa kuwa 'wake up call''. Wapinzani hawakuzingatia.

Sasa wameungana kuzuia mswada usisainiwe na rais baada ya kufanyiwa vitimbwi bungeni.
Pengine ushirika ulipaswa kuanza mapema ili kukabiliana na nia mbaya.
Pamoja na kuchelewa au kukosa maono bado wanaendelea na makosa waliyoyafanya mwazoni,kuimba nyimbo za CCM!

NYIMBO ZA CCM
Tume ya katiba imeshatoa rasimu ya muelekeo wa katiba mpya. Suala la serikali 2, mkataba na mengine hayamo.Kinachojadiliwa ni maboresho ya rasimu inayoongelea serikali 3 au basi kuvunja muungano kama haliwezekani.
CCM wanarudisha hoja ya serikali 2 makusudi kabisa wakivuta muda. (Tutaangalia mbele)

KUSUSIA BUNGE NA MSWADA.
Marekebisho ya sheria ya mchakato wa katiba yameletwa na serikali ya CCM kwa hofu ya kushindwa hoja

1. Mswada unasema kura katika bunge la katiba zipigwe kwa 'simple majority' na siyo 2/3 kwa kuelewa hoja za CCM haziwezi kupata 2/3 kutoka pande zote. Kinachotakiwa ni kupata kura hata moja tu zaidi ili kushinda.
Kwamba mustakabali wa nchi utaamuliwa na kura mbili au tatu na si wingi wa wananchi.
Hii itafanyika kwa kutumia mbinu, tuangalie hoja ya pili.

2. Kumpa rais uwezo wa kuchagua wajumbe 166 watiifu na kufanya idadi ya kura kufikia' simple majority'.
Kama bunge lina wajumbe 604, wajumbe 300 wakakataa au kukubaliana na rasimu kwa namna yoyote tofauti na CCM, wale 304 wa CCM watiifu ambao 166 ni kutoka kwa rais watafanya 304 na kushinda(watu 4 tu).
Ili kuchakachua matokeo kwa urahisi kitafanyika nini? Tuangalie sehemu ya 3

3. Tume ya Warioba imeambiwa ikome shughuli zake kabla ya bunge la katiba kinyume na sheria ya sasa.
Kwamba atakayetetea rasimu atatoka kule CCM wanakotaka. Ni wapi hapo? Jibu ni hili
a) Wajumbe wengi wa CCM wakiwemo 166 wa rais ambao ni watiifu kwake.
b) Watachagua Spika kutokana na majority ya CCM na kusukumiza hoja kwa kutumia Spika na wabunge wao.

Nini kitafuta?
Uchakachuaji wa aina mbili.
1. Kwamba rasimu itakayokuwa imetengenezwa na Warioba inaweza kupigwa chini au kufanyiwa mabadiliko makubwa kulingana na matakwa ya CCM ambao watakuwa wengi wakiwemo wajumbe binafsi wa rais 166.
2. CCM itakuwa na njia ya kushinikiza hoja ya serikali 2 ambayo wanaibembeleza iendelee endelee kutajwa ili wakati ukifika wasema majority wanataka serikali 2.
Kwa kutumia wajumbe wengi na Spika wao uchakachuaji utakuwa umetimia.
Rasimu ya CCM kwa jina la wananchi itapatikana!.

MAKOSA YA WAPINZANI
1. Hawaelezi kwa kina kwanini wamekataa mswada na kwanini kuna marekebisho wasiokubalina nayo na madhara yake ni nini kwao. Wao wamejikita katika idadi ya wajumbe 166. Hata kama watapewa idadi hiyo kwa jinsi wanavyotaka bado wanavikwazo kama nilivyosema 1,2 na 3 hapo juu.

Wanasimamia hoja ya znz kutoshirikishwa hoja ambayo wznz wenyewe wamegawanyika,wengine wakisema wameshirikishwa na wengine la.

2. Akina Tundu Lisu,Mbowe, Lipumba, Mbatia n.k. wameng'ang'ania wajumbe sawa kutoka Zanzibar, znz huru na hoja zingine zisizolingana na suala la mswada wanaougomea. Wengine wamezidi kujikita katika wimbo wa serikali 2 wa CCM kitu wasichopaswa kukiongela maana hakipo katika rasimu.

WAFANYE NINI?
Kwanza lazima wajue nini CCM imekusudia kabla ya kuanza kupambana nao majukwaani.
Pili, waeleze hoja kwa njia rahisi ili mwananchi wa kawaida aelewe na si kutumia vifungu na maneno yanayowachanganya.

Tatu, Wakati wanajipanga lazima wajue wanagomea nini na wanataka iweje.
Hadi sasa kusema wajumbe 166 au znz kutoshitrikishwa ndilo tatizo na kuacha hoja nyingine za msingi ni kupunguza nguvu ya hoja zao na kushindwa

Ndio maana tunasema kwa mwendo walio nao wanapaswa kujipanga na kuetete hoja zao kwa mantiki tena zikieleweka na average Tanzanian. Vinginevyo naona kama wanatwanga maji kwenye kinu.

Natumaini kuna maono tofati juu ya hili. Wanajamvi karibuni tujadili, tukosoane, tuelekezane kwa mustakabali wa taifa.

Mchambuzi JokaKuu Jasusi AshaDii gfsonwin Ngongo Bongolander Kimbunga Remote Zitto JJ Mnyika Nape Nnauye Mwita Maranya Mzee Mwanakijiji EMT Mag3 Zinedine The Big show Ritz Yericko Nyerere@Masopyakindi Fundi Mchundo Ngambo Ngali Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3,

Kwanza huu muungano ni wa vyama vya siasa au ni muungano wa Prof. Lipumba, Mbatia, Mbowe.

Ukiangalia msimamo wa CUF Tanzania Bara na CUF Zanzibar misimamo yao tofauti kwenye suala zima la Katiba.

Ukiangalia msimamo wa Tundu Lissu na Mbowe kuhusu Katiba hoja zao na suala la Zanzibar wapo tofauti.

Wapinzani wataweza kuwaongoza Watanzania kuelekea kwenye Katiba, wapinzani wanajua watanzania wanataka nini.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nikuite Mh kwa sababu umenikuna akili yangu,you deserve to be a great thinker. Hoja zako zinamashiko...wapinzani umewapa mwanga na wayforward nzuri sana ambayo in the other way wananchi wataelewa kama tu haya yatafanyika, congrats Mkuu:clap2::clap2::clap2:
 
hoja yako ni nzito, mimi binafsi nilikuwa sijaelewa vizuri wanapinga nini, hoja yao kubwa niliyosikia mara zote ni ya kwamba zanzibar haikushirikishwa vizuri kwenye utoaji wa maoni, sasa ni wa ngapi hawana taarifa za kutosha kama mimi? Nafikiri wapinzani tupinge vitu kwa hoja nzito kama na kuzifafanua kwa uzuri kama huyu jamaaa alivyofafanua hapa, Mshikamano mliouonyesha sasa ni mzuri kwa manufaa ya watanzania, naunga mkono hoja yako mkuu
 
Ndio maana tunasema ujumbe wao haupo clear kwa watu. Nina hakika mamia ya watu hawafahamu kwa undani kwanini wamegomea mswada na hoja zao ni zipi.
Ukweli ni kuwa hoja zao ni nyingi na nzito sana lakini hawaziweki katika lugha rahisi ya mawasiliano na kibaya wametumbukia katika shimo la malumbano badala ya ufafanuzi.
 
Mkuu Nguruvi3,

Kwanza huu muungano ni wa vyama vya siasa au ni muungano wa Prof. Lipumba, Mbatia, Mbowe.

Ukiangalia msimamo wa CUF Tanzania Bara na CUF Zanzibar misimamo yao tofauti kwenye suala zima la Katiba.

Ukiangalia msimamo wa Tundu Lissu na Mbowe kuhusu Katiba hoja zao na suala la Zanzibar wapo tofauti.

Wapinzani wataweza kuwaongoza Watanzania kuelekea kwenye Katiba, wapinzani wanajua watanzania wanataka nini.
Hoja nzito wanazo tena zenye mashiko sana, tatizo sijui kama walikaa pamoja na kuweka sawa kile wanachokitetea au kila mmoja alikuwa na hoja yake na kupitia jukwaa moja zinaelezwa.
Sina uhakika na hilo.

Ninakubaliana nawe pia kuwa kuna hoja ambazo sijui wapinzani wanasimamia wapi. Najaribu kumsoma Tundu Lissu naona amefikia mahali anajichanganya.
1. Yeye anadai muungano ni kiini macho na haupo hadi sasa. Ni kweli
2. Anadai znz washirikishwe katika katiba kama wabia sawa. Nina shaka kama hilo litafanyika kila sehemu au ni katika mafao tu, labda tuanzie na gharama za tume na bunge la katiba.

Lakini nashangaa pia Tundu anakuwa msemaji wa waznz wale wale anaosema hawataki muungano.
Tundu anataka washirikishwe kikamilifu na nyakati nyingine akisema wawe huru.
I mean ni ngumu kumwelewa Tundu kwa urahisi hasa mtu wa kawaida.
Labda wanajamvi watafafanua Tundu anasimamia wapi maana naona kama simwelewi.

Baada ya kusoma haya maalezo yako maswali haya ya mejitokeza?

Je Watanzania na viongozi wetu tulikuwa tunauelewa vizuri mchakato wa uundaji katiba kwa maana ya nadharia na kwa vitendo?

Kama rasimu imeshaelekeza serikali tatu, hii ni kutokana na maoni, na ikitokea katiba ipatikane hivyo, katiba ya tanganyika itapatikana vipi na kwa muda gani? Naya znz itarekebishwa vipi na kwa muda gani tukizingatia mwakani kuna chaguzi?

Hiyo katiba mpya inatarajiwa ianze kutumika rasmi lini?

Kuna maoni kama muundo wa serikali yaani mawaziri wasiwe wabunge nk. Katiba ikishapitishwa na kuanza kufanya kazi pengine tumeambiwa mwezi wa 4 mwakani. Utekelezaji wake utawezekana vipi?

Mtu ukisema huu mchakato umenza na utaishia kama ulivyo anza utakuwa umekosea? Yaani serikali mbili.
 
Swali la kuelewa mchakato lina sehemu mbili. Wapo walioelewa mchakato na wakatoa maoni yao.
Viongozi walielewa lakini utamaduni wa kufanya mambo kwa ulaghai ndio umetufikisha hapa.

Suala la katiba ya Tanganyika linafanyiwa hila ili muda upite na isemwe haliwezekani.
Hapa ndipo wapinzani wanapaswa kujiuliza kama madai dhidi ya znz huru ni muhimu kuliko katiba ya Tanganyika.

Katiba kupatikana kwa sasa ni kama ndoto na hata ikipatikana itakuwa ile iliyotengenezwa nao na si wananchi.
 
Na kwa kuongezea nafikiri uwanja wa Wapinzani kuelezea hoja zao waliufanya wenyewe kuwa finyu sana.
Mathalani ilitakiwa mwanzo kabisa kabla muswada haujaanza kujadiliwa Waziri kivuli autolee ufafanuzi wa kina na kila
udhaifu uwekwe hadharani, hapa wangepata "political gain" kwenye siasa za Kitaifa kama Watu makini wanaotarajia kuongoza dola.

Nachokiona ni kama hawa wote wanategemea watu wawili watatu waseme nao wafuate mkumbo.

Pili, hawakujadili kwa kina namna Tume ya Warioba ilivyominywa pale ambapo inatakiwa kuvunjwa ili kupisha Bunge la Katiba. Wangelisemea hili kwa lugha nyepesi wangepata uungaji mkubwa zaidi wa Wananchi, na hapa wangeonekana si tu wanajali maslahi ya upande mmoja (kwa maana ya kusisitiza "Utaifa") bali wangeonekana wanaitetea Tume na kwamba CCM inaivuruga kwa maslahi yake na siyo ya Kitaifa.

Tatizo la Wabunge wengi ikiwemo wa Upinzani hawajishughulishi kusoma na kuchambua makabrasha kabla ya kuzungumza. Nimewaona mara nyingi Dodoma hata nyakati ambazo kuna hoja nyeti inaletwa kesho Bungeni wao jioni mpaka usiku wa manane wanapiga pombe!!
 
Kimsingi sio wapinzani tu wajipange, wewe, mimi, yeye, wao, na wote wapenda mabadiliko ni jukumu letu kujipanga kukwamua mchakato ambao umeshakwenda kombo. Majibu kama yale ya Chikawe ni ishara ya mtu aliyekutwa na mkwe with pants down. Waziri wa sheria na nasikia alipata kusoma sheria, anasema haoni matatizo kwanye mswada waliopitisha kishabiki. Hiyo ndio kauli ya Wasira, Lukuvi, Werema na wengine wengi ambao hadi sasa sijui wanatumia nini kufikiri. Tatizo la CCM wanafikiri ukishapewa uwaziri basi hata kama ulikuwa tabula rasa unapewa akili. Kumbe ukweli ni kwamba ka ni kilaza hata ukapewa ufalme bado we ni kilaza. Matokeo yake ni kutumia mamlaka kuficha ukilaza wako. Wanachofanya wapinzani ni mkakati wa wa kukabili adui kwa kutengeneza maarafiki wengi kuliko maadui. Kama forum itakapopatikana nondo ziko tayari tena very systematic and straight to the enemy's heart. Let's mobilize support to this noble course towards achievement of democratic constitution.
 
No doubt that where the opposition parties are weak, the ruling party is more tempted to abuse power. Hata hivyo, nadhani kuwa tatizo kubwa tulilo nalo hapa nchini siyo tuu kuwa na vyama vingi vya upinzani ambavyo baadhi yao havina hata mwelekeo.

Pia tuna tatizo la uwepo wa chama kikongwe ambacho ndani yake hakuna "loyal opposition". In fact, chama hicho kikongwe hakiruhusu "loyal opposition" ndani yake. Kuwa na chama tawala ambacho ndani yake hakuna "loyal opposition" ni janga kubwa sana kwa taifa.

Kama hakuna "loyal opposition" ndani ya chama, ina maana kuwa maamuzi yatakuwa yanafanyika kwa manufaa ya chama. Kutakuwa hakuna loyalty to the fundamental interests and principles of the nation as a whole, but to the interests and principles of the ruling party.

Legislative debate will be one-sided kwa sababu chama kitakuwa hakina genuine loyal opposition ndani yake. Ndiyo maana wabunge wa chama tawala wamepitisha sheria ambayo itampa Rais mamlaka ya kuteua wajumbe wake binafsi 166 kwenye Bunge la Katiba bila hata kuhoji. Kwani kinachotengenezwa ni Katiba ya Rais au ya Tanzania?

Of course, vyama vya upinzani vina matatizo yao, na process nzima ya ya katiba mpya ina walakini mkubwa, lakini wabunge wa chama tawala waliopitisha hiyo sheria are a disgrace to the nation. Ndiyo hao hao waliopitisha sheria ya kodi za simu na internet and they managed to get away with it.

Sheria mama ya nchi haitengenezwi kihuni hivyo. Ndiyo maana niliikataa huu mchakato wa katiba mpya tokea mwanzoni kabisa. Whether I was wrong, time will tell.
 
Nguruvi, nashukuru sana kwa kukumbushia jambo hili. Mimi mwenzenu labda nina tabia mbaya - kurudia sana kitu kile kile kwa watu wale wale siwezi kwa kweli. Hii ndiyo sababu niliachana na hoja za Mohammed Said kwa sababu hata mbuzi ukimpigia gitaa anaweza kutikisa mkia!

Suala la Katiba Mpya ni suala ambalo wapinzani walipewa kamba wakaweka fundo halafu wakaining'iniza mtini. Kwenye sheria ya Katiba Mpya wakaambiwa ingizeni vichwa vyenu wakaingiza wakitegemea kuwa CCM watasimama kuwasaidia wasianguke na kuning'inia. Tatizo ni kukosa mkakati mzuri; si kwa sababu hawajui bali kwa sababu wao wanataka kuwa wanasiasa, wao wanamkakati, wao wabunge, wao viongozi wa chama wao kila kitu - the jack of all trades. Matokeo yake hata wakikwama kama walivyokwama sasa hakuna wa wakuwawajibisha au kuwasahihisha!

Walikosea walipokubali mchakato wa CCM wa Katiba Mpya; walikosea walipokubali maneno kuwa ni "katiba ya wote"; na walifanya makosa walipokubali sheria ile ya kwanza kabisa - kabla ya mabadiliko. Mtu yeyote aliyesoma ile sheria aliweza kuona mapungufu na laghai iliyokuwa mbele na bado haijakoma.

Hii ndio sababu mimi kwa upande wangu na kwa kufuata dhamira yangu nilikataa kutambua mchakato huu na nilisema wazi kuwa siyo halali. Yaani haukuwa halali kwa Katiba ya sasa (chini ya Ibara ya 98) na haukuwa halali hata kwa sheria na mantiki ya sheria waliyopitisha CCM. Matatizo yote haya tunayoyana na tutayaona kwenye Bunge lao la Katiba na hata kwenye kura ya maoni (wapinzani wataanza kulalamika kwanini katiba mpya ipite kwa asilimia 50 tu kana kwamba kipimo hicho kitakuwa kimeingizwa huko mbeleni!) yanatokana na wapinzani kukubali ajenda yao ibebwe na CCM!! Hili lilikuwa ni kosa kubwa la Kimkakati na sasa wanalilipia.

Hata hivyo, tatizo lililoko kwa wapinzani sasa hivi ni kuwa wanaonekana kama wanataka mchakato unaowafaa wao au unaokubaliana na wao. Hii si haki sasa. Kama walikubali sheria, wakaingia na kushiriki sasa hivi hawawezi kuruka sehemu ya mchakato kwa sababu hauendi walivyotarajia! Unapokubali kushiriki mchezo ni LAZIMA uelewe sheria za mchezo sasa ukakubali kushirikia na kucheza kipindi cha kwanza sasa kinapokuja kipindi cha pili na tayari ushafungwa magoli kadhaa huwezi kuanza kulalamika kuwa sheria siyo nzuri! Kwani zilianza kuwa mbaya baada ya wewe kufungwa!?

Wapinzani wamejitokeza na kuunga mkono rasimu ya Katiba kwa sababu ina mambo mazuri wanayokubaliana nayo? Hawatuambii mambo hayo wanayokubaliana nayo yametoka kwa Tume ya Warioba au kwa wananchi? Maana kama yalitoka kwa wananchi ni wananchi gani hawa? Ni hawa chini ya asilimia 1 ya wapiga kura wanaweza kweli kuamua hatima ya nchi nzima? Au yanatoka kwa wasomi (kina Warioba) ambao wanaamini wanajua Watanzania wanahitaji nini.

Watoke vipi?
Well hii kwa kweli ni swali gumu. Sasa hivi sioni njia nyingine yeyote ya kubadilisha mwelekeo wa mchakato huu. Hata maandamano wanayopanga kwa kweli hayana sababu; Wassira kawashauri vizuri tu kuwa kama wanaona sheria siyo nzuri hivyo waandike wao mabadiliko ya sheria wanayotaka na wayapeleke Bungeni njia za kidemokrasia zitumike kupitisha au la. Kwenda kwa wananchi na kumtegemea Rais kutaturudisha kule kule kwa wao kuitwa tena Ikulu (na Wassira kawaambia hawaaliki tena Ikulu!).

Ndio maana sasa hivi hili la mchakato wa Katiba miye yangu macho kwani hakuna lolote linalofanywa na CCM na serikali yake wapinzani hawakulijua 2012. Waliamini wanaweza kucheza na nyigu kama kucheza na kipepeo.
 
Mkuu wewe ndiyo huna hoja hata chembe muungano wenyewe wa mbowe mbatia na lipumba halafu usipende kupotosha rasimu bado haijatoa msimamo juu ya serikali ngapi zinafaa ila ni mapendekezo tu.
 
Mkuu nianze ulipomalizia.
Kuanzia siku ya kwanza nilikataa kabisa mchakato. Nadhani rekodi zitatuhukumu na historia itatusuta kwa hilo kama likifanikiwa, historia itatutetea na rekodi kushadidia kama litashindikana.

Nilisema haiwezekani CCM na Kikwete waliogoma kuandika katiba wabadilike siku moja.
Lipo jambo. Hakuna mahali penye rekodi ya JK kuongelea katiba katika uhai wake kisiasa isipokuwa baada ya kuwa rais. Leo anaaminika kwa lipi. Heri ya Warioba maana kumbu kumbu zinaonyesha alishawahi kukataa katiba mpya akiwa mwanasheria wa serikali. Huenda uzee umekuwa dawa.

Tulisema mchakato wa katiba unahusu wananchi, serikali inaanda mazingira mazuri.
Sasa hivi serikali ndiyo inaanda katiba na wananchi kupitia wabunge wao wanasingiziwa walishirikishwa.

Kuhusu Wabunge wa CCM, hao wote wameingia katika rekodi ya aibu na usaliti wa umma.
Wabunge wa CCM wanaweza kuuza nchi kwa gharama yoyote ili mradi asiwepo anayepoteza Ubunge.

Huwezi kuamini kuna wasomi wa kila aina, kwa woga tu wa nafasi za kunyooshewa vidole wameweka akili na maarifa yao ukumbini mwa nyumba ili mradi tu wakae kitako na kusomeshwa na Nape Nnauye.
Ukiangalia wasomi wa CCM na jinsi wanavypoigishwa kwata left and right na Lukuvi utajiuliza kama elimu ina msaada kwa maisha ya Mtanzania.

Kuhusu kukokosekana kwa 'loyal opposition' pamoja na madhara yake kitaifa hilo acha liwepo. Udhaifu wa CCM ni kutokana na kukosekana kwa loyal opposition na bora itokee ili tuisahau kwasababu hakuna kipya zaidi ya kuvurunda kama suala la katiba linavyoonekana.
 
Swala la katiba siyo swala la kushinikizwa na akina mbowe ni swala ambalo liko na taratibu zake ndizo zifuatwe kuvuta bangi na kufoka majukwaani hakuna mpango wa maana.
 
USULI: Suala la katiba lilitolewa tahadhari nyingi kabla ya kuanza. Tulionya nia mbaya iliyokuwepo tukizingatia CCM haikuwa tayari kwa mabadiliko. Tukaonya hoja kutekwa nyara na serikali, wapinzani kuridhia kwenda Ikulu na miswada bungeni. Taratibu za kuandika katiba hazikufuatwa na hilo lilipaswa kuwa 'wake up call''. Wapinzani hawakuzingatia.

Sasa wameungana kuzuia mswada usisainiwe na rais baada ya kufanyiwa vitimbwi bungeni.
Pengine ushirika ulipaswa kuanza mapema ili kukabiliana na nia mbaya.
Pamoja na kuchelewa au kukosa maono bado wanaendelea na makosa waliyoyafanya mwazoni,kuimba nyimbo za CCM!

NYIMBO ZA CCM
Tume ya katiba imeshatoa rasimu ya muelekeo wa katiba mpya. Suala la serikali 2, mkataba na mengine hayamo.Kinachojadiliwa ni maboresho ya rasimu inayoongelea serikali 3 au basi kuvunja muungano kama haliwezekani.
CCM wanarudisha hoja ya serikali 2 makusudi kabisa wakivuta muda. (Tutaangalia mbele)

KUSUSIA BUNGE NA MSWADA.
Marekebisho ya sheria ya mchakato wa katiba yameletwa na serikali ya CCM kwa hofu ya kushindwa hoja

1. Mswada unasema kura katika bunge la katiba zipigwe kwa 'simple majority' na siyo 2/3 kwa kuelewa hoja za CCM haziwezi kupata 2/3 kutoka pande zote. Kinachotakiwa ni kupata kura hata moja tu zaidi ili kushinda.
Kwamba mustakabali wa nchi utaamuliwa na kura mbili au tatu na si wingi wa wananchi.
Hii itafanyika kwa kutumia mbinu, tuangalie hoja ya pili.

2. Kumpa rais uwezo wa kuchagua wajumbe 166 watiifu na kufanya idadi ya kura kufikia' simple majority'.
Kama bunge lina wajumbe 604, wajumbe 300 wakakataa au kukubaliana na rasimu kwa namna yoyote tofauti na CCM, wale 304 wa CCM watiifu ambao 166 ni kutoka kwa rais watafanya 304 na kushinda(watu 4 tu).
Ili kuchakachua matokeo kwa urahisi kitafanyika nini? Tuangalie sehemu ya 3

3. Tume ya Warioba imeambiwa ikome shughuli zake kabla ya bunge la katiba kinyume na sheria ya sasa.
Kwamba atakayetetea rasimu atatoka kule CCM wanakotaka. Ni wapi hapo? Jibu ni hili
a) Wajumbe wengi wa CCM wakiwemo 166 wa rais ambao ni watiifu kwake.
b) Watachagua Spika kutokana na majority ya CCM na kusukumiza hoja kwa kutumia Spika na wabunge wao.

Nini kitafuta?
Uchakachuaji wa aina mbili.
1. Kwamba rasimu itakayokuwa imetengenezwa na Warioba inaweza kupigwa chini au kufanyiwa mabadiliko makubwa kulingana na matakwa ya CCM ambao watakuwa wengi wakiwemo wajumbe binafsi wa rais 166.
2. CCM itakuwa na njia ya kushinikiza hoja ya serikali 2 ambayo wanaibembeleza iendelee endelee kutajwa ili wakati ukifika wasema majority wanataka serikali 2.
Kwa kutumia wajumbe wengi na Spika wao uchakachuaji utakuwa umetimia.
Rasimu ya CCM kwa jina la wananchi itapatikana!.

MAKOSA YA WAPINZANI
1. Hawaelezi kwa kina kwanini wamekataa mswada na kwanini kuna marekebisho wasiokubalina nayo na madhara yake ni nini kwao. Wao wamejikita katika idadi ya wajumbe 166. Hata kama watapewa idadi hiyo kwa jinsi wanavyotaka bado wanavikwazo kama nilivyosema 1,2 na 3 hapo juu.

Wanasimamia hoja ya znz kutoshirikishwa hoja ambayo wznz wenyewe wamegawanyika,wengine wakisema wameshirikishwa na wengine la.

2. Akina Tundu Lisu,Mbowe, Lipumba, Mbatia n.k. wameng'ang'ania wajumbe sawa kutoka Zanzibar, znz huru na hoja zingine zisizolingana na suala la mswada wanaougomea. Wengine wamezidi kujikita katika wimbo wa serikali 2 wa CCM kitu wasichopaswa kukiongela maana hakipo katika rasimu.

WAFANYE NINI?
Kwanza lazima wajue nini CCM imekusudia kabla ya kuanza kupambana nao majukwaani.
Pili, waeleze hoja kwa njia rahisi ili mwananchi wa kawaida aelewe na si kutumia vifungu na maneno yanayowachanganya.

Tatu, Wakati wanajipanga lazima wajue wanagomea nini na wanataka iweje.
Hadi sasa kusema wajumbe 166 au znz kutoshitrikishwa ndilo tatizo na kuacha hoja nyingine za msingi ni kupunguza nguvu ya hoja zao na kushindwa

Ndio maana tunasema kwa mwendo walio nao wanapaswa kujipanga na kuetete hoja zao kwa mantiki tena zikieleweka na average Tanzanian. Vinginevyo naona kama wanatwanga maji kwenye kinu.

Natumaini kuna maono tofati juu ya hili. Wanajamvi karibuni tujadili, tukosoane, tuelekezane kwa mustakabali wa taifa.

Mchambuzi JokaKuu Jasusi AshaDii gfsonwin Ngongo Bongolander Kimbunga Remote Zitto JJ Mnyika Nape Nnauye Mwita Maranya Mzee Mwanakijiji EMT Mag3 Zinedine The Big show Ritz Yericko Nyerere@Masopyakindi Fundi Mchundo Ngambo Ngali Mchambuzi

Huu ndiyo uchambuzi yakinifu. Well done. Ni elimu pia kwa wengine ambao hawakuwa kwenye mstari.....twenzetu...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wewe ndiyo huna hoja hata chembe muungano wenyewe wa mbowe mbatia na lipumba halafu usipende kupotosha rasimu bado haijatoa msimamo juu ya serikali ngapi zinafaa ila ni mapendekezo tu.
Hoja yako nzima ipo wapi kama hakuona chembe? Rasimu imetoka na mapendekezo kwa ajili ya kuangalia na kuboresha kwa mujibu wao na si mimi. Wamekubaliana kuwa kwa kuzingatia tume zilizotangulia na maoni ya wananchi suala la serikali 1,2 au mkataba ni nje.
 
Nguruvi, nashukuru sana kwa kukumbushia jambo hili. Mimi mwenzenu labda nina tabia mbaya - kurudia sana kitu kile kile kwa watu wale wale siwezi kwa kweli. Hii ndiyo sababu niliachana na hoja za Mohammed Said kwa sababu hata mbuzi ukimpigia gitaa anaweza kutikisa mkia!

Suala la Katiba Mpya ni suala ambalo wapinzani walipewa kamba wakaweka fundo halafu wakaining'iniza mtini. Kwenye sheria ya Katiba Mpya wakaambiwa ingizeni vichwa vyenu wakaingiza wakitegemea kuwa CCM watasimama kuwasaidia wasianguke na kuning'inia. Tatizo ni kukosa mkakati mzuri; si kwa sababu hawajui bali kwa sababu wao wanataka kuwa wanasiasa, wao wanamkakati, wao wabunge, wao viongozi wa chama wao kila kitu - the jack of all trades. Matokeo yake hata wakikwama kama walivyokwama sasa hakuna wa wakuwawajibisha au kuwasahihisha!

Walikosea walipokubali mchakato wa CCM wa Katiba Mpya; walikosea walipokubali maneno kuwa ni "katiba ya wote"; na walifanya makosa walipokubali sheria ile ya kwanza kabisa - kabla ya mabadiliko. Mtu yeyote aliyesoma ile sheria aliweza kuona mapungufu na laghai iliyokuwa mbele na bado haijakoma.

Hii ndio sababu mimi kwa upande wangu na kwa kufuata dhamira yangu nilikataa kutambua mchakato huu na nilisema wazi kuwa siyo halali. Yaani haukuwa halali kwa Katiba ya sasa (chini ya Ibara ya 98) na haukuwa halali hata kwa sheria na mantiki ya sheria waliyopitisha CCM. Matatizo yote haya tunayoyana na tutayaona kwenye Bunge lao la Katiba na hata kwenye kura ya maoni (wapinzani wataanza kulalamika kwanini katiba mpya ipite kwa asilimia 50 tu kana kwamba kipimo hicho kitakuwa kimeingizwa huko mbeleni!) yanatokana na wapinzani kukubali ajenda yao ibebwe na CCM!! Hili lilikuwa ni kosa kubwa la Kimkakati na sasa wanalilipia.

Hata hivyo, tatizo lililoko kwa wapinzani sasa hivi ni kuwa wanaonekana kama wanataka mchakato unaowafaa wao au unaokubaliana na wao. Hii si haki sasa. Kama walikubali sheria, wakaingia na kushiriki sasa hivi hawawezi kuruka sehemu ya mchakato kwa sababu hauendi walivyotarajia! Unapokubali kushiriki mchezo ni LAZIMA uelewe sheria za mchezo sasa ukakubali kushirikia na kucheza kipindi cha kwanza sasa kinapokuja kipindi cha pili na tayari ushafungwa magoli kadhaa huwezi kuanza kulalamika kuwa sheria siyo nzuri! Kwani zilianza kuwa mbaya baada ya wewe kufungwa!?

Wapinzani wamejitokeza na kuunga mkono rasimu ya Katiba kwa sababu ina mambo mazuri wanayokubaliana nayo? Hawatuambii mambo hayo wanayokubaliana nayo yametoka kwa Tume ya Warioba au kwa wananchi? Maana kama yalitoka kwa wananchi ni wananchi gani hawa? Ni hawa chini ya asilimia 1 ya wapiga kura wanaweza kweli kuamua hatima ya nchi nzima? Au yanatoka kwa wasomi (kina Warioba) ambao wanaamini wanajua Watanzania wanahitaji nini.

Watoke vipi?
Well hii kwa kweli ni swali gumu. Sasa hivi sioni njia nyingine yeyote ya kubadilisha mwelekeo wa mchakato huu. Hata maandamano wanayopanga kwa kweli hayana sababu; Wassira kawashauri vizuri tu kuwa kama wanaona sheria siyo nzuri hivyo waandike wao mabadiliko ya sheria wanayotaka na wayapeleke Bungeni njia za kidemokrasia zitumike kupitisha au la. Kwenda kwa wananchi na kumtegemea Rais kutaturudisha kule kule kwa wao kuitwa tena Ikulu (na Wassira kawaambia hawaaliki tena Ikulu!).

Ndio maana sasa hivi hili la mchakato wa Katiba miye yangu macho kwani hakuna lolote linalofanywa na CCM na serikali yake wapinzani hawakulijua 2012. Waliamini wanaweza kucheza na nyigu kama kucheza na kipepeo.
Kulikuwa na viashiria vyote na maonyo kuhusu suala hili.
Nakumbuka tuliuliza hivi rekodi ya JK kuhusu katiba ilikuwaje huko nyuma.
Hakuna mahali katika umri wa rais kisiasa alipowahi kunukuliwa akiongelea katiba. Wema huo ulianzia wapi?

Tukasema CCM haikuwa na manifesto ya katiba. Leo hoja ya mtu inakuwaje hoja ya chama?
Hakuna kikao chochote cha CCM kilichowahi kuzungumzia jambo hilo, vipi CCM iongoze mabadiliko isyoyajua?

Tukasema pongezi hazifai JK hana nia njema. Wapinzani acheni majagi ya juisi za maembe ya Mkuzi na Kwedikwazu.Susieni mswada wa kwanza ili mchakato utokane na wananchi na si serikali.
Yote hayo yakapuuzwa.

Tunashuhudia mambo ya kuchanganya, ujumbe wao ni wa kuparaganyika na ni ngumu kuelewa wanasimama wapi na kusimamia nini kwasababu tayari wameshazingirwa. Sad! Ngumu kumesa.

Maoni yaliyomo kwenye rasimu ni maoni ya wananchi hasa hili serikali tatu, lazima ya heshimiwe.
 
Back
Top Bottom