Nimeupenda huu Uchambuzi makini na wa kina wa bwana Nguruvi3.Ni kweli kwamba wanachofanya CHADEMA na Wapinzani wengine sijui kama kitaleta matokeo yanayotarajiwa.Kosa lilifanyika tangu awali pale walipokubali kwenda Ikulu kujadiliana na Rais kuhusu ile rasimu ya kwanza ambayo ilisainiwa kuwa sheria.Ni lazima tukiri kuwa hapa Kambi ya Upinzani ilionyesha uchanga wao katika siasa za Nchi hii.Kwa CHADEMA kukubali mwaliko wa Rais na Mwenyekiti wa Chama ambacho mwanzoni hakikuwa tayari kabisa kukubaliana na hoja ya Katiba mpya kwenda kujadiliana na kudhani kuwa angewafanyia yale wayatakayo!!?CCM walijua walichokuwa wanakifanya na kwa bahati mbaya sana kwamba CHADEMA hawakung'amua mtego huu wa CCM japo tuliokuwa huku mitaani tulijuwa nini hasa kitakachowapata CHADEMA mbeleni ambacho ni kugeukwa.Chanzo cha CHADEMA kuyumba katika hoja nyingi walizozianzisha ni kwasababu wamekosa Kiongozi makini.Natamani kama Dr Slaa angekuwa Bungeni na kuongoza Kambi ya Upinzani nadhani Bunge lingependeza kwa vita vya hoja nzito.