Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimeona kwenye mitandao ya kijamii wapinzani na wanaharakati wakishambulia na kulaumu tamko la ubalozi wa Marekani kuhusu kukamatwa na kuwachiwa kwa viongozi wa CHADEMA kwamba ni tamko dhaifu sana lakini zaidi wakiilamu Marekani na Washirika wake Ulaya kutoweka shinikizo la kutosha kwa serikali ya Tanzania kuhusiana na masuala ya demokrasia.
Huku ni ukosefu mkubwa sana wa uelewa wa geopolitics hasa ulewa kuhusiana na nafasi ya Tanzania kwa Marekani.
Ili kutoendelea na hizi lawama zisizo za msingi ni muhimu kufahamu haya
Tanzania sio mshirika muhimu wa kimkakati wa Marekani kwa Africa katika uchumi na usalama wa taifa. Hatuna rasilimali muhimu kwa wingi ambazo zinaivutia sana Marekani, hatuna biashara kubwa na Marekani na pia masuala ya ugaidi na dawa za kulevya sio masuala makubwa hapa nchini.
Tanzania sio mmojawapo ya mataifa mengi ya Africa yaliyo karibu kiutamaduni na Marekani. Siasa za ujamaa ziliufanya muelekeo wetu kuwa wa siasa za Mashariki/ Ukomunisti na imetufanya kuwa karibu zaidi na China, hata chama tawala mshirika wake mkubwa wa nje ni chama cha CCP cha China.
Tanzania sio jirani na Marekani, ujirani ni jambo muhimu sana kwenye geopolitics. Kama tungekuwa karibu na Marekani tungeweza kutazamwa kwa jicho la ziada.
Marekani inapitia wimbi la siasa za kujitenga(isolationism) na hivyo sio rahisi kujiingiza sana kwenye siasa za ndani za nchi nyingine.
Marekani inapitia changamoto kubwa ya ukuu wake/hegemony duniani baada ya vita vya Urusi na Ukraine. Marekani ilipigwa na butwaa baada ya kuona nchi nyingi za Africa zikiunga mkono au kubaki neutral katika uvamizi wa Urusi kwa Ukraine. Kuna sauti za raia katika nchi nyingi za Africa wanafurahia hili kwa sababu tu wanaamini ni "balance of powers". Marekani Isengetaka kuendelea kutibua sehemu ambazo bado inakubalika na watawala.
Jambo muhimu zaidi ni bora kufahamu Marekani inapokuwa nje ya taifa lake demokrasia sio kipaumbele kwake bali maslahi ya taifa lake hasa ya usalama na uchumi ndio vitu muhimu zaidi. Ndio maana kuna nchi nyingi sana ambapo inashirikiana na tawala za kiimla mfano Saudi Arabia, Misri na Angola.
Mwisho pia Marekani imeanza kukubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwalazimisha ng'ombe kunywa maji mtoni. Marekani kila raia anaamini katika demokrasia ila wanapishana tu katika sera na itikadi. Katika taifa ambalo kuna raia wengi hawaamini katika demokrasia, wengine wanawazia utawala wa sharia na wengine wanaona uimla unawafaa zaidi kwa sababu wanaamini demokrasia inachelewesha na kukwamisha baadhi ya mambo muhimu huku ikiwaleta pia mambo wasiyoyahitaji unafanyaje??