Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Naomba nitoe wito kwa wanasiasa upinzani pamoja na wanaharakati, waombe kibali cha kufanya maandamano ya amani kushinikiza uwazi wa mikataba ukiwemo mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Mradi huu ni mkubwa sana na kwa maana hiyo, unaweza kuleta matokeo makubwa kwa nchi yetu ambayo yanawe kuwa ni chanya( positive) au hasi(negative) kwa nchi yetu9 hivyo hatupawi kukaa kimya.
Mradi huu ukiwa na matokeo chanya, utafaidisha mpaka vitukuu wetu, na ukiwa na matokeo hasi, basi utaathiri mpaka vitukuu wetu pia kwahiyo ni lazima sisi wananchi tushirikishwe.
Tungekuwa na Bunge imara, tungeshirikishwa kupitia wawakilisha wetu (wabunge) , ila kwakuwa hatuna Bunge la aina hiyo(kwa mtazamo wangu), basi mkataba uwekwe wazi kwa umma na wananchi tutoe maoni yetu kama mradi huo uanze au vinginevyo.
Kamwe tusiwaachie wanasiasa waaamue peke yao jambo kubwa na nyeti kama hili hasa ukizingatia wanasiasa wetu wmekosa msimamo katika mambo nyeti kama haya. Zaidi wao huangalia watawala wameegemea upande gani na wao huunga mkono mawazo yao.
Kujadili huu mradi pasipo kujua nini hasa kimo katika huo mkataba huku wengine wakiupinga na wengine wakiutetea,ni uwendawazimu na ujinga mtupu na zaidi ni kupotezeana muda.
Bila shinikizo, tutajadili wee halafu tutachojadili hakitabadilisha kitu chochote, na mwisho wa siku, wataingia makubaliano wanayoyajua wao huku sisi tukibaki kuomba Mungu mkataba uwe fair kwa pande zote( kelele zote hizi zitakuwa ni sawa na kelele za chura ambazo hazimzui Tembo Kunywa maji).
Hivyo, natoa wito wa kufanyika maandamano ya amani kutaka uwazi juu ya mkataba huu vinginevyo tukubali matokeo hapo baadae.
Kumbukeni ya gesi ya Mtwara na maneno mazuri ya watawala wakati ule- Tanzania ya uchumi wa gesi.