Wapinzani tusimame pamoja kwenye miradi ya nchi tuikosoe Serikali inapokosea

Wapinzani tusimame pamoja kwenye miradi ya nchi tuikosoe Serikali inapokosea

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2019
Posts
1,524
Reaction score
4,477
Tuungane pamoja kuiombea na kuitetea miradi mikubwa kama:

SGR
STIGLERS GORGE
MIUNDOMINU
UMEME
MAJI
HOSPITALI
SHULE

Na miradi mingine mikubwa kama:

Ubungo Interchange.
Salender Bridge
Busisi Bridge
Meli nk

Tukiendelea kuipinga serikali hata kwenye mambo ya maana matokeo yake inatumia nguvu ya ziada kukuadhimu ili kulinda masilahi ya wengi.

Imefikia hatua kabisa mpaka kutengeneza upinzani mpya maana uliopo haujui unataka nn unashiriki kuihujumu nchi moja kwa moja.

Wapinzani kati ya watanzania mill50+ wako wengi wanaotamani kutoa mchango wao kwenye maendeleo ya nchi yao bila kuiumiza Serikali na bila kuiumiza nchi.
 
Boss Nigrastratatract Kunywa Fanta Kubwa hapo kwa Mangi, nakuja kulipa, Akupe na Doom ya kuuwa nyuki.

Naunga Mkono Hoja, Kwenye Interest za Nchi, Tunatakiwa tuwe kitu kimoja, Siasa tuweke pembeni.
Najua Maumivu ya wengine wanayopitia mpaka wanaombea mpaka Interest za Nchi zisifanikiwe tu kwa sababu tu Watawala wamekuwa na Mitazamo chanya kwao.

Ifike mahali pia Jamhuri na Serikali kuacha ku deal na Sisimizi, Mimi nafananisha Jamhuri aka Serikali na Tembo na Wapinzani au Wakosoaji kama Sisimizi, waache watu waongee, waache watu watoe maoni na ushauri wao, as long havunji sheria, wachiwe tu, Watu wakiwa huru, ni afya kwa Taifa.
 
Tungekuwa na wapinzani wenye maono kama yako, hakika tungekuwa tunakimbizana na South Africa sahivi na #covid19 tungeshaishinda zamani.

High five mkuu.
 
WAPINZANI wa African huwa wanafanya vitu kwa maslahi ya wazungu

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM imeongoza hii nchi miaka 60 na hakuna maendeleo na karibu miaka 45 haikua na upinzani na miaka 15 ina upinzani dhaifu sana lakini mbona hakuna maendeleo. Umasikini, ujinga na maradhi ndio yamezidi kuongezeka.

Kwa miaka yote hiyo wao walikua wanafanya kazi kwa maslahi ya nani? Nchi ni bado ni masikini Duniani.
 
Ccm imeongoza hii nchi miaka 60 na hakuna maendeleo na karibu miaka 45 haikua na upinzani na miaka 15 ina upinzani dhaifu sana lakini mbona hakuna maendeleo. Umasikini, ujinga na maradhi ndio yamezidi kuongezeka.

Kwa miaka yote hiyo wao walikua wanafanya kazi kwa maslahi ya nani? Nchi ni bado ni masikini Duniani.
Si kweli
 
Tungekuwa na wapinzani wenye maono kama yako,hakika tungekuwa tunakimbizana na South Africa sahivi na #covid19 tungeshaishinda zamani.
High five mkuu.
Hii nchi haikuwahi kua na upinzani kwa miaka zaidi ya 40, mbona hatukuifikia hata Kenya? Kwa miaka 60 karibu hakukua na upinzani kabisa na miaka 20 kumekua na upinzani dhaifu. Mbona hayo maendeleo hayakuja?

Iwapo watu wenye mawazo kama ninyi ndio watu wengi tulionao nchi hii basi hata maendeleo tutayasikia redioni.

Yaani mnahamisha sababu za underdevelopment kwa wapinzani? Wapinzani ambao hawajawahi hata kua 30% ya wabunge, wapinzani ambao wamekua dhaifu kwa miaka yote ndio walaumiwe kwa umasikini, ujinga na maradhi yanayotamalaki kwa kasi nchi hii kwa miaka 60? Aisee.

Basi sawa.
 
Ukweli unaoujua ni upi? Maana inaonekana una version yako ya ukweli.

Sio kweli kwamba ccm haijaongoza hii nchi miaka 60?

Sio kweli kwamba karibu miaka 40 hatukua na upinzani kabisa?

Sio kweli kwamba ujinga, maradhi na umasikini vimezidi kuongezeka kwa kasi kila siku?

Sio kweli kwamba kwa miaka 20 hatunawahi kua na upinzani wa maana wa kutela pingamizi zozote? Hawajahi hata kufika 30% ya wabunge.

Sio kweli kua kwa miaka 60 bado tumeendelea kushika usukani aa nchi masikini zaidi Duniani sawa na Sudani kusini.

Miaka yote hiyo mtawala nadhani ni wapinzani na sio ccm.
 
Paza sauti wewe unayeipenda Tanzania
IMG-20200515-WA0000.jpg

Huo umasikini wa Tz na South Sudan unalingana vipi? Huo usukani wa umasikini Tz imeushikaje? In terms of what? Is it GDP? Or Per Capita? Au kwa lipi?
 
Back
Top Bottom