Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wapinzani wa Simba SC, Al-Ahli Tripoli kutoka Lybia, wamewasili nchini na tayari wameshuka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakiwa na Bordguards kibao. Timu hiyo inajiandaa kukabiliana na Simba SC katika mechi ya marudio itakayochezwa Jumapili, Septemba 22, katika Dimba la Benjamin Mkapa saa 10:00 jioni.
Al Ahli Tripoli wamejipanga vyema na kuajiri timu ya usalama ya Watanzania itakayowalinda kuanzia uwanja wa ndege hadi siku ya mechi. Wamefanya makubaliano ya kuwajibika kwa usalama wao, na pia wameahidi kuwazawadia timu hiyo ya usalama ikiwa watatekeleza kazi yao kwa ufanisi.
Video: Mwanaspoti