Wapinzani wa Simba Washtuka, Washuka na Bordguards Kibao Airport

Wapinzani wa Simba Washtuka, Washuka na Bordguards Kibao Airport

Ila caf lazima iangalie jinsi ya kutunga sheria ili kudhibiti vitendo vya kishenzi kwenye michezo ,mbona ujinga kama huu atuusikii huko uefa, caf imelala sana hawapo inovative
Caf ni toothless entity linapokuja kuwaadhibu warabu, yaani ni kama brush la chooni ambalo warabu wanalitumia kukata ticket ya kwenda kishiriki michuano mikubwa ya kidunia kwa kuzikandamiza timu za waafrika weusi.
 
Wapinzani wa Simba SC, Al-Ahli Tripoli kutoka Lybia, wamewasili nchini na tayari wameshuka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakiwa na Bordguards kibao. Timu hiyo inajiandaa kukabiliana na Simba SC katika mechi ya marudio itakayochezwa Jumapili, Septemba 22, katika Dimba la Benjamin Mkapa saa 10:00 jioni.
Al Ahli Tripoli wamejipanga vyema na kuajiri timu ya usalama ya Watanzania itakayowalinda kuanzia uwanja wa ndege hadi siku ya mechi. Wamefanya makubaliano ya kuwajibika kwa usalama wao, na pia wameahidi kuwazawadia timu hiyo ya usalama ikiwa watatekeleza kazi yao kwa ufanisi.
Video: Mwanaspoti
Tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom