BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
....badala ya kujifanya ni Wapinzani kumbe ni Mamluki!? Cheyo na Mrema wakati umefika sasa wa kurudi CCM na kuacha usanii wenu wa kujifanya nanyi pia ni Wapinzani.
~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
MATOKEO ya ripoti ya Shirika la Utafiti la Synovate yaliyotolewa juzi yamewagusa watu wa kada mbalimbali wakiwamo wa vyama vya upinzani,baadhi wamekiri kumkubali Rais Jakaya Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wengine wanadai ni uongo.
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo amekiri kwamba, CCM na viongozi wake wanakubalika kwa kuwa wameota mizizi kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameponda matokeo hayo akisema ni uongo na ufisadi mtupu.
Lipumba amelinganisha utafiti huo na utabiri wa Mnajimu maarufu, Shehe Yahya Hussein wa Dar es Salaam.
Amesema, matokeo ni ya kupanga na mtu anayefahamu masuala ya takwimu, atabaini kwamba ni uongo uliotungwa kwa ajili ya kumfagilia Rais Kikwete.
Ametoa mfano kwamba,katika uchaguzi mdogo uliopita, waliopiga kura walikuwa si zaidi ya asilimia 30 kwa maana kwamba ni vigumu utafiti huo wa Synovate kuonesha kuwa asilimia 94 ya wananchi walisema wako tayari kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Cheyo amesema,matokeo hayo yaliyoifanya CCM kupewa asilimia nyingi yanaifanya ijiimarishe zaidi kwa ajili ya uchaguzi ujao.
Sipendi kusema moja kwa moja kuwa matokeo yaliyotolewa juu ya Rais Kikwete hayaendani na hali halisi iliyopo, wala sipendi kumzungumzia Kikwete kutokana na matokeo hayo, kwa kuwa nitakuwa nampigia kampeni, ila ukweli ni kuwa Kikwete anakubalika na wanachi wake na hata chama hicho, amesema.
Pamoja na kwamba hakutaka kueleza kwamba hakuna anayeweza kufua dafu kwa Rais Kikwete kwenye uchaguzi wa mwaka huu, Cheyo alisema, mimi kwenye urais wala hata sitarajii kugombea, nitaendelea kugombea nafasi yangu hii niliyonayo ya ubunge, kwanza kuna mipango mizuri kwa wananchi wangu inayonipasa kuitekeleza, amesema Cheyo.
Mwanachama wa CHADEMA na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Profesa Mwesiga Baregu, alisema kukubalika kwa CCM na Rais Kikwete kunategemeana na utafiti wenyewe kuwa umefanywa katika maeneo yapi.
Alisema unaweza kwa upande wa maeneo ya vijijini CCM au Rais Kikwete wakakubalika sana tofauti na ilivyo mijini.
Hata leo hii ukiuliza jambo lolote kuhusu utendaji wa Rais Kikwete, yapo baadhi ya mambo utakayoambiwa kuwa ameshindwa kutekeleza ipasavyo, alisema.
Akizungumzia demokrasia nchini, Profesa Baregu alisema chama tawala kimeshindwa kutoa nafasi kwa vyama vya upinzani kutawala.
Kuhusu kukubalika kwa Zitto Kabwe, viongozi hao walisema hali hiyo imetokana na namna Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema) alivyopambana kutetea mambo mbalimbali kwa maslahi ya Taifa hili huku upande mwingine akithubutu hata kutofautiana na wanachama na viongozi wenzake wa Chadema.
Mwanaharakati wa masuala ya amani na Katibu Mkuu wa Amani Forum, Risasi Mwaulanga alisema CCM chini ya Mwenyekiti wake Kikwete, bado ina nafasi kubwa ya kutawala hasa kutokana na jinsi ilivyo karibu na wananchi ikilinganishwa na vyama vingine.
Alisema pia Chadema imejizolea umaarufu zaidi kwa kuwa baadhi ya viongozi wanakubalika wanapokuwa majukwaani .
Leo nitakwambia kuwa CCM inakubalika zaidi majukwaani kutokana na mgongo wa Rais Kikwete na uzoefu wa ujumla wa chama hicho, Chadema wao inatokana na viongozi wake kama Wilbrod Slaa, Zitto na Freeman Mbowe, lakini si kwa chama chenyewe, alisema Mwaulanga.
Synovate,iliyokuwa Steadman Group zamani,juzi ilitoa matokeo ya kura zilizopigwa na wananchi huku zikionesha kuwa Rais Kikwete anawaacha mbali wapinzani wake katika uchaguzi wa mwaka huu.
Viongozi waliopitwa na Kikwete ni pamoja na Mbowe na Profesa Lipumba huku Zitto akingara katika ubunge.