Wapinzani wanapinga miradi ya Awamu ya Tano na kuwalisha sumu watu kwamba haina maana

Wapinzani wanapinga miradi ya Awamu ya Tano na kuwalisha sumu watu kwamba haina maana

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Kwanza: Wao sera yao ni ya majimbo .hivyo miradi mikubwa ya kitaifa kwao haina maana maana miradi mikubwa ya kitaifa ni kwa ajiri ya taifa na siyo jimbo.Hivyo mtu kutoka majimbo ya sera ya chadema anaona wivu mkubwa kwa sababu anahisi kodi yake ingebaki jimboni Kwake ili inufaishe watu wake na siyo wengine .kwa maana hiyo miradi kama hiyo siyo keki ya taifa Bali keki ya jimbo.

Sera hii ya majimbo inapingana vikali na sera ya ujamaa ambayo inawaleta watu karibu katika umoja kama baba wa taifa Hayati Mwalimu kambarage Nyerere alivyotuacha tukiwa wa moja.wanaoshabikia sera ya majimbo ndani mwao lazima kuna ubinafsi.

Pili:
Mashabiki wa chadema na wanaopinga miradi mikubwa ya taifa ni watu wa elimu ya chini,wasomi wa elimu ya dot com ambao Hawajui history ya Dunia kwa ujumla na historia ya Tanzania,lakini pia ni watu ambao kwa sasa Hawana Ajira, ni wale ambao wanataka upate leo ule leo,ni watu wa hapa hapa yani hata kutoka nje ya mkoa hawajawai kabisa.ukimwambia train ya umeme anajiuliza hivi hicho ni kidudu gani?hata kuona ndege ikitua hajawahi ona.

3. CHADEMA ilishaishiwa sera dhabiti za kuleta maendeleo ya taifa hili ,hivyo kwa sababu siasa Mahala pengine ni mchezo mchafu wakaona wawadanganye watanzania kuwa miradi hiyo haina maana kwa mtanzania wa hali ya chini.Lakini watu wa hali ya juu na wenye kujielewa ambao wao siyo nipate leo Nile leo,wanafurahia miradi mikubwa hii kwa sababu hata usipopata Matunda leo kesho au kesho kutwa watafurahia watoto wetu ana wajukuu wetu na vizazi vijavyo.

Kuwadanganya watanzania kuwa miradi mikubwa iliyojengwa na awamu ya Tano ni kete kubwa sasa kwa wa wapinzani. CCM msibwete maana huu ni uchaguzi mhimu sana kuliko Nyengine zote maana ni uchaguzi wa kuonyesha kati ya mjinga na mwelewa, mzalendo na msaliti,msomi mwelewa na smomi wa kukarili, mshamba na mtoto wa mjini,mkweli na muongo, nipate leo Nile leo na mwekezaje, mmjamaa na mbepari. CCM mkiruhusu kutoka madarakani hamtarudi milele maana historia itakuwa imeandikwa. mtakuwa mmeisaliti kazi nzuri mliyowatendea watanzania hasa kipindi cha awamu ya tano na kukubariana na ujinga kama siyo upumbavu.
 
Sisi Wapinzani sera yetu Tanzania ijengwe na watanzania wenyewe sio wafungwa wa kichina waje wajenge barabara na nyumba za majeshi wakati wenyewe tunaweza.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mkiendelea na hizi fikra, kama alivyosema jamaa mmoja huku kuna siku mtajikuta wananchi wote ni wapinzani wenu. Chukueni changamoto zinazoibuliwa na wananchi na mzifanyie kazi kama kweli mnataka kuendelea kutawala. Vinginevyo kuna siku mtajikuta mikononi mwa wananchi.
 
Mkuu wewe ndio msomi kati ya hao uliosema mnaipenda CCM?
Hamjakatazwa kujenga miradi lakin kwanini msubirishe wafanyakazi kupata increments zao kisa nyie mna ujenzi?
 
..Ndege hazina faida.

..CCM endeleeni kutufokea.
 
Mkiendelea na hizi fikra, kama alivyosema jamaa mmoja huku kuna siku mtajikuta wananchi wote ni wapinzani wenu. Chukueni changamoto zinazoibuliwa na wananchi na mzifanyie kazi kama kweli mnataka kuendelea kutawala. Vinginevyo kuna siku mtajikuta mikononi mwa wananchi.
Umesema ukweli mtupu kabisa.lakini awamu ya tano Ndicho ilichokifanya. Kuna kipindi nilisikia wapinzani wakisema eti nchi gani hata ndege haina.sasa awamu ya tano ikazifanyia kazi ajenda zote za wapinzani.cha ajabu wakanza kuichukia awamu ya tano kisa tu nazi limepata mkunaji
 
Mkuu wewe ndio msomi kati ya hao uliosema mnaipenda CCM?
Hamjakatazwa kujenga miradi lakin kwanini msubirishe wafanyakazi kupata increments zao kisa nyie mna ujenzi?
Kupanga ni kuchagua.increment inaweza kuwa elfu Kumi.lakini nikuulize kitu wewe ni mwajiriwa wa serikali?
 
Sera ya majimbo ni muendelezo wa ubinafsi na uchoyo. Wanajaribu kuipamba kwa nadharia nyingi lakini ujumbe uliojificha ni uchoyo tu.

Kadri watu wanavyozidi kuelimika ndivyo wanapoibuka wabinafsi wenye uwezo wa kujenga hoja. Watu wenye ushawishi.

Umoja aliotufundisha Nyerere bado haujapoteza maana na mantiki.
 
Hata kama CCM wanafanya vizuri kujenga miundombinu wanakosea kwa kuwanyima wananchi haki za msingi. Pia majigambo yanawaangusha sana.
 
Sisi Wapinzani sera yetu Tanzania ijengwe na watanzania wenyewe sio wafungwa wa kichina waje wajenge barabara na nyumba za majeshi wakati wenyewe tunaweza.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Ni sahihi kabisa.lakini shida ya mtanzania ni kupenda rushwa na vya bure.unampa mtanzania ajenge daraja mwishoe linazama na watu Mtoni
 
Kupanga ni kuchagua.increment inaweza kuwa elfu Kumi.lakini nikuulize kitu wewe ni mwajiriwa wa serikali?
Mkuu sio chaguzi ni nzuri wakati mwingine unachagua vibaya. Huwezi nunua ndege kwa cash watu wakitaka increments unawajibu mpaka umalize mipango yako. Sasa sijui atamaliza lini
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hii sera ya majimbo ipo kwa ajili ya watu wa nyanda za juu kaskazini...wanataka maendeleo wapate wao tuu maana wao ndio wanaongoza katika sekta ya utalii.....halafu huyo anayesema hataki maendeleo ya vitu yeye huko ulaya alipokuwa anaishi alikuwa anaishi kwenye nyumba ya udongo? au alikuwa anapita kwenye barabara za vumbi? na je mbona alikimbia kutibiwa tanzania huko alipoenda kulikuwa hakuna maendeleo kwenye secta ya afya au ndio hizo hoja za kutaka kuuza nchi na vipi aliporudi alipanda ungo au alipata ndege.....hiko chama hakiitakii mema nchi yetu.
 
Ni sahihi kabisa.lakini shida ya mtanzania ni kupenda rushwa na vya bure.unampa mtanzania ajenge daraja mwishoe linazama na watu Mtoni
Mambo ya rushwa hata huko China na ulaya yapo ila kisiri sana. Lakini Tanzania ikijengwa na wenyewe italeta umoja na upendo wa nchi yetu sio hawa wachina.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Tangu upepo umebadilika naona malalamiko kila muda kutoka ccm.

Safari ccm inang'oka
 
Mkiendelea na hizi fikra, kama alivyosema jamaa mmoja huku kuna siku mtajikuta wananchi wote ni wapinzani wenu. Chukueni changamoto zinazoibuliwa na wananchi na mzifanyie kazi kama kweli mnataka kuendelea kutawala. Vinginevyo kuna siku mtajikuta mikononi mwa wananchi.
Hao ndio wale wanaomshauri vibaya m.kiti.
 
Mkuu sio chaguzi ni nzuri wakati mwingine unachagua vibaya. Huwezi nunua ndege kwa cash watu wakitaka increments unawajibu mpaka umalize mipango yako. Sasa sijui atamaliza lini
Kwani ukinunua kwa mkopo hutalipa?unajua mtu akikuuzia kwa deni humo kwanye bei anakuwa ameweka na riba humo?
 
Wananchi vijijini hujawapeleka maji ,wanakunywa maji machafu ,unakula hela za rambirambi ,hizo ndo inamsaidiaje mwananchi asiye na maji kijijini, unanunua ndege haileti faida bado unachukua kodi ununue zingine wakati hata 5% ya watanzania haipandi ndege
 
Kwani ukinunua kwa mkopo hutalipa?unajua mtu akikuuzia kwa deni humo kwanye bei anakuwa ameweka na riba humo?
Hapa tunaongelea chombo kinachogenerate cashflow na faida wakati mwingine na sio kwa matumizi binafsi useme kitakuumiza kwenye kurudisha.

Ndiomana unaona matajiri wengi mabasi au malory wananunua kwa mkopo sio wajinga wanapofanya hivo.
 
Back
Top Bottom