WAPO Radio msijilazimishe kutangaza habari zinazohusu Upinzani kama Mungu wenu hataki

WAPO Radio msijilazimishe kutangaza habari zinazohusu Upinzani kama Mungu wenu hataki

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Ni nadra sana kusikia WAPO RADIO ikitangaza jambo linalohusu upinzani, labda jambo hilo liwe linaifurahisha CCM.

WAPO RADIO mnacho kipindi cha asubuhi kinachohusu matukio, ambacho wasikilizaji hushauriwa kuwatumia ujumbe kuhusu matukio mliyoyatangaza. Cha ajabu, mara nyingi mnakuwa na vigugumizi (eeeeem) kusoma ujumbe mnaouona hautaifurahisha CCM. Ushauri wangu ni kwamba ujumbe huo msiuruhusu kuingia kwenye meza ya mtangazaji ili kigugumizi kisiwepo.

Leo asubuhi, kwenye kipindi hicho kinachohusu matukio, milijitahidi kuweka hotuba ya Mwenyekiti wa Chadema, jambo ambalo si la kawaida kufanywa na kituo chenu. Katika hali ambayo haikutegemewa, ni kuona ile hotuba mmeihariri kwa kukata kipande cha maneno, hivyo kupoteza maana ya alichokizungumza.

WAPO RADIO, matangazo mnayoyafanya hamlazimishwi na wasikilizaji. Hivyo, mkiona jambo ambalo halitaifurahisha CCM, liacheni. Mkumbuke, uchaguzi uliopita mlitangaza waziwazi mlipoingia makubaliano na Polepole kuifanyia kampeni CCM, hakuna aliyewahoji kwa kulifanya hilo kwani ilikuwa ni haki yenu.
 
Hizi si chombo cha dini?wapi wapi na siasa?
Kilijiingiza kwenye siasa kikiwa ni tawi la CCM na kilifanya makubaliano na Polepole, WAPO RADIO hii siyo ile ya mwanzo iliyowahudumia watu wote kwa kuwa na mijadala huru kitu kilichowavutia wasikilizaji wengi, kutokana na makubaliano hayo kile kipindi kilifanyiwa ukarabati na kuzungurushiwa uzio wa nondo na zege.
 
Kilijiingiza kwenye siasa kikiwa ni tawi la CCM na kilifsnya makubaliano na Polepole, WAPO RADIO hii siyo ile ya mwanzo iliyowahudumia watu wote kwa kuwa na mijadala huru kitu kilichowavutia wasikilizaji wengi, kutokana na makubaliano hayo kile kipindi kilifanyiwa ukarabati na kuzungurushiwa uzio wa nondo na zege.
Sikiliza Redio Imani, utapata Dawwa na jinsi ya kuendesha maisha yako
 
Kama ni chombo cha kidini na kilichangiwa na waumini wenye vyama na wasio na vyama,walikosea sana kufanya kampeni kwa ajili ya chama kimoja.
Ni vema sasa waachana na siasa au kama wanataka kufanya siasa wasiegemee upande mmoja
 
Ni nadra sana kusikia WAPO RADIO ikitangaza jambo linalohusu upinzani, labda jambo hilo liwe linaifurahisha CCM.

WAPO RADIO mnacho kipindi cha asubuhi kinachohusu matukio, ambacho wasikilizaji hushauriwa kuwatumia ujumbe kuhusu matukio mliyoyatangaza. Cha ajabu, mara nyingi mnakuwa na vigugumizi (eeeeem) kusoma ujumbe mnaouona hautaifurahisha CCM. Ushauri wangu ni kwamba ujumbe huo msiuruhusu kuingia kwenye meza ya mtangazaji ili kigugumizi kisiwepo.

Leo asubuhi, kwenye kipindi hicho kinachohusu matukio, milijitahidi kuweka hotuba ya Mwenyekiti wa Chadema, jambo ambalo si la kawaida kufanywa na kituo chenu. Katika hali ambayo haikutegemewa, ni kuona ile hotuba mmeihariri kwa kukata kipande cha maneno, hivyo kupoteza maana ya alichokizungumza.

WAPO RADIO, matangazo mnayoyafanya hamlazimishwi na wasikilizaji. Hivyo, mkiona jambo ambalo halitaifurahisha CCM, liacheni. Mkumbuke, uchaguzi uliopita mlitangaza waziwazi mlipoingia makubaliano na Polepole kuifanyia kampeni CCM, hakuna aliyewahoji kwa kulifanya hilo kwani ilikuwa ni haki yenu.
Ahsante sana kwa angalizo zuri. Kama una mawasiliano yao naomba wapelekee dukuduku hilo moja kwa moja ili wapate cha kujifunza na kuboresha upashanaji habari.
 
Kwahiyo wapokea kitu kidogo na kuacha kusimamia misingi ya haki kwa wote. Hivi hii si redio ya kanisa??
 
Ahsante sana kwa angalizo zuri. Kama una mawasiliano yao naomba wapelekee dukuduku hilo moja kwa moja ili wapate cha kujifunza na kuboresha upashanaji habari.
Wanacho kipindi cha DUKUDUKU ninakuhakikishia hawawezi kupokea, hawa waliwahi kuonywa na CCM wakati ule wananchi wengi walipokuwa wakiishambulia CCM kwenye kile kipindi chao maarufu.
 
MOD's JF, nilikwisha waambia sipendi mhariri Post zangu, niliandika "mungu" nikiwa na sababu zangu, inawezekana nyie hamjui kuwa duniani kuna Mungu na mungu, rudisheni neno "mungu" kama nilivyoweka.
 
Ile redio nikiacha kitambo kuisikiliza.

Kwanza imejaa matangazo ya wachungaji plus biashara ya kilimo cha Vanilla ambayo watu wamekuwa wakilalamika kuhusu kutapeliwa.
 
Back
Top Bottom