Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Nadhani ni muhimu zaidi chadema wakafungua kituo cha radio na television japo hakitadumu kwa namna wanavyolumbana..Ni nadra sana kusikia WAPO RADIO ikitangaza jambo linalohusu upinzani, labda jambo hilo liwe linaifurahisha CCM.
WAPO RADIO mnacho kipindi cha asubuhi kinachohusu matukio, ambacho wasikilizaji hushauriwa kuwatumia ujumbe kuhusu matukio mliyoyatangaza. Cha ajabu, mara nyingi mnakuwa na vigugumizi (eeeeem) kusoma ujumbe mnaouona hautaifurahisha CCM. Ushauri wangu ni kwamba ujumbe huo msiuruhusu kuingia kwenye meza ya mtangazaji ili kigugumizi kisiwepo.
Leo asubuhi, kwenye kipindi hicho kinachohusu matukio, milijitahidi kuweka hotuba ya Mwenyekiti wa Chadema, jambo ambalo si la kawaida kufanywa na kituo chenu. Katika hali ambayo haikutegemewa, ni kuona ile hotuba mmeihariri kwa kukata kipande cha maneno, hivyo kupoteza maana ya alichokizungumza.
WAPO RADIO, matangazo mnayoyafanya hamlazimishwi na wasikilizaji. Hivyo, mkiona jambo ambalo halitaifurahisha CCM, liacheni. Mkumbuke, uchaguzi uliopita mlitangaza waziwazi mlipoingia makubaliano na Polepole kuifanyia kampeni CCM, hakuna aliyewahoji kwa kulifanya hilo kwani ilikuwa ni haki yenu.
hii itasaidia sana kuondoa gubu na mihemko kama yako gentleman, dhidi ya matangazo ya radio stations zingine 🐒