Waziri wa madini
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 379
- 466
Ukimya umekuwa mkubwa kwa wanaharakati na wanasiasa ,ukimya ambao unashtusha na kutia hofu kubwa.
Leo hii yupo wapi Zitto Kabwe tuliyemzoea kukosoa serikali kwa hoja zenye mashiko, yupo wapi Freeman mbowe na tindu lissu wasemaji hodari wa kuwasemea wanachi pale Mambo serikalini yanapoenda mrama, wapo wapi wale wakereketwa wa CCM waliokuwa wanamshambulia mwenda zake na serikali yake kipindi Mambo yalipokuwa hayaeleweki wapo wapi wale wakina kigogo 2014 na Mange Kimambi watu waliokuwa wakifichua maovu ya serikali ya awamu ya tano, vipi Tweeter ya kina chaali na wapazaji sauti wengine mbona kimya hapa jamii forum hatuwasikii Tena kina mzee Mwanakijiji na Faizafox.
Je, ukimya huu ni kielelezo kuwa Mambo yapo shwari?
Au ukimya huu ni kwamba watu wamechoka kuongea ukweli na wamesusa Sasa kila mtu apambane na hali yake?
Au ukimya huu ni kwamba wamefungwa midomo kwa kupewa asali warambe?
Kipindi ambacho ufisadi na ubadhilifu upo waziwazi, kipindi ambacho tozo zimepitiliza, kipindi ambacho vitu vimependa bei kupitiliza, kipindi ambacho uchumi wa nchi umeshuka sana, kipindi ambacho miradi mikubwa imesimama, kipindi ambacho umeme wetu sio wa uhakika, kipindi ambacho tunakopa hela kupitiliza, kipindi ambacho matumizi ya serikali ya mekuwa makubwa kuliko makusanyo, kipindi ambacho wenye nacho wanaongezewa na maskini wanapokonywa hadi kidogo walichonacho, kipindi ambacho wamachinga wananyanyaswa.
Je, ni sahihi watu tunaowategemea watusemee kukaa kimya je ukimya huu na kutokupaza sauti ni kwamba hawayaoni yanayoendelea au wameridhika na machozi ya Watanzania kila kukicha. Nani wakutusemea wananchi wanyonge tumebaki kulalamika tu nani wa kukosoa utendaji mbovu wa serikali nani wa kumwajibisha waziri wa nishati na waziri wa fedha kwa utumbo wanaotufanyia Nani wa kukemea ubadhilifu yupo wapi au tukamfufue magu?[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]