Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Sijafanya utafiti wa kutosha kuhusu mikoa mingine, lakini karibu nimetembea mikoa yote ya Tanganyika. Hali zinafanana—utofauti ni mdogo sana.
Turudi mkoani kwangu, Lindi. Kule, ndugu wa damu kabisa ndiye mchawi wako namba moja. Ni kama Yesu alivyosema: "Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake".
Nakumbuka mwaka fulani huko Kilwa Kipatimwa, watoto wengi wa shule ya msingi walifaulu na kwenda sekondari. Miaka hiyo, ukienda sekondari ilikuwa kama umeenda Ulaya. Wanafunzi wa kidato cha nne walifaulu, wa kidato cha sita pia wakafaulu—karibu wote wakaenda UDSM wakitokea shule tofauti.
Miaka hiyo, kazi za kuokota ziliwaleta wote katika ajira nzuri, wakaanza kujenga vijijini kwao. Thubutu! Ndoto zao zilikatishwa ghafla—misiba tu ndiyo iliyotawala. Kwa muda mfupi, wote walifariki kwa hali za kushangaza. Mchezo ukaisha hapo.
Mfano mwingine:
Jamaa mmoja aliyekuwa polisi Dar es Salaam kwa miaka mingi hakuwa anarudi likizo. Mwaka mmoja akakopa pesa na kuamua kujenga nyumbani kwao. Nyumba ilipokamilika, akaja likizo ili afaidi matunda ya kazi yake. Siku ya kwanza tu, asubuhi wakaamka wakimuita—hakuamka. Alikuwa tayari maiti.
Hata ndugu wa damu hawaachi. Brother wangu, ambaye tumezaliwa baba mmoja na mama mmoja, alikuwa na ramani nzuri sana ya maisha. Sasa hivi amechoka kama mzee, ilhali ana miaka 46 tu. Sasa anajichomea mkaa ili apate mkate wa kila siku. Amepigwa na kitu kizito kisichoeleweka, hata akilima hekari tano, mavuno yake hayazidi debe moja au mbili.
Mimi mwenyewe niliwahi kufungua duka la bidhaa mchanganyiko, nikawekeza mamilioni. Lakini cha kushangaza, mauzo kwa siku yalikuwa shilingi elfu 20, elfu 30, mara chache elfu 40. Watanzania wana wivu na uchawi mwingi sana. Kama hujui namna ya kuwakabili, hutafanikiwa hata uwe na juhudi na ubunifu kiasi gani.
Nimeona watu wakiacha kazi nzuri bila sababu za maana baada ya kurogwa.
Watu wana wivu mwingi sana—wanaokuchekea mdomoni, moyoni hawamaanishi hivyo.