Wapo Watanzania wapambanaji lakini hawajafanikiwa kwasababu ya kurogwa na ndugu au majirani zao

Wapo Watanzania wapambanaji lakini hawajafanikiwa kwasababu ya kurogwa na ndugu au majirani zao

Ili kutoboa katika jamii za Watanzania usisahu kuzingatia jadi. Nafikiri imeeleweka. Kuna watu ni komesha, wamefuata jadi wapo maofisi makubwa yenye hela, hata uweke sumu kwenye chakula hali na anashtukia. Hao ndio wanadumu katika ulimwengu huu!

Atakuja kufa Mungu akipenda. Katika Tanzania ye leo watu wanaharibiana sana kupitia jadi.

Nakuhakikishia, katika Tanzania hii, ukiwa na mafanikio na nguvu zako za kiroho ni dhaifu haufiki mbali. Watu wana wivu balaa!
Watu kukutoa roho ni dk sifuri tu
 
Kuna hii kauli umeisema

"Mimi mwenyewe niliwahi kufungua duka la bidhaa mchanganyiko, nikawekeza mamilioni. Lakini cha kushangaza, mauzo kwa siku yalikuwa shilingi elfu 20, elfu 30, mara chache elfu 40. Watanzania wana wivu na uchawi mwingi sana. Kama hujui namna ya kuwakabili, hutafanikiwa hata uwe na juhudi na ubunifu kiasi gani.."

Mkuu,Uliwezaje kujua uchawi ndio sababu pia ulifanyaje ili ku-solve
 
Kuna jamaa bush flan aliuziwa ndinga na mzungu rafiki yake.Ila mzungu alikua jiji flani kaskazini huko,ikabidi jamaa atume dereva wa palepale bush akaifate ndinga.Kuna raia wakampigia dereva simu akiwa njiani anarudi kuwa sijui kama hiyo ndinga itafika salama.Kweli ndinga ikapiga chini ikaja inavutwa hadi gereji.Ikaitengenezwa halafu usiku mmoja kabla jamaa hajaichukua gereji,fundi akaenda kupigia misele viwanja vyake akazinguana na wahuni wakaivunja vioo,akiwa anakimbia msala wa wahuni agonga mtu akafa.Fundi akala kona mkoa mwingine.Ndinga ikaenda polisi
 
Sijafanya utafiti wa kutosha kuhusu mikoa mingine, lakini karibu nimetembea mikoa yote ya Tanganyika. Hali zinafanana—utofauti ni mdogo sana.

Turudi mkoani kwangu, Lindi. Kule, ndugu wa damu kabisa ndiye mchawi wako namba moja. Ni kama Yesu alivyosema: "Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake".

Nakumbuka mwaka fulani huko Kilwa Kipatimwa, watoto wengi wa shule ya msingi walifaulu na kwenda sekondari. Miaka hiyo, ukienda sekondari ilikuwa kama umeenda Ulaya. Wanafunzi wa kidato cha nne walifaulu, wa kidato cha sita pia wakafaulu—karibu wote wakaenda UDSM wakitokea shule tofauti.

Miaka hiyo, kazi za kuokota ziliwaleta wote katika ajira nzuri, wakaanza kujenga vijijini kwao. Thubutu! Ndoto zao zilikatishwa ghafla—misiba tu ndiyo iliyotawala. Kwa muda mfupi, wote walifariki kwa hali za kushangaza. Mchezo ukaisha hapo.

Mfano mwingine:
Jamaa mmoja aliyekuwa polisi Dar es Salaam kwa miaka mingi hakuwa anarudi likizo. Mwaka mmoja akakopa pesa na kuamua kujenga nyumbani kwao. Nyumba ilipokamilika, akaja likizo ili afaidi matunda ya kazi yake. Siku ya kwanza tu, asubuhi wakaamka wakimuita—hakuamka. Alikuwa tayari maiti.

Hata ndugu wa damu hawaachi. Brother wangu, ambaye tumezaliwa baba mmoja na mama mmoja, alikuwa na ramani nzuri sana ya maisha. Sasa hivi amechoka kama mzee, ilhali ana miaka 46 tu. Sasa anajichomea mkaa ili apate mkate wa kila siku. Amepigwa na kitu kizito kisichoeleweka, hata akilima hekari tano, mavuno yake hayazidi debe moja au mbili.

Mimi mwenyewe niliwahi kufungua duka la bidhaa mchanganyiko, nikawekeza mamilioni. Lakini cha kushangaza, mauzo kwa siku yalikuwa shilingi elfu 20, elfu 30, mara chache elfu 40. Watanzania wana wivu na uchawi mwingi sana. Kama hujui namna ya kuwakabili, hutafanikiwa hata uwe na juhudi na ubunifu kiasi gani.

Nimeona watu wakiacha kazi nzuri bila sababu za maana baada ya kurogwa.
Watu wana wivu mwingi sana—wanaokuchekea mdomoni, moyoni hawamaanishi hivyo.

Wachawi ni wale wanaokujua. Mtu baki au mpita njia hawezi kukuloga. Yule unaye msaidia mara kwa mara muangalie sana.
 
Kuna jamaa bush flan aliuziwa ndinga na mzungu rafiki yake.Ila mzungu alikua jiji flani kaskazini huko,ikabidi jamaa atume dereva wa palepale bush akaifate ndinga.Kuna raia wakampigia dereva simu akiwa njiani anarudi kuwa sijui kama hiyo ndinga itafika salama.Kweli ndinga ikapiga chini ikaja inavutwa hadi gereji.Ikaitengenezwa halafu usiku mmoja kabla jamaa hajaichukua gereji,fundi akaenda kupigia misele viwanja vyake akazinguana na wahuni wakaivunja vioo,akiwa anakimbia msala wa wahuni agonga mtu akafa.Fundi akala kona mkoa mwingine.Ndinga ikaenda polisi

Hayo ni mauza uza
 
Kuna kajiukweli fulani ila sidhani kama ni ndugu labda washindani
Mtu wa kwanza kunukuliwa kifo chake, amenukuliwa kwenye Biblia.

Ni Habili mdogo wake na Kaini (yaani toka nitoke)

Chanzo cha kifo, wivu wa baraka.

Yaani Habili alibarikiwa na Mungu, Kaini hakubarikiwa, akaona wivu.

Kama hicho kisa huwa unakipitapita tu ukidhani hakina maana rejea mstari huu

1 Wakorintho 10:11
[11]Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

Niendelee na mifano ya ndugu kuoneana wivu na kuangushana iliyopo ndani ya Biblia?

Nimechoka, kasome mwenyewe kisa cha Yusufu mtoto wa Yakobo kuanzia sura ya 37 ya kitabu cha Mwanzo.
 
Kuna jamaa bush flan aliuziwa ndinga na mzungu rafiki yake.Ila mzungu alikua jiji flani kaskazini huko,ikabidi jamaa atume dereva wa palepale bush akaifate ndinga.Kuna raia wakampigia dereva simu akiwa njiani anarudi kuwa sijui kama hiyo ndinga itafika salama.Kweli ndinga ikapiga chini ikaja inavutwa hadi gereji.Ikaitengenezwa halafu usiku mmoja kabla jamaa hajaichukua gereji,fundi akaenda kupigia misele viwanja vyake akazinguana na wahuni wakaivunja vioo,akiwa anakimbia msala wa wahuni agonga mtu akafa.Fundi akala kona mkoa mwingine.Ndinga ikaenda polisi
Hahaha! Watu wa jadi kutoka vijijini wakienda kununua gari mbali kwanza hawaagi. Pili, wanaenda wakiwa wamejipanga. Wanaifunga tunguri na kurudi nayo vijijini salam salminj
 
Omba haya mambo ya kurogwa uyasikie kama story namna hii yakikukuta ni zaidi ya mateso. Sisi tuliorogwa tunayajua vizuri sana.
Kuna watu wana bahati miili yao haijaguswa ila siku ukinyooshwa wa leo sio wa jana, utasikia alipigwa stroke yule kijana
 
Hiyo ni imani ya hovyo ,hakuna anayeweza kukurudisha nyuma ...Hakuna ndugu Yako anayekuroga ..

Ukishaanza kuamini hayo mambo basi unakuwa kama zombie.
Hakika,
 
Back
Top Bottom