WARAKA WA MOYO KWA MAMA YETU; RAIS DOKTA SAMIA SULUHU HASSAN
(SEHEMU YA KWANZA)
Na: Alex Msama Mwita 🇹🇿
Julai 26, 2025
UTANGULIZI
Mama. Nakuita tena, mama. Leo nikiwa nyumbani kwetu Tarime, mkoani Mara, moyo wangu umenisukuma kuandika waraka huu maalum kwako—waraka wa tafakari, shukrani na matumaini.
Si kwa maneno mengi, bali kwa uzito wa hisia za Mtanzania ninayeshuhudia mabadiliko kupitia uongozi wako.
SALAAMU NA UTAMBULISHO
Mama Mheshimiwa Rais, Amiri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Chama chetu (Cnama Cha Mapinduzi) Taifa, nakutumia salamu za heshima; Kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mimi ni Alex Msama Mwita, Mkristo kwa imani, mcha Mungu, raia mwaminifu niliyezaliwa wilayani Tarime, Mkoa wa Mara. Nakuandikia si kwa tambo za kisiasa, bali kwa sauti ya Mwananchi anayeshuhudia uongozi wa hekima.
TARIME NA MIFUMO YA UCHAGUZI
Wilaya ya Tarime ina majimbo mawili ya uchaguzi: Tarime Mjini na Tarime Vijijini.
Jimbo la Mjini linajumuisha kata zifuatazo:
Bomani, Sabasaba, Turwa, Nyamisangura, Kenyamanyori, Ketare, Nkende na Nyandoto.
Tarime Vijijini ni pana mno. Kata nyingine nitazitaja katika barua inayofuata, ila kwa sasa maeneo kama Nyabilongo na Susuni yapo ndani ya jimbo hilo.
JINSI NILIVYOKUFAHAMU
Awali, sikujua mengi kukuhusu wewe, hadi nilipoanza kukufuatilia ukiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Aidha, nilikushuhudia kwa umakini zaidi katika Bunge Maalum la Katiba, ukiwa Makamu Mwenyekiti chini ya Mwenyekiti Hayati Samuel John Sitta. Hapo ndipo hekima yako ilianza kunishawishi, si kwa kelele, bali kwa mtazamo wa kina na nidhamu ya hoja zako.
SIFA ZA UONGOZI WAKO
Wewe mama ni mtulivu, mstaarabu, mnyenyekevu pia ni imara. Hautangazi kwa maneno bali kwa matendo. Hutumii vitisho au jazba kuthibitisha mamlaka yako. Una tabia ya ushawishi wa kimya. Umetufundisha kuwa uongozi wa kitaifa unaweza kuwa wa heshima, ucha Mungu na busara bila kupoteza nguvu ya uamuzi.
SABABU YA KUANDIKA WARAKA
Waraka huu nimeandika ili kutoa shukrani kwa uongozi wako mama Samia, kushuhudia mabadiliko nchini, kusimulia historia ya kipekee, na kuhimiza mawasiliano ya staha kwa viongozi kupitia mfano wa heshima na busara zako.
MUUNDO WA WARAKA
Waraka huu nimeugawa katika sehemu tatu:-
MAFUNZO KUTOKA KWAKO
Mama huna papara, huna maneno mengi, huna vitisho. Unavumilia matusi, kejeli na dharau. Hasa kutoka kwa wale waliobebwa na fadhila zako. Unajibu kwa kimya chenye majibu. Kazi bora, ushawishi wa kimataifa na sifa kutoka kwa mashirika ya nje. Huo ndiyo ujasiri wa kweli.
HITIMISHO
Sehemu hii ya kwanza ni hatua ya kuanza safari ya waraka huu. Nakuahidi, sehemu ijayo nitafichua mambo ya kihistoria ambayo hayajasimuliwa. Sifa na mafanikio ambayo si wote wameyafahamu, lakini yana nguvu ya kutufundisha kuhusu Tanzania mpya na falsafa yako ya 4R.
Imeandikwa na: Alex Msama Mwita.
Mtanzania Mtiifu wa Dkt Samia Suluhu Hassan.

- Sehemu ya kwanza (huu hapa) ni utangulizi wa heshima na utambulisho.
- Sehemu ya pili na ya tatu nitafafanua historia, sifa zisizojadiliwa sana, na somo la kipekee kutoka kwako ambalo naamini litakuwa rejea ya kizazi.