Huyu ndio waziri wa ardhi alisema nintapeli namba moja la viwanja haijawahi toka kauli tofauti na ile hivyo inaendelea kusimamaImeandikwa na Alex Msama Mwita.
MAMA. nakuita tena, mama. Naandika waraka au ujumbe huu mzito kwako. Leo Julai 26, 2025 nikiwa nyumbani kwetu, Tarime, mkoani Mara.
Mama. Mheshimiwa Rais. Amiri Jeshi Mkuu. Mwenyekiti wa chama chetu, chenye machungu na mahitaji ya Watanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), nakusalimia kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (namini moyoni mwako umeitikia; "Kazi Iendelee")
Mama, naitwa Alex Msama Mwita. Nimezaliwa wilayani Tarime.
Mama, Tarime ni Wilaya yenye majimbo mawili ya uchaguzi. Jimbo la Tarime Mjini na Tarime Vijiini.
Jimbo la Tarime Mjini, lina kata za; Bomani, Sabasaba, Turwa, Nyamisangura, Kenyamanyori, Ketare, Nkende na Nyandoto.
Kata za Tarime Vijiini, nitazitaja katika barua yangu kwako ijayo ( Ni Jimbo kubwa mno), ila maeneo kama Nyabilongo na Susuni ni Tarime Vijiini.
Mama, mimi Alex Msama Mwita, ni Mkristo kwa Imani ya Dini, mwenye hofu ya Mungu ninayeabudu katika Roho na Kweli.
Mama, naomba niseme ukweli. Nilikuwa sikufahamu sana. Nilianza kukufahamu ukiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Nikakufahamu ukiwa Makamu Mwenyekiti, katika Bunge Maalumu la Katiba, chini ya Mwenyekiti, Hayati Samweli John Sitta.
Ukiwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, hapo ndipo nilipoanza kuelewa vyema uwezo wa akili yako!
Mtu mjinga asiyekuwa na uelewa, ni vigumu mno kutambua uwezo wa akili yako mama yangu!
Wewe ni mkimya. Mstaarabu unayefanya mambo kwa weledi na umakini!
Hutumii nguvu kubwa kuwaaminsha watu uwezo wako kiuongozi, unafanya vitendo zaidi!
Huko nyuma, Watanzania tuliaminishwa Rais ni lazima atumie maneno makali na vitisho ndipo aaminike na kuheshimika, lakini ulipoingia wewe madarakani, umetupa somo kubwa kuhusu namna ya kuongoza! Kwa hekima, busara, ustahimilivu na hofu ya Mungu zaidi.
Mhe. Rais, nakuandikia barua hii nikiwa nyumbani Tarime. Mimi ni mwanao, sijawahi kuongea na wewe, kwa namna yoyote, ila leo nimeona ni vyema niwasiliane na wewe, kupitia barua hii maalum!
Mama, Mheshimiwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika maisha yangu, sikuwahi kuwaza, kudhani na wala kufikiria kama kuna siku nitaingia kwenye masuala ya siasa, sikuwahi kuwaza.
Lakini namna unavyoendesha nchi, nimelazimika kuwa sehemu ya viongozi, katika Serikali yako. Nimetia nia ya
Ubunge, katika Jimbo la Ukonga, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Barua hii ni ndefu, nimeigawa katika matoleo matatu! Sehemu ya pili na ya tatu, nitaandika mambo mengi adimu ambayo naona kabisa watu hawajawahi kuyasema kuhusu wewe, ambayo ni ya kihistoria, tangu nchi yetu ipate Uhuru!
Sehemu ya pili na ya tatu ya barua hii, nitaandika mambo ambayo Watanzania wengi watashangaa kuhusu wewe.
Mama huna papara. Mama huna maneno mengi. Mama huna vitisho. Mama huna haraka!
Umatukanwa kwa mengi ya kijinga, lakini mama unastahimili. Huwa najiuliza; mimi Alex Msama Mwita, licha ya kuwa muumini na mcha Mungu, kweli ningevumilia matusi haya!?
Wengine mama umewatoa majalalani na kuwapa nyadhifa na hadhi za kimataifa, ubalozi, leo wameshiba mishahara ya ubalozi, wanaamua kukutukana, kama shukurani yao kwako. Bado mama umekaa kimya!
Najifunza mambo mengi mno kutoka kwako, kuhusu uongozi na maisha. Sehemu ya pili na ya tatu ya barua hii kwako, nitaandika kwa ufafanuzi zaidi.
Kwa leo, huu ni utangulizi tu wa barua yangu kwako mama yangu.
Imeandikwa na Alex Msama Mwita. Mtoto Mtiifu wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
ASANTE MUNGU KWA UHAI NA AFYA NJEMA.View attachment 3419793
Una maanisha jamaa ana majini yake ya kazi?Huyu ndiye alikuwa meneja wa Rose Muhando, walipogombana ndio akampiga majini dada wa watu kidogo achanganyikiwe?
Ukonga pana shida, kule nako kuna tapeli Jerry
Samia Hoyeee
Tapeli wa ViwanjaImeandikwa na Alex Msama Mwita.

Njaaa njaaa eti nimetia nia nani akubali kuongozwa na huyu kenge miaka ya leo hii?Huyu nae na makengeza yake anataka kusema nini mbona haeleweki yuko mama! Mama!
In which sense of fairness🤔Not fair!
Huyu sio yule alilalamikiwa na Rose Muhando kwa kum..."...Mama, Mheshimiwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan,......"
HAya masifu yoteeee inaonyesha ulivyo na njaa Sana, unatafuta nafasi ya kushiba na sio kuwatumikia Watu!
WanaJF huyu ndiye Msama promoter wamziki wa injili na wakala WA ushuru wa maegesho na figisu figisu nyiiingi au ni mingine?
"....Wengine mama umewatoa majalalani na kuwapa nyadhifa na hadhi za kimataifa, ubalozi, leo wameshiba mishahara ya ubalozi, wanaamua kukutukana, kama shukurani yao kwako. Bado mama umekaa kimya!...."
Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
Hakuomba kipochi manyoya cha 🌹 huyu?Huyu ndiye alikuwa meneja wa Rose Muhando, walipogombana ndio akampiga majini dada wa watu kidogo achanganyikiwe?
Ukonga pana shida, kule nako kuna tapeli Jerry
Samia Hoyeee
Kwa WagalatiaMsama bila Ruge wa Clouds ni mweupe kabisa kichwani 😂😂
Hapo kaona Jerry Silaa anafanyiwa Kampeni ya Ubunge na Mchengerwa ndio anajifanya kuandika Waraka kama Paulo Mtume 🐼
Kajifedhehesha mwenyewe, kwani Wakurya au watu wa Mara walimtuma?Amewafedhehesha wakurya na watu wa kanda ya ziwa wote. Kuna watu, njaa huwa inawafanya mpaka kuwa wendawazimu. Amesahau hata wazazi wake, amebakia kujipendekeza kwa Samia kuwa eti yeye ni mwanae!! Ameanzisha mashindano na mwashambwa.