Elections 2010 Waraka wa Lowassa kwa vyombo vya habari

Elections 2010 Waraka wa Lowassa kwa vyombo vya habari

Huyu Lowassa na family yake wanaishi katika borrowed time.
Data watu wanazo,huwezi kuwafool watu milele,anaweza kufanya kwa wachovu Wamasai huko Monduli.
 
sema lowasa wehu wa chadema wanatuzingua tu na maneno ya kuumba, sema maji hayajafika kijijini kwenu diwani akusaidia na wananchi wenzako mlete maendeleo na sio kuzusha na kuongea uongo, kidumu chama tawala
 
Da dr slaa amewatikisa japo wameshinda bado hawajiamini.. Kaz ipo
 
Huyu fisadi wa kunuka anataka kusema nini mbona simwelewi? Lowassa kama wewe mrume kweli kanusha kuwa hukushiriki uchafu wa Richmond. Kanusha kuwa wewe ni fisadi. Kanusha kama huna mimali mingi ya kuiba.
Usikimbilie kumnukuu mwalimu Nyerere aliyekupiga chini ulipoanza harakati za kutaka ukuu. Kanusha kuwa ni mdhamini wa msukule uliotangazwa kushinda uchaguzi baada ya kuchakachua. Kanusha kuwa wewe unanuka kuliko hata huo msukule wenu.
 
Ukiona mwenye njaa katulia usidhani ana amani...ni udhaifu tu wa mwili unamfanya aonekane ana "amani". Hii propaganda ya "amani na utulivu" ni mtaji wa wanasiasa wengi uchwara wa bongo.

Tanzania inaelekea kuwa kama Korea ya kaskazini, Cuba, China na nchi nyingine za kikomunisti ambapo wananchi huonekana kama "wana amani" lakini ni kwa sababu ya mfumo wa ukandamizaji wa nchi hizo unaohakikisha tabaka/kikundi fulani cha jamii ndicho kinaamua mustakabali wa taifa na kinahodhi madaraka huku walio wengi wakitaabika na kuambiwa wana amani na utulivu.

Utakuwaje na amani na utulivu wakati hujui kama utaweza kupata japo mlo mmoja wa siku huku ukisikia wateule wameiba mabilioni na 'mkuu wa kaya' kawasamehe "waliorejesha"? Mheshimiwa Lowassa - usitufanye hamnazo.....tumevumilia saana sasa mnatufanya mabwege!
 
Anatoa taarifa kwa umma kama nani?

Buriani akijifungua atatoa taarifa??

Fisadi ni fisadi tu.

Na hutakuwa Rais wa nchi yetu ng'ooooooooooooooooooooo
 
Amani ya nchi hii itavunjwa na mafisadi kama Lowassa ambao wanaiba kura ili wabaki madarakani kwa kuogopa kufikishwa mbele ya Pilato!!
 

Mwasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alituachia amani na utulivu ambavyo ni tunu ya taifa hili.


Hatujasahau...........................

Ni Lowasa huyu huyu aliyekuwa anatamani kifo cha Kambarage.

Unafiki hatutaki
 
Wito wangu kwa Watanzania, ni kwamba tusiichoke amani. Amani tuliyonayo ndiyo imetutofautisha na mataifa mengi yaliyotuzunguka na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kupigiwa mfano. Tuelekeze nguvu zetu katika shughuli halali za kutuletea kipato zisizoharibu amani yetu.

Tukiiharibu amani tuliyonayo, mwisho wa siku nchi yetu itateketea na sote hatutakuwa salama. Tutakuwa tumekwisha.

Mwisho, namsihi Dk. Slaa ajipe muda wa kuzifahamu vyema siasa za nchi hii. Asidanganywe na mahudhurio ya mikutano ya hadhara akadhani ndizo kura katika masanduku ya kupigia kura. Namsihi ajifunze` zaidi jinsi ya kufanya siasa za kistaarabu bila kueneza uvumi, uongo, chuki na uzushi vyenye kutetelesha amani ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.
Tusiichoke amani!??amani mmeichoka nyie mafisadi kwa kutuibia kupita kiasi na sasa tuko mbioni kuwadhibiti! na usImntaje Nyerere kabisa:nono:, mwache apumzike mzee wa watu, the guy would have chosen Dr Slaa and not you mate! simply because Dr ni mkombozi! uuummm! who are you??? , aaand wht have you done to this Nation?? UFISADI!??
 
Ni bora ukae kimya tumekuchoka umeshaiba vya kutosha,
ndio zenu hata kuhusu Richmond, EPA mlikataa na mkabisha lakini ukweli ukajulikana.
Taarifa kama hizo wape Wamasai wenzako wa uko Monduli ndio wanaweza kukuelewa
 
Watu wanatumia nukuu za baba wa taifa bila kutekeleza alichokiamini.

Suala la amani na utulivu lilikuwepo Tanzania kwa sababu viongozi walikuwa waadilifu na hawakumnyonya mwananchi.Kulikuwa hakuna vikao vya kuchakachua,kulikuwa hakuna majizi kama EL na maskini mwananchi hafaidi lasilimali zilizopo na hata zile huduma za jamii kiduchu anazopewa hazilingani na kodi anayolipia kwenye kila huduma na bidhaa.

Sasa wametokea watu kama kina slaa ambao wanafichua mauchafu yote ya hawa miungu watu na ndo wanakuwa maadui wa watawala. Mngekuwa mna akili mngekuwa mnajiuliza kwanini asilimia za kura za uraisi zimepungua kutoka 82% 2005 mpaka 61% 2010!

Kwa nini idadi ya wabunge wa CCM inapungua huku za CHADEMA(chama cha slaa,anayeitwa mropokaji na mzushi)zinaogezeka kwa kasi(400%). Hata kura za uraisi za chadema zimeongezeka kwa zaidi ya 300% baada ya CHADEMA kumsimamisha huyo mzushi na mropokaji!Kiukweli ni kwamba mtandao wa mkwere na wenzake unakiteteresha chama cha mapinduzi.

Na kwakuwa mtandao una nguvu ya fedha (za kifisadi) unaendelea kuchanua ndani ya CCM lakini umeanza kuangushwa na nguvu ya uma.

Ushauri wangu kwenu mrudieni mungu mtubu na kisha muwaombe radhi watanzania kwa kuwaibia na kuwarudishia kilicho chao na sio kutoa matamko kama haya ya kutetea udhalimu.
 
Ha haaa, mbona hajasema amani ndiyo inamsaidia katika kufanikisha ufisadi wake? Huyu naye kawa wa kumnukuu Nyerere? Si sawa na shetani kuuwa huku akilitaja jina la Mungu?

Inabidi mkakati wa elimu huko umasaini uboreshwe inawezekana hata ufisadi hawajui ni nini ndio maana utaona wanaendelea kumpa kura kama vile takwimu zinavyooshesha sehemu ambazo mwamko wa kimaendeleo uko chini ndio wachakachuaji wamapata kura (ingawa bado kuna shaka, manake wamechakachua wakapata 61pc sasa haki ingechukua mkondo ingekuwaje?),wanatakiwa kufuata mfano wa Rombo na Nyamagana.
 
PEACE, PEACE kilapahali AMANI kwanini? au ndio janja ya kuendelea kutuongoza?

WE DON'T NEED PEACE, E NEED EQUAL RIGHTS AND JUSTICE
 
dah. mkuu sikuwezi kwa kumbukumbu.
mie nimejiinamia pembeni naangalia mambo yanavyokwenda. wakishamuapisha jeikei tujue kuwa maisha bora ni kwaheri baibai

Maisha bora yatakuwepo kwa wale wenye NACHO ..... yaani matajiri wakubwa wanaokwepa kulipa kodi na wanaifadhili CCM...
Sisi wengine ni maumivu kwenda mbele
 
Back
Top Bottom