Waraka wa Marehemu Chacha Wangwe na Hatma ya Siasa za CHADEMA

Miaka mitano baadae Waraka wa Marehemu Chacha Wangwe UNATIMIA.
Damu ya Chacha Wangwe haitamuacha MBOWE na Genge lake salama. Ni suala la muda tu.
Pumzika kwa Amani Chacha Wangwe....kwa hakika ulipigana vita vyema.
 
Wakati ule sikumuelewa Chacha ila sasa namuelewa! Hata Zitto aliwahi kukiri alikuja kumuelewa Chacha baadae sana ila mwanzo alimuona msaliti.
Wala usijilaumu mkuu...huwa ni suala la muda tu. Muda unapotimia ni lazima maandiko yatimie.
Damu ya Chacha Wangwe haitawaacha hao Wahuni salama. Muda tu ndio hutoa Hukumu sahihi.
Hata suala la Tundu Lissu muda utakapofika kwa hakika Watanzania watabaki vinywa wazi!
 
Nini kilimtoa Chaha uenyikiti makamu?
Nini kilimtoa Zitto?
Nini kilimtoa Walid?
Nini kilimtoa Slaa?
Nini kilimtoa Arfi?
I guess, next time around Lisu would face the music.
Tayari Lissu yameshamtokea.
 
Kila jambo lina wakati wake uliopangwa, wakati utaamua tu.
 
Asante Chacha Wangwe Mungu akupunguzie dhambi huko uliko...uliyoyapigania leo yanaenda kukiua Chadema.

Kweli muda ni mwalimu mzuri sana.!
 
waraka unaishi

ni mwiba kwa cdm maana wanachama hawana namna bali wanakataa ukweli ila umesimama na wanakufa huku wakitukana jirani
 

sema wewe

2018 bado ni mbowe
 
Waraka huu unaishi aisee
 
Kipindi hiki Slaa alikuwa bado ni Katibu mkuu. Ndo mtu pekee anayeweza kutueleza nini kilichotokea kwa Wangwe.
 
Huyu Mb

Ni yale yale! Miaka yote.
 
Kuna waraka ambao ni wa siku nyingi kidogo ambao inaonekana kama uliwekwa humu JF tarehe 28/6/2013. Na member ambaye anajurikana kama Maulid Daniel.

Nimejaribu kuupitia huu waraka na kwa ufupi inaonekana kuwa ni andiko la mwisho mwisho la Marehemu Chacha Wangwe(Rip)
Katika waraka huo inaonekana marehemu analalika juu ya kuvuliwa umakamu mwenyekiti na kamati kuu.

Pia katika waraka huu kuna mambo mengi sana ambayo marehemu ameyalalimikia. Mojawapo ni matumizi mabaya ya ruzuku. Wakati huo yaani baada ya uchaguzi wa 2005 ruzuku ya Chadema ilikuwa kama Mil 66.

Na katika waraka huu marehemu analalamika jinsi alivyoshauri ruzuku itumike vizuri ili kukiboresha chama chao. Lakini Mbowe alipinga na kuamua kufanya matumizi anavyotaka badala ya kupeleka pesa kusaidia chama majimboni na wilayani.

Mbali ya hayo malalamiko pia Mbowe alidai kukipopesha chama mil 218,338,949. Na kwa sababu hiyo ruzuku ya chama ilitumika kumlipa deni hilo. Na hivyo chama kukosa pesa za kujiendesha.

Mbali ya hapo kuna tuhuma pia walichakachua majina ya wabunge wa viti maalumu ili kuwapachika wanaowataka wao kinyume na walioteuliwa na kamati kuu.

Ukioamisha tuhuma alizozitoa Waitara na hizi zilizopo kwenye huu waraka utabaini kuwa huu ni mchezo ambao umekuwa ukifanyika ndani ya Chadema kwa muda mrefu. Yaani Chama kinakopeshwa kwa mdomo alafu ruzuku inatumika kulipa.

Hivyo basi takukuru kwa kuwa wameshaanza kulishugulikia hili suala tunaomba wafanye haraka ili hatua stahiki zichukuliwe. Maana hizi ni pesa za umma.
 


Mbona mahangaika sana / Chadema nimoto juu moto chini.
 
Nafikiri usichokijua ni kuwa vyama vya siasa ni vyama vya hiyari, kama hukubaliani na maamzi yake hulazimishwi kubaki ndani unaondoka kama ulivyoingia.
 
Baba anapoamua kufanya colabo na watoto kumshughulikia mtoto.
Ujue tayari mshua kesha kuwa house boy (kapoteza sifa za kuwa baba)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…