Kuna waraka ambao ni wa siku nyingi kidogo ambao inaonekana kama uliwekwa humu JF tarehe 28/6/2013. Na member ambaye anajurikana kama Maulid Daniel.
Nimejaribu kuupitia huu waraka na kwa ufupi inaonekana kuwa ni andiko la mwisho mwisho la Marehemu Chacha Wangwe(Rip)
Katika waraka huo inaonekana marehemu analalika juu ya kuvuliwa umakamu mwenyekiti na kamati kuu.
Pia katika waraka huu kuna mambo mengi sana ambayo marehemu ameyalalimikia. Mojawapo ni matumizi mabaya ya ruzuku. Wakati huo yaani baada ya uchaguzi wa 2005 ruzuku ya Chadema ilikuwa kama Mil 66. Na katika waraka huu marehemu analalamika jinsi alivyoshauri ruzuku itumike vizuri ili kukiboresha chama chao. Lakini Mbowe alipinga na kuamua kufanya matumizi anavyotaka badala ya kupeleka pesa kusaidia chama majimboni na wilayani.
Mbali ya hayo malalamiko pia Mbowe alidai kukipopesha chama mil 218,338,949. Na kwa sababu hiyo ruzuku ya chama ilitumika kumlipa deni hilo. Na hivyo chama kukosa pesa za kujiendesha.
Mbali ya hapo kuna tuhuma pia walichakachua majina ya wabunge wa viti maalumu ili kuwapachika wanaowataka wao kinyume na walioteuliwa na kamati kuu.
Ukioamisha tuhuma alizozitoa Waitara na hizi zilizopo kwenye huu waraka utabaini kuwa huu ni mchezo ambao umekuwa ukifanyika ndani ya Chadema kwa muda mrefu. Yaani Chama kinakopeshwa kwa mdomo alafu ruzuku inatumika kulipa.
Hivyo basi takukuru kwa kuwa wameshaanza kulishugulikia hili suala tunaomba wafanye haraka ili hatua stahiki zichukuliwe. Maana hizi ni pesa za umma.