BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
WARAKA WA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SONGWE KWA ASKOFU MWAMAKULA!
Bwana Yesu Asifiwe mtumishi wa Mungu. Ninaitwa OBADIAH SIMON MWAIPALU. Ni Mgombea UBUNGE Jimbo la SONGWE Mkoa wa SONGWE kupitia CHADEMA. Nilienguliwa na Msimamizi wa Uchanguzi Jimbo la SONGWE kwa kuchezea fomu yangu na kugushi namba za vitambulisho vya mpiga kura ambao ndio wadhamini kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.
Msimamizi wa Uchanguzi, Bi FAUZI HAMIDU NGATUMBURA kwa makusudi amefanya hujuma hii bila kujali madhara yanayoweza kutokea kutokana na hili. Alichokifanya ni kubadili baadhi ya namba kihuni ili kunipotezea sifa ya kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Songwe. Kanuni zinataka Mgombea UBUNGE awe amedhaminiwa na wapiga kura halali wasiopungua 25 na fomu yangu ilikuwa na wadhamini 30+
Alichofanya yeye na Wasaidizi wake ni kubadili baadhi ya namba yaani 1 kuifanya kuwa 4 na 5 kuwa 8 na 7 kuwa 9 na kupelekea kupunguza idadi ya wadhamini hadi kufikia 23 na kuniengua kihuni. Na mbaya zaidi, Mgombea wa CCM ndugu PHILIPO MULUGO anasema wazi katika vijiwe nongwa kwamba alishamalizana na Msimamizi wa Uchanguzi na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na kwa kuwapa chochote kitu hivyo basi hata ningefanyaje Tume haiwezi rudisha jina langu.
Haya ndio yaliyotokea Jimbo la SONGWE na wananchi wanalia na wanapiga simu kila wakati na hata ninapokutana nao huangua kilio sana wanaongea maneno ya kuralua moyo na kupoteza tumaini na watawala kwa hiki walicho kifanya!
Na pia wameengua madiwani wangu 10 kati ya 18 ambao ndio idadi ya madiwani Jimbo zima kwa Sababu za hovyo kabisa.
Ni hayo baba askofu
Kutoka kwa Obadiah Simon Mwaipalu, tarehe 17 Septemba 2020
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki