Waraka wa Pili wa Pascal Mayalla.Maisha Binafsi.

Waraka wa Pili wa Pascal Mayalla.Maisha Binafsi.

Status
Not open for further replies.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wana jf wenzangu.

Binafsi, sipendi kujizungumzia maisha yangu binafsi, lakini leo, imebidi kwa vile kuna thread ambayo mimi nilihusishwa kwa tuhuma za ushoga.

Nilijipanga kuijibu, nikakuta imefutwa. Namuomba mode, airudishe. Kama humu jf tunayasema yoyote kuhusu yoyote akiwemo mkuu wa nchi, basi ni busara uhuru huo ukaachwa hivyo hivyo ulivyo hata kama ni tuhuma zinazomhusu member wa humu ndani kuepusha jf kuonekana ina play double standards, kutuhumiwa watuhumiwe wengine bila hata ya ushahidi, lakini akituhumiwa jf member, thread inafutwa.

Naomba irudishwe ili nipate fursa ya kuzijibu baadhi ya tuhuma.

kaka Mayalla habari,
, nimeona umeifatilitia hii topic kwa muda mrefu na mwisho umetajwa jina kabisa, nakupongeza kwa kuwa mpore na muelewa (hukurupuki), samahani sana kaka kwa ombi langu hili la wewe kukanusha ama kuikubali hii habari,vinginevyo wengine tutachukulia ni habari ya kweli maana kimya kinamaanisha kukubali
ni ombi tu kaka
Kituko, na wengine,
Mimi ni memba humu JF, na binafsi sipendi kwenda deep kwenye personal issues za watu, lakini kwa vile hii issue ni 'trivial' na iliwahi kuvumishwa huko nyuma, sikuona haja ya kuijibu kwa kuamini, kwenye ukweli, uongo hujitenga, niliamini imekufa kama ilivyoibuliwa, lakini uongo ukisemwa sana, na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwishowe hugeuka ndio ukweli machoni na masikioni mwa watu.

Baada ya issue hii, kuibuka tena kwenye hii, thread, niliamua kuifuatilia na hatimaye ningeijibu, hata kama usingeniomba.

Kwa wakati huu ninapojiandaa kujibu,
Naombeni kwa yoyote mwenye facts zozote kuhusu mimi na mahusiano ya kihivyo aziweke humu, ili wakati wa kujibu nijibu jumla.
1. Kwa kuanzia, naomba niweke CV yangu fupi, ili yoyote mwenye hoja yoyote dhidi yangu, ailete hapa jamvini.
Mimi ni mwandishi wa habari na Mtangazaji,
• Nimesoma primary Oyaterbay -miaka 7
• Tambaza Sekondari- miaka 4
• Ilboru High School-miaka 2
• JKT Makotupora na MMJKT-mwaka 1
• Tanzania School of Journalism- miaka 2
• Chuo Kikuu cha Dar es Salaam -miaka 4 - Nikiwa UDSM, nimeishi Block F, single room no 128. Kama kuna watu waliona any frequecy visitor wa jinsia yangu chumbani kwangu, pia naomba mseme.
Hivyo sehemu hizo zote, nimesoma na watu ambao wanazifahamu tabia na mwenendo wangu tangu utotoni mpaka ukubwani, hivyo namuomba yoyote aliyewahi kuona tabia, mwenendo au viashiria vyovyote vya tabia hizo, naomba aziweke wazi ili kuthibitisha hilo.

2. Nimefanya kazi
• Daily News - miezi 6 (intern)
• Radio Tanzania -miaka 5
• DTV/Channel Ten -miaka 5
• TVT/TBC -miaka 2
• Umoja House -miaka 2
• PPR ambako niko mpaka sasa
Hivyo kote huko nilikofanya kazi, naamini kuna members humu JF ambao wananifahamu, kama kuna mwenendo wowote unaofanana na tuhuma hizo, naomba waeleze kwa ukweli na uwazi.

3. Mimi naishi Mbezi hapa jijini Dar es Salaam, lakini pia kwa vipindi tofauti, nimewahi kuishi katika miji ya London, Washington DC, New York, Stockholm, Rome, Geneve, New Dheli, Nairobi, Kampala, Bujumbura, Kigali, Lilongwe, Pretoria, J'burg etc. Kote huko, nimekuwa nikiishi na jamii za Watanzania huku ni interact kwenye sherehe, mitoko na maisha ya kawaida, hivyo lazima kuna watu wanaijua mienendo yangu, na ukweli huwa sifanyi mambo yoyote kwa kificho, kama nina tabia hizo, nawaomba waseme wazi tuu.

4. Life style yangu mimi ni lifest hivyo mambo yangu mengi ni mambo ya hadharani. Miaka 15 ya maisha yangu, nimekuwa nikiendesha bike's, big na racing bikes, kama kuna mtu ana kumbukumbu ya kuniona nimepakizana na mtu wa jinsia yangu au hata tuu kuandamana naye popote, naomba aseme wazi.

5. Nimeitumia sehemu kubwa ya ujana wangu kuishi maisha ya kawaida, kujirusha kwa kiasi, kunywa na makundi ya watu, na kujichanganya sana tuu, hivyo kwenye michanganyiko yote hiyo, kama ni mtu wa kihivyo, lazima wapo walioshuhudia, please just come forward and say it!.

6. It takes two to tangle!, kwa vile mimi ni mlengwa, basi lazima nitakuwa nimeshawahi kuwa na patner mwingine yoyote zaidi ya huyo anayetajwa, hivyo kama kuna yoyote aliyewahi kusikia mtu mwingine yoyote ana mahusiona ya kihivyo na mimi, naomba aje forward.

Baada ya kuuliza maswali yote hayo, nitakusanya majibu, ndipo nije na jibu, why me, kwanini niuhusishwe na Mataka

7.Mataka namfahamu tangu akiwa PPF, na mimi nikiwa mwanahabari. Mwaka 1999, nilidhaminiwa na PPF, NPF na Masai Studio, kufanya ziara ya kihabari nchini Marekani, hivyo nilikwenda ofisini kwake kwenye masuala ya udhamini, kwa hisia zangu, kwa vile ombi langu lilikuwa la dharura, nilipata udhamini husika na kulipwa in US $, sasa hizo pilika za malipo wakati huo, tena kwa fedha za kigeni, shughuli yake ilikuwa kubwa. Naamini ni kufutia kupatikana kwa udhamini huo, kukapelekea mabingwa wa kudhania, kujiaminisha udhamini ule, kwa uharaka ule, sio bure, lazima kuna kitu, ndipo uvumi huo ukaenezwa.
8. Nilisafiri safari husika, na katika safari hiyo, Mataka hakuwepo, sijawahi kukutana popote na Mataka tangu baada ya kuupata udhamini ule. Sijawahi kukaa nae hoteli moja popote, au kukutana naye privately popote.
9. Niliporejea nchini, mwaka 2000 ndipo Uvumi huo ukaibuka, nikiwa TBC. uliwafikia rafiki zangu wa karibu walifadhaishwa sana, hata mimi pia nilifadhaishwa na uvumi huo. Nilishauriwa ili kuufuta, nionyeshe uanamume wangu kwa kujifanya kijogoo, sikuona sababu nikiamini kwenye ukweli uwongo hijitenga, kwa vile ni uwongo, sikuujali nikiuacha ujitenge.
10. Mimi Pascal Mayalla, nathibisha kwenu, sio shoga, sina vitendo vyovyote vya ushoga. Ni baba wa watoto 6, watutu kati yao wako sekondari na wawili ni member humu JF. Naamini wale watu wangu wa karibu, wananielewa, wale wengine wasio nielewa naombeni mnielewe.

Asanteni.

Pascal.

Pascal pole na hongera kwa kuamua kuweka wazi, haswa kukanusha huu uvumi mbaya. Naelewa namna inavyofadhaisha kupatikana na tuhuma za namna kama hiyo.

Pole sana bwana Pasco. Kwa kweli inatiaga hasira sana pale watu ambao hawakujui kujifanya wanakujua na kuanza kueneza mambo ambayo hawawezi hata kuthubutu kuyathibitisha.

Watu wa hivyo wapo wengi sana humu JF. Amini usiamini hata mimi nimewahi kuzushiwa eti ni shoga. Tena nilizushiwa na watu ambao hawanijui kabisa. Watu ambao hawajawahi kuniona na ambao hata nikikutana nao mtaani hawataweza kunitambua mimi ni nani. Lakini wakazusha hivyo. Inasikitisha kwa kweli.

10. Mimi Pascal Mayalla, nathibisha kwenu, sio shoga, sina vitendo vyovyote vya ushoga. Ni baba wa watoto 6, watutu kati yao wako sekondari na wawili ni member humu JF. Naamini wale watu wangu wa karibu, wananielewa, wale wengine wasio nielewa naombeni mnielewe.

Asanteni.

Pascal.

Dah tangu mwanzo nikiona giza tu, heri hapo kwenye nimejua nnini kinaendelea, so pole kwa kuzushiwa Ushoga

Duh Kaka Pole sana, ni dhahiri umeeleza kila kitu kwa kina, Ingawa najua hunijua by JF ID, personal nakufahamu niliwahi kufika hadi kwako pale mbezi jogoo na hata kabla ya hapo pale Ilala nikiwa na rafiki yangu mmoja ambaye ni mwanahabari akiwa anamsarandia shem wako aliyekuwa akiishi na watoto wako wawili by then. Frankly speaking kuna mambo ya kawaida niliyajua kuhusu wewe lakini kwa kweli sikuwahi kusikia hiyo habari.

My Take:

Kuna namna ya chuki ambayo imejitokeza kwa sababu moja ama nyingine aidha kwa sababu tu za kimaisha, Kazi au shughuli nyingine ambayo binafsi ndo hasa chanzo cha kuchafuana kwa kiasi hiki.

Mayalla, unachotakiwa kwa hivi sasa ni ku-ignore ili isizidi kuumiza Moyo wako maana kwa namna ambavyo umeelza kwa uchungu ni sifa kwa wale waliokusudia kukuchafua!

Maneno sio mwisho wa maisha ingawa kwa kweli yanadescourage kwa namna ya pekee!

Pole sana Brother, Naamini Yataisha Maana yanenwayo na mwanadamu yanakwisha!!!

Yaani mtu akienda nssf kufuatilia malipo basi tabu

tutafika mahali tukimuona huyo mataka yupo sehemu tunakimbia mbio
kabla hujaaanzishiwa habari sizo

Pole sana Paschal! Kuzushiwa habari mbaya kiasi ...pole sana ni kweli kuna habari nyingi sana za ajabu na maisha ya watu zinaletwagwa humu na inahitaji hekima kuu kujitokeza kutoa ukweli husika

Wengine wanaamua kuacha , wengine wanajibu lakini maisha yanasonga mbele nakupongeza kuvunja ukimya!

Pole sana Pascal....binadamu ni furushi la moto......halibebeki

so sad,kwanin mtu anaweza kumbebesha mwenzie kashfa nzito kama hii.....duh,bor uzushiwe mwizi si ushoga......

Pole sana bwana Pasco. Kwa kweli inatiaga hasira sana pale watu ambao hawakujui kujifanya wanakujua na kuanza kueneza mambo ambayo hawawezi hata kuthubutu kuyathibitisha.

Watu wa hivyo wapo wengi sana humu JF. Amini usiamini hata mimi nimewahi kuzushiwa eti ni shoga. Tena nilizushiwa na watu ambao hawanijui kabisa. Watu ambao hawajawahi kuniona na ambao hata nikikutana nao mtaani hawataweza kunitambua mimi ni nani. Lakini wakazusha hivyo. Inasikitisha kwa kweli.

Pole , lakini angalau umezushiwa thru ur Nyani Ngabu alias and not ur true identity....japo pia ni mbaya but heri kuliko kutajwa...

pole paschal....propaganda zingne ata zsambazwe vp WALA HAZIVUMI.....WALA HAZISHK MASIKIO YA WATU....uwongo ujitenga always..

wapotezeee...shoga haji kwa kupakaziwa...ata ukiambiwa john ni shoga lakin ukmchek km hana dalili za ushoga ..basi habar hufa na wala aikai kichwani.....

achana nao..iyo ni vta ..yaweza kuwa ya maslahi...kaza buti....watachonga wataacha wenyewe

Jamani naomba nilete kisa kama hiki kilitokea tanga zamani

kuna jaamaa mmoja tanga anaitwa bwana kaka
huyo jaamaa ni maarufu mno tanga kwa mambo kama yanayosemwa kuhusu mataka
halafu ni mshabiki mkubwa mno wa coastal union

sasa kuna siku kuna mtu aklikwenda kumtembelea nyumbani kwake.
Na huyo bwana kaka nyumba yuko peke yake na alikuwa katoka bafuni kuoga
yupo na taulo,
jamaa hakukaa mda mrefu ,mazungumzo mafupi,sasa
anatoka nje kuondoka na bwana kaka anamsindikiza kumtoa nje huku amevaa taulo.....
Na huku nje kuna watu.....unaweza pata picha ilivyokuwa
uzushi ulisambaa haraka mno....
Imenikumbusha hii story nlisimuliwa zamani kidogo...

Niliifuatilia ile thread kwa umakini pasipo kuamini kilichokuwa kimeandkwa.. MY TAKE: Bro relax and take that challenge as part of life, najua ilikuumza sana na kukuleta mfadhahko.

pole sana bwana pasco. Kwa kweli inatiaga hasira sana pale watu ambao hawakujui kujifanya wanakujua na kuanza kueneza mambo ambayo hawawezi hata kuthubutu kuyathibitisha.

Watu wa hivyo wapo wengi sana humu jf. Amini usiamini hata mimi nimewahi kuzushiwa eti ni shoga. Tena nilizushiwa na watu ambao hawanijui kabisa. Watu ambao hawajawahi kuniona na ambao hata nikikutana nao mtaani hawataweza kunitambua mimi ni nani. Lakini wakazusha hivyo. Inasikitisha kwa kweli.

nn
unaweza sema only famous people ndo wanazushiwa hayo mambo
mfano
obama,jay z,lenox lewis,the list is endless
inawezekana wewe ni famous thats why??

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom