Kaka Pascal Mayalla Heshima mbele Mkuu,
Nakupa tena pole kwa uzushi uliopewa, nahita uzushi kwa sababu kauli yako ndio ya mwisho na ndio inayosimama, anayesema kinyume na wewe ni kutaka kukuchafua ama ni mtu asiye na ustaarabu (NI KITU CHA KAWAIDA KWENYE JAMII)
Mimi binafsi nimejifunza mengi kutoka kwako, kwa kweli ulivyoichukua hii issue kutoka mwanzo mpaka mwisho, busara uliyotumia na ushahidi uliotoa bila kugombana na mtu wala kutukanana na mtu ni funzo kubwa kwangu na kwa wengine wanaoishi kwenye mistari monyoofu na wanaotaka kujifunza na waliotayari kukosolewa
sina cha kukushauri bali ni kukumbushana tu kwamba, kuwa mtu maarufu kunakuwa na mambo mengi yanayoambatana nayo, kitu atakachokifanya mtu wa kawaida ni tofauti na kitu hicho akikifanya mtu maarufu, nadhani watu wengi walishaenda kwa MAtaka lakini ikaonekana nikawaida tu lakini kitendo cha mtu maarufu (Mayalla) kwenda kwa MAtaka basi kimezua uzushi na kuaribiana jina
Pole sana Kaka,nadhani utabaki kuwa yuleyule wa kawaida, MPOLE MSTAARABU NA MWELEWA
"ONGW'ANA O' SHIMBA NANG'WE SHIMBA"