Waraka wa pongezi kwa Miss Judith

Waraka wa pongezi kwa Miss Judith

Ujumbe mzuri nausia uliompatia nadhani utamjenga sana katika ndoa yake.
Kila la kheri😛oa
 
Bila shaka Miss Judith (Keren Happuch) atazingatia sana huu ushauri kwa msaada wa hekima anazozipata kwa Mungu kwani ninavyomfahamu judith ni mcha Mungu sana.

mkuu................ hiyo maneno kwenye bold imekaaje??.............. unataka kusema ni multiple ID syndrome inaendelea hapo??.............

Heee!:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:
Inawezekana hao watu wawili ni mtu mmoja?
Mbona itakuwa maajabu ya aina yake?

mkuu................. hata mimi hapo bado kuniingia kumukichwa kabisa................
 
mwisho wa jambo moja ndoo mwanzo wa jingine. hongera na zingatia ujumbe huu.
 
Bila shaka Miss Judith (Keren Happuch) atazingatia sana huu ushauri kwa msaada wa hekima anazozipata kwa Mungu kwani ninavyomfahamu judith ni mcha Mungu sana.

Mkuu...Miss Judith na Keren_Happuch ni watu wawili tofauti. Ubarikiwe
 
Heee!:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:
Inawezekana hao watu wawili ni mtu mmoja?
Mbona itakuwa maajabu ya aina yake?

mkuu................ hiyo maneno kwenye bold imekaaje??.............. unataka kusema ni multiple ID syndrome inaendelea hapo??.............

mkuu................. hata mimi hapo bado kuniingia kumukichwa kabisa................

Duuu...JF...is never boring..(source: The Boss)
 
Duuu...JF...is never boring..(source: The Boss)

hivi wewe Keren_Hapuch, ........................... unajua kuwa unatuhumiwa kumuibia miss judith biblia??................... (hint: mwendesha mshatka ni AshaDii)..................... haya, hebu tuambie kesi yenu imeishia wapi!!.......................
 
Dear Miss Judith,

Nimesukumwa na upendo mwingi wa dhati uliojaa furaha kukuandikia waraka huu mfupi kukupongeza na kukutakia heri ktk maisha yako mapya ya ndoa unayokaribia kuyaanza hivi karibuni, taarifa niliyoipata kupitia thread yako ya "Mwaka Mpya na Maisha Mapya... Ooh, Glory to God!"

Maamuzi haya si madogo, ni maamuzi ya kuunganisha koo mbili zilizokuwa hazifahamiana na kujikuta zikijenga umoja wa kifamilia na undugu. Hapa ndipo Mawifi, Mashemeji, Wajomba, Mashangazi, Mama Mdogo, Wakwe na ndg wengine wapya huzaliwa.

Ndoa mara nyingi hufurahiwa na wengi, lakini pia wapo wachache ambao kamwe hawafurahii kusikia taarifa hizi. Wapo ambao wangependa kuona hufanikiwi, wanapenda kukuona ukiharibikiwa, mipango yako ikikwama na hufurahia kuona ukikosa furaha na amani ktk maisha yako. Watu hawa huanza kama marafiki na baadaye kukuletea umbea na maneno mabaya. Kataa maneno ya umbea, chuki, majivuno, kiburi, infedility na mengine yafananayo na hayo! Utapoteza ndoa!

Nakushauri, ili ndoa yako idumu, jitahidi sana kutimiza majukumu yako kama mama wa kiafrika. Mpende Mumeo, kumbuka kuwa Kazi ya mama ni kutunza familia, contrary na kazi ya baba ambayo ni kulinda familia! Maandiko yanasema "Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake … na mpumbavu huvunja nyumba yake …", pia baba ni "kichwa cha nyumba …" Ubeijing usikutawale sana, ukizidi ni hatari, nimeshuhudia ukivunja ndoa nyingi. Pika, fua na shiriki kazi za ndani ukisaidiwa na msichana/mvulana wa kazi. Upendo huo, utamvuta baba pia akusaidie ktk majukumu ya ndani. Nakushauri ujifunze kuwa mnyenyekevu kwa mumeo, atakupenda, kukusaidia na kamwe hata kuacha.

Usijisahau ukasema mumeo mtarajiwa kaokoka hivyo hawezi kukamata nyumba ndogo, utakuja kulia! Tumeshuhudia watumishi wa Mungu wakinasa ktk kupata utamu usio halali! Kumbuka kumchunga kwa kumuombea na kumtunza vyema. Mfanye aone nyumbani ni sehemu ya kimbilia au tulizo la moyo wake, atakupenda daima.

Sababu za kuvunjika ndoa, ni nyingi na baadhi yake ni kutokuwa muaminifu ktk ndoa, kutokuwa na upendo wa dhati, tamaa za pesa & mali, kutokujisheshimu, kukosa mapenzi ya dhati, kulipiza kisasi, ndoa kuingiliwa na ndg, majirani & marafiki, kutokuridishana ktk mapenzi, mitazamo tofauti nk. Jiepushe na hayo ili udumu ktk ndoa yako.

Kuna yale mambo mema ambayo mlionyeshana wakati wa uchumba wenu.Yale mema na mazuri yaliyowasukuma mpaka mkaamua kufunga pingu za Maisha, hayo myadumishe, yatawadumisha pia. Usisahau mipango ya maendeleo. Kumbuka kuwapenda ndg wa pande zote, ila usiwape nafasi ya kutawala ndoa, ishi nao kwa hekima hasa mawifi!

Nakutakia mema yote ya ndoa yakukute. Ndoa yako izae matunda ya watoto wa kukutosha, wake kwa waume, na amani na upendo utawala familia yako Mpya.

Mungu awe nawe daima,
Wako,

HorsePower

Mpendwa HP,

asante sana kwa waraka mzuri sana wa pongezi uliojaa hekima tele, sifa na utukufu apewe Bwana!

nimekuwa nikiusoma waraka huu na kuurudiarudia mara nyingi lakini hekima iliyomo ndani yake inanifanya nisichoke kuusoma. sio siri umeongea kila kitu cha kuzingatia kudumisha ndoa yenye upendo wa kweli na ulio endelevu. mwenzenu ndo kwanza nimeingia humu kwenye hii taasisi (kama anavyoiita PJ) msinisahau kwenye maombi yenu ili niwe mke na mama bora kwa utukufu wa Mungu mwenyewe katika kristo Yesu.

amani ya Bwana ipitayo akili zote iendelee kuwahifadhi nyote,
sasa na hata milele na milele.
amina.

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
Mpendwa HP,

asante sana kwa waraka mzuri sana wa pongezi uliojaa hekima tele, sifa na utukufu apewe Bwana!

nimekuwa nikiusoma waraka huu na kuurudiarudia mara nyingi lakini hekima iliyomo ndani yake inanifanya nisichoke kuusoma. sio siri umeongea kila kitu cha kuzingatia kudumisha ndioa yenye upendo wa kweli na ulio endelevu. mwenzenu ndo kwanza nimeingia humu kwenye hii taasisi (kama anavyoiita PJ) msinisahau kwenye maombi yenu ili niwe mke na mama bora kwa utukufu wa Mungu mwenyewe katika kristo Yesu.

amani ya Bwana ipitayo akili zote iendelee kuwahifadhi nyote, sasa na hata milele na milele. amina.

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!

Umesikia?
Mmeo akichelewa kurudi mwekee chakula mezani ale na usimhoji hoji kwa nini kachelewa labda katoka nyumba ndogo na nyumba ndogo inakusaidia sana wewe nyumba kubwa lasivyo utakuwa unachoka sana.
 
alleluhya,desa hilo MissJ

nimeishalikamata Bishanga!

Hongera sana Miss Judith!
Wengine tulisha kucheza siku nyingi sana juu ya maisha ya ndoa na vikwazo vyake, tokea siku zile za mambo ya Loliondo kwa babu, naamini ulisha'save kila ushauri kwenye pc yako!
Cha ziada kwa leo ni kidogo tu, ukumbuke kuwa MFUMO DUME UPO, NA UNAFANYA KAZI 24 HRS!
HONGERa sana.

PJ usichoke kutoa ushauri kaka, kumbuka mambo ya IT haya, unaweza kusave file kisha likawa corupted! ila ule ushauri wako bado uko salam mpendwa na nitaendelea kuutunza kwa ajili ya rejea ya siku zijazo. hapo kwenye mfumo dume panafikirisha na kwa hekima itokayo kwa Mungu naamini tunayaweza yote!

Bila shaka Miss Judith (Keren Happuch) atazingatia sana huu ushauri kwa msaada wa hekima anazozipata kwa Mungu kwani ninavyomfahamu judith ni mcha Mungu sana.

neno la Mungu ni taa ya miguu yangu na mwangaza wa njia zangu. haleluya!!

lakini mpendwa mie siye Keren_Happuch!

Heee!:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:
Inawezekana hao watu wawili ni mtu mmoja?
Mbona itakuwa maajabu ya aina yake?

hapana mpendwa, tu watu wawili tofauti!

Mungu ni mwema........!

........ na uaminifu wake wadumu vizazi hata vizani!! Glory to God!

....wakati wote, na awajaze upendo wake mkuu!!!

amina , amina....... amina tena na amina!!

mkuu................ hiyo maneno kwenye bold imekaaje??.............. unataka kusema ni multiple ID syndrome inaendelea hapo??.............

mkuu................. hata mimi hapo bado kuniingia kumukichwa kabisa................

nimeishafafanua mpendwa, alitufananisha tu. asante sana kwa kunitakia heri!

mwisho wa jambo moja ndoo mwanzo wa jingine. hongera na zingatia ujumbe huu.

ni kweli mpendwa,

ni Mungu mwenyewe atupandishaye kutoka utukufu mmoja hadi utukufu mwingine. heshima na ukuu wote vina yeye hata milele na milele. amina!

Kwa kweli Mungu amtangulie!

amina mpendwa, siku zote tutazitangaza fadhili zake za ajabu kwa nyumba yetu!

hivi wewe Keren_Hapuch, ........................... unajua kuwa unatuhumiwa kumuibia miss judith biblia??................... (hint: mwendesha mshatka ni AshaDii)..................... haya, hebu tuambie kesi yenu imeishia wapi!!.......................

dah! hivi lile gazeti la udaku bado liko mitaani, au lilishafungiwa?

ukimuona AshaDii, msalimie sana!

wapendwa wote katika Bwana, mbarikiwe sana na tuzidi kudumu katika pendo lake!
amani ya Bwana ipitayo akili zote na izidi kutuhifadhi tunapozitafakari njia zake
na ukuu wa jina lake takatifu!

Glory to God!
 
Hongera Mrs Judith .........
Neno langu kwako Efeso 5:22-24 na Mithali 31:10-31
Ubarikiwe mamii
 
Mpendwa HP,

asante sana kwa waraka mzuri sana wa pongezi uliojaa hekima tele, sifa na utukufu apewe Bwana!

nimekuwa nikiusoma waraka huu na kuurudiarudia mara nyingi lakini hekima iliyomo ndani yake inanifanya nisichoke kuusoma. sio siri umeongea kila kitu cha kuzingatia kudumisha ndoa yenye upendo wa kweli na ulio endelevu. mwenzenu ndo kwanza nimeingia humu kwenye hii taasisi (kama anavyoiita PJ) msinisahau kwenye maombi yenu ili niwe mke na mama bora kwa utukufu wa Mungu mwenyewe katika kristo Yesu.

amani ya Bwana ipitayo akili zote iendelee kuwahifadhi nyote,
sasa na hata milele na milele.
amina.

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!

Mpendwa hongera sana na karibu katika taasisi ya ndoa, daima mtangulize Mungu na hakika hatakuangusha.
 
Umesikia?
Mmeo akichelewa kurudi mwekee chakula mezani ale na usimhoji hoji kwa nini kachelewa labda katoka nyumba ndogo na nyumba ndogo inakusaidia sana wewe nyumba kubwa lasivyo utakuwa unachoka sana.

na kwa nini kuhojihoji mpendwa??

kwani mkiwa mwili mmoja, kiungo kimoja cha mwili huo mmoja kinaweza kuhoji juu ya nini kimefanywa na kiungo kingine?? nakupa siri moja ndugu yangu, ukisikia mtu anahoji jua hao si mwili mmoja!kama ni mwili mmoja kweli, kila kitu kifanywacho na mwili huo toka mawio hata machweo ya jua, kinajulikana na mwili mzima kwa ajili ya utukufu wa Mungu! neno hili linathibitishwa na neno la Mungu katika 1 wakorintho 6: 16 kuwa yeye aliyeungwa na kahaba, amekuwa mwili mmoja na kahaba! hivyo mtu mwenye nyumba ndogo amefanywa mwili mmoja na nyumba ndogo hiyo na amelitia unajisi hekalu la Mungu yaani mwili wake.

nakuhakikishia mpendwa wangu kuwa nitayaweza yote kwake yeye anitiaye nguvu!! nitashinda na zaidi ya kushinda. nasi kwa pamoja, tutamshinda ibilisi kwa damu ya Mwana Kondoo na kwa neno la ushuhuda (Ufunuo 12:11)

ubarikiwe sana mpendwa,

Glory to God!

Hongera sana Ms. Judith, Mungu awatangulie katika ndoa yenu.

amina mpendwa, asante sana. amina na tena amina!!

All the best sweetheart.

asante sana mpendwa,

Glory to God!!

Hongera Mrs Judith .........
Neno langu kwako Efeso 5:22-24 na Mithali 31:10-31
Ubarikiwe mamii

asante sana mpendwa.

Efeso 5;23 inasema Kristo ni kichwa cha kanisa naye ni "mwokozi wa mwili". hivyo basi, mume kama kichwa cha mkewe (au kichwa cha nyumba), ni mwokozi wa mkewe (au mwokozi wa nyumba). hakika ni wajibu mkubwa sana huu. nami nitamzingira kikamilifu ili kumwezesha kutimiza majukumu yake haya yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu

ubarikiwe sana mpendwa

glory to God!

Mpendwa hongera sana na karibu katika taasisi ya ndoa, daima mtangulize Mungu na hakika hatakuangusha.

asaante sana mpendwa.

tunayaweza yote kwake yeye atutiaye nguvu

Glory to God!
 
Mpendwa HP,

asante sana kwa waraka mzuri sana wa pongezi uliojaa hekima tele, sifa na utukufu apewe Bwana!

nimekuwa nikiusoma waraka huu na kuurudiarudia mara nyingi lakini hekima iliyomo ndani yake inanifanya nisichoke kuusoma. sio siri umeongea kila kitu cha kuzingatia kudumisha ndoa yenye upendo wa kweli na ulio endelevu. mwenzenu ndo kwanza nimeingia humu kwenye hii taasisi (kama anavyoiita PJ) msinisahau kwenye maombi yenu ili niwe mke na mama bora kwa utukufu wa Mungu mwenyewe katika kristo Yesu.

amani ya Bwana ipitayo akili zote iendelee kuwahifadhi nyote,
sasa na hata milele na milele.
amina.

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
Hongera sana mama NA karibu kwenye club!
 
Back
Top Bottom