Ave Ave Maria
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 10,707
- 5,678
Mungu ni mwema........!
Bila shaka Miss Judith (Keren Happuch) atazingatia sana huu ushauri kwa msaada wa hekima anazozipata kwa Mungu kwani ninavyomfahamu judith ni mcha Mungu sana.
Heee!:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:
Inawezekana hao watu wawili ni mtu mmoja?
Mbona itakuwa maajabu ya aina yake?

mkuu................ hiyo maneno kwenye bold imekaaje??.............. unataka kusema ni multiple ID syndrome inaendelea hapo??.............
mkuu................. hata mimi hapo bado kuniingia kumukichwa kabisa................
Duuu...JF...is never boring..(source: The Boss)
Dear Miss Judith,
Nimesukumwa na upendo mwingi wa dhati uliojaa furaha kukuandikia waraka huu mfupi kukupongeza na kukutakia heri ktk maisha yako mapya ya ndoa unayokaribia kuyaanza hivi karibuni, taarifa niliyoipata kupitia thread yako ya "Mwaka Mpya na Maisha Mapya... Ooh, Glory to God!"
Maamuzi haya si madogo, ni maamuzi ya kuunganisha koo mbili zilizokuwa hazifahamiana na kujikuta zikijenga umoja wa kifamilia na undugu. Hapa ndipo Mawifi, Mashemeji, Wajomba, Mashangazi, Mama Mdogo, Wakwe na ndg wengine wapya huzaliwa.
Ndoa mara nyingi hufurahiwa na wengi, lakini pia wapo wachache ambao kamwe hawafurahii kusikia taarifa hizi. Wapo ambao wangependa kuona hufanikiwi, wanapenda kukuona ukiharibikiwa, mipango yako ikikwama na hufurahia kuona ukikosa furaha na amani ktk maisha yako. Watu hawa huanza kama marafiki na baadaye kukuletea umbea na maneno mabaya. Kataa maneno ya umbea, chuki, majivuno, kiburi, infedility na mengine yafananayo na hayo! Utapoteza ndoa!
Nakushauri, ili ndoa yako idumu, jitahidi sana kutimiza majukumu yako kama mama wa kiafrika. Mpende Mumeo, kumbuka kuwa Kazi ya mama ni kutunza familia, contrary na kazi ya baba ambayo ni kulinda familia! Maandiko yanasema "Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake … na mpumbavu huvunja nyumba yake …", pia baba ni "kichwa cha nyumba …" Ubeijing usikutawale sana, ukizidi ni hatari, nimeshuhudia ukivunja ndoa nyingi. Pika, fua na shiriki kazi za ndani ukisaidiwa na msichana/mvulana wa kazi. Upendo huo, utamvuta baba pia akusaidie ktk majukumu ya ndani. Nakushauri ujifunze kuwa mnyenyekevu kwa mumeo, atakupenda, kukusaidia na kamwe hata kuacha.
Usijisahau ukasema mumeo mtarajiwa kaokoka hivyo hawezi kukamata nyumba ndogo, utakuja kulia! Tumeshuhudia watumishi wa Mungu wakinasa ktk kupata utamu usio halali! Kumbuka kumchunga kwa kumuombea na kumtunza vyema. Mfanye aone nyumbani ni sehemu ya kimbilia au tulizo la moyo wake, atakupenda daima.
Sababu za kuvunjika ndoa, ni nyingi na baadhi yake ni kutokuwa muaminifu ktk ndoa, kutokuwa na upendo wa dhati, tamaa za pesa & mali, kutokujisheshimu, kukosa mapenzi ya dhati, kulipiza kisasi, ndoa kuingiliwa na ndg, majirani & marafiki, kutokuridishana ktk mapenzi, mitazamo tofauti nk. Jiepushe na hayo ili udumu ktk ndoa yako.
Kuna yale mambo mema ambayo mlionyeshana wakati wa uchumba wenu.Yale mema na mazuri yaliyowasukuma mpaka mkaamua kufunga pingu za Maisha, hayo myadumishe, yatawadumisha pia. Usisahau mipango ya maendeleo. Kumbuka kuwapenda ndg wa pande zote, ila usiwape nafasi ya kutawala ndoa, ishi nao kwa hekima hasa mawifi!
Nakutakia mema yote ya ndoa yakukute. Ndoa yako izae matunda ya watoto wa kukutosha, wake kwa waume, na amani na upendo utawala familia yako Mpya.
Mungu awe nawe daima,
Wako,
HorsePower
Mpendwa HP,
asante sana kwa waraka mzuri sana wa pongezi uliojaa hekima tele, sifa na utukufu apewe Bwana!
nimekuwa nikiusoma waraka huu na kuurudiarudia mara nyingi lakini hekima iliyomo ndani yake inanifanya nisichoke kuusoma. sio siri umeongea kila kitu cha kuzingatia kudumisha ndioa yenye upendo wa kweli na ulio endelevu. mwenzenu ndo kwanza nimeingia humu kwenye hii taasisi (kama anavyoiita PJ) msinisahau kwenye maombi yenu ili niwe mke na mama bora kwa utukufu wa Mungu mwenyewe katika kristo Yesu.
amani ya Bwana ipitayo akili zote iendelee kuwahifadhi nyote, sasa na hata milele na milele. amina.
mbarikiwe sana wapendwa
Glory to God!
alleluhya,desa hilo MissJ
Hongera sana Miss Judith!
Wengine tulisha kucheza siku nyingi sana juu ya maisha ya ndoa na vikwazo vyake, tokea siku zile za mambo ya Loliondo kwa babu, naamini ulisha'save kila ushauri kwenye pc yako!
Cha ziada kwa leo ni kidogo tu, ukumbuke kuwa MFUMO DUME UPO, NA UNAFANYA KAZI 24 HRS!
HONGERa sana.
Bila shaka Miss Judith (Keren Happuch) atazingatia sana huu ushauri kwa msaada wa hekima anazozipata kwa Mungu kwani ninavyomfahamu judith ni mcha Mungu sana.
Heee!:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:
Inawezekana hao watu wawili ni mtu mmoja?
Mbona itakuwa maajabu ya aina yake?
Mungu ni mwema........!
....wakati wote, na awajaze upendo wake mkuu!!!
mkuu................ hiyo maneno kwenye bold imekaaje??.............. unataka kusema ni multiple ID syndrome inaendelea hapo??.............
mkuu................. hata mimi hapo bado kuniingia kumukichwa kabisa................
mwisho wa jambo moja ndoo mwanzo wa jingine. hongera na zingatia ujumbe huu.
Kwa kweli Mungu amtangulie!
hivi wewe Keren_Hapuch, ........................... unajua kuwa unatuhumiwa kumuibia miss judith biblia??................... (hint: mwendesha mshatka ni AshaDii)..................... haya, hebu tuambie kesi yenu imeishia wapi!!.......................
Mpendwa HP,
asante sana kwa waraka mzuri sana wa pongezi uliojaa hekima tele, sifa na utukufu apewe Bwana!
nimekuwa nikiusoma waraka huu na kuurudiarudia mara nyingi lakini hekima iliyomo ndani yake inanifanya nisichoke kuusoma. sio siri umeongea kila kitu cha kuzingatia kudumisha ndoa yenye upendo wa kweli na ulio endelevu. mwenzenu ndo kwanza nimeingia humu kwenye hii taasisi (kama anavyoiita PJ) msinisahau kwenye maombi yenu ili niwe mke na mama bora kwa utukufu wa Mungu mwenyewe katika kristo Yesu.
amani ya Bwana ipitayo akili zote iendelee kuwahifadhi nyote,
sasa na hata milele na milele.
amina.
mbarikiwe sana wapendwa
Glory to God!
Umesikia?
Mmeo akichelewa kurudi mwekee chakula mezani ale na usimhoji hoji kwa nini kachelewa labda katoka nyumba ndogo na nyumba ndogo inakusaidia sana wewe nyumba kubwa lasivyo utakuwa unachoka sana.
Hongera sana Ms. Judith, Mungu awatangulie katika ndoa yenu.
All the best sweetheart.
Hongera Mrs Judith .........
Neno langu kwako Efeso 5:22-24 na Mithali 31:10-31
Ubarikiwe mamii
Mpendwa hongera sana na karibu katika taasisi ya ndoa, daima mtangulize Mungu na hakika hatakuangusha.
Hongera sana mama NA karibu kwenye club!Mpendwa HP,