The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Safi sanaaaaaa mchango wenye tija sanaaΓ aaa huu.asante sana1. Nimesoma andiko la Prof. Anna Tibaijuka juu ya hali tete Mkoa wa Kagera tunapojikuta tuko mwisho kwa vigezo vya kiuchumi hususan GDP.
2. Ningeomba atupe namba ya mkoa katika quality of life/happiness index kutokana na household survey. Ni kwa kutazama vyote viwili ndio tunaweza kusema kama tupoteze imani kabisa au tupendekeze mikakati ya kutupandisha chati katika kipindi cha miaka 5 hadi 10.
3. Huko nyuma nimeshandika sababu ambazo zinaelezea kuanguka kwa uchumi wa Mkoa wa West Lake/ Kagera katika miaka 60 kutoka wa 2 hadi wa
Tusidai katiba mpya kwa kutukanana tafadhali Sasa andiko langu na matusi Yako wapi na wapi ebu jitafakari nani mpuuzi kati yangu na wew? Kama mnataka katiba mpya kwa matusi HIV mtaipata kwenye gulio katerero.Upuuzi mtupu, tukiambiwa tuwe na katiba nzuri yenye kupunguza madaraka kwa Rais ili ngazi za chini ziwe na mamlaka ya kuamua maendeleo yao hatutaki. Tutapiga jeramba sana na kulamba viatu vya Rais mpaka kiama
Someni vizur andiko langu sijasema hajasema ukweli, ila kwa nafasi aliyokuwa nayo katika nchi hii alitakiwa kufanya mengi mkoani kwake ila she did nothing leo hii ndo anatoka usingizi wakati kaisha kojoa kitandani.?Jamani tuwe wakweli.Huyu mama ameandika ukweli.Mkoa umetelekezwa.Hakuna shughuri za vijana kujipatia kipato.Maeneo ya ardhi ambayo yalitumika kulima mazao Kama njugu mawe, ulezi,Karanga, mtama, hayapo tena.Yamenunuliwa na watu ambao wanaishi nje ya mkoa na kupanda miti. Kwakweli hili ni janga kubwa. Wahaya wamebakiza kwenda nyumbani wakati wa misiba na Christmas kwa kuwanunulia vijana waliochoka gongo.Nyumba za kifahari zilizojengwa vijijini wanaishi popo.
Umeumbuka na thread zako zamajigambo,Sasa sisi tufanyeje kama mnafunga mipaka yote ya Uganda,Rwanda na Burundi...
Sijui hizi kuuza kahawa yako au vanilaa yako Uganda ni kama umeuza bangi???
Acha tu tukimbie huu mkoa na kubaki kujenga nyumba Kali vijijini za kufikia na kuzikwa
Kwa Nini mnatukana?Umeumbuka na thread zako zamajigambo,
Si huwa unasema kagera imeendelea sana,kuna majumba yakifahari vijijini kabisa!
Mkiwa dar magari yenu mnaoshea maji ya uhai wakati ndugu zenu wanashindia mlo mmoja kijijini,hopeless kabisa!
Hivi utakuwa timamu kuoshea gari maji ya dukani wakati ndugu zako kijijini wanakula mlo mmoja kwa siku?Kwa Nini mnatukana?
Ukiupata utuwekee hapa mkuuNgoja kwanza niutafute waraka
Nawaambia mtoke Dar na Mwanza mkaijenge KagereMmeanza lini kutubagua? Mnatufukuza twende Kwetu wapi? Uganda,Rwanda ,Congo ama Kamerun? Idd Amin alipotuchukua mbona mlimpiga na kumfukuza kama mwizi hadi akafia ukimbizini? Ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu,alisema Nyerere.Mkimaliza kutufukuza sisi atamfuata nani? Otagwisa Mkono 2022.
Wahaya waliipenda Dar ya wazaramo sana kuliko kwao.ππππ.
Mashilingi umemshambulia sana mkuu, eti anachonga ndevu kama kamshungu shungu na kupaka piko.
Wahaya sasa mnawazidi wazaramo kwa michamboπ.
Kumuongelea iddi amini miaka 45 iliyopita kuwa amewarudisha nyuma ni ujinga sana1. Nimesoma andiko la Prof. Anna Tibaijuka juu ya hali tete Mkoa wa Kagera tunapojikuta tuko mwisho kwa vigezo vya kiuchumi hususan GDP.
2. Ningeomba atupe namba ya mkoa katika quality of life/happiness index kutokana na household survey. Ni kwa kutazama vyote viwili ndio tunaweza kusema kama tupoteze imani kabisa au tupendekeze mikakati ya kutupandisha chati katika kipindi cha miaka 5 hadi 10.
3. Huko nyuma nimeshandika sababu ambazo zinaelezea kuanguka kwa uchumi wa Mkoa wa West Lake/ Kagera katika miaka 60 kutoka wa 2 hadi wa 26; kama mtu ambaye ameona haya yote yakitokea.
4. Sababu ya kwanza ni demographic na nategemea Prof. aielezee hii point. Kupiga hatua katika elimu bila kukua kwa viwanda au estate agriculture kuweza kuwaajiri wasomi wake huko kumesabaisha brain drain ya watu wetu walio kwenye productive age kuajiriwa nje ya mkoa wetu na kwa hiyo kuchangia kuendeleza mikoa mingine ya Tanzania.
Tumeacha watoto na wazee ambao mchango wao katika uzalishaji ni haba wakibaki kulima mashamba ya migomba na mibuni iliyopandwa miaka 100 iliyopia. Wachache walio na uwezo wa kuzalisha wamezembea kuhamia mahala ambako wangejiongeza kiuzalishaji na kuendekeza land fragmentation; mojawapo ya sababu ikiwa kuishi kwa invisible earnings kutoka kwenye mishahara ya jamaa zao walioko nje ya mkoa.
5. Sababu nyingine ni historical disruptions za
(a) vita ya Tanzania na Uganda au na Idi Amin. Wengi huiona kama athari katika miaka ya 1978 mpaka 1980;
wanasahau kwamba uhusiano na Uganda ulififia kwa miaka zaidi ya 10 kuanzia 1971. Mathalan uwekezaji wa Serikali/NAFCO katika shamba la Ngano Kibanda,Murongo,lililokuwa mechanised ukiwa na matrekta hadi combine harvestor, ulisitishwa kwa kuhofia Amin asipate target ya kupiga mabomu. Prof. atafiti agundue kwa nini Serikali haikuendelea nao baada ya vita.
(b) Pili,ni Vita ya Kiuchumi ya Sokoine ambapo tofauti na mikoa mingine, wafanyabiashara wote muhimu katika mkoa waliswekwa ndani, na malori zaidi ya 400 yalikamatwa na kuteketea Kaitaba Stadium. Prof. na wasomi wengine watupe kiwango cha economic disruption iliyotokana na vita hiyo na fidia ambayo haikutolewa. Sheria maalumu kutaifisha malori yasiyozidi miaka 5 ambayo ilihusu Kagera tu ilikuwa ya kibaguzi na fidia ilikuwa kiduchu,ambayo kutokana na inflation,hawakuweza kununua lori nyingine. Nilishangaa sifa alizopewa Nsa Kaisi miaka ya karibuni, bila watu kukumbuka ukatili(sadism) alioufanyia mkoa wa Kagera.Serikali na CCM walipaswa kutengeneza Marshall Plan ya kuwekeza katika mkoa kuurudisha kwenye maendeleo iliyokuwa nayo.
(c) Mathalan,mwaka 1967 serikali ilipotaifisha mabenki na Viwanda, kampuni ya West Lake Bus Service iliyokuwa na mabasi ya routes zote mkoani ilifilisiwa na wamiliki wa Kihindi na kukomba hela yote na kumwacha Mzee Daniel K Rwiza, mtu aliyedhamini watu kujenga nyumba za bati Karagwe, kubaki masikini. Shida zote za usafiri mkoani tangu hapo mpaka miaka ya 1990s zinaanzia hapo,na ziliathiri mkoa sana.
Nadhani nimempa Prof. Anna na wapenda maendeleo wa Mkoa wa Kagera nafasi ya kuanzia. Sijataja athari za kuhujumu BCU,kuleta Mamlaka ya Kahawa na kuanzisha BCU(1990) Ltd na KDCU bila mali za Union zote kupatikana nyingine zikichukuliwa na RTC na CCM kuchukua kiwanja cha Union ambako kumejengwa makao makuu ya CCM ambayo ni gofu ambalo halikwisha na halitaisha.
Wakati yote hayo yanatokea viwanda vinajengwa Mbeya,Mwanza, Moshi,Arusha tulikuwa na viongozi wazawa. Nani tumlaumu?
Mbona ujumbe mzuri tu hakuna tatizo.Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wazalendo wote nchini na Duniani kwa Ujumla
Nimeambatanisha Waraka Kutoka kwa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu uduni wa Maendeleo kwa Mkoa wa Kagera
View attachment 2082264
View attachment 2082267
View attachment 2082268
View attachment 2082269
Msomi wa kihaya
Wahaya hawapendani, sehemu yoyote esie karibisha wageni, na imeja wivu na fitina miongoni mwao haiwezi kupata maendeleo, walio endeleza dar sio wenyejiWaraka unaosemekana umeandikwa na Prof Msomi wa kihaya Anna Tibaijuka ukionesha Dunia jinsi mkoa wa kagera unavyorudi nyumba kimaendeleo ni waraka ambao umebeba ujumbe ambao haukustaili kuandikwa na Anna Tibaijuka, au mtu kama wilsoni Masilingi.
Watu hawa wekuwa viongozi wa wakubwa katika serikali za awamu tofauti, mathalani mtu kama Prof amekuwa mbunge wa huko huko mkoani kagera lakini unaambiwa hakuna Alichokifanya zaidi ya kusambaza maji pale muleba.
Ukienda kwa ta mwami wilsoni Masilingi aliishia kuchonga ndevu na kupaka piko bungeni hakuna aliro lifanya ,leo hii wapo nje ya mfumo wanaanza kuropoka ovyo paspo kuja na suluhisho.
Mali alizo Nazo Tibaijuka nusu na robo ya Mali zake ziko mikoa mingine kwa nininl hakuwekeza kwao? Ze same bushit to Masilingi na ndevu zake kama kamshungu shungu leo hii wako nje ya mfumo wanaona mkoa ukidorola wanaanza kelele.
Anna Tibaijuka akiwa mbunge alishindwa hata kuomba barabara ya lami leo hii barabara zinajengwa anaona wivu yeye aliishia kuongea lugha za ajabu ajabu bungeni mfano ile ya KUPANUA na nyingine atulie hata afanyeje Samia hawezi enda na kizee kama yeye apambane na Hali yake.