Waraka wa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu Maendeleo ya Mkoa wa Kagera. "Kagera Twafa"

Wahaya wakubali kuachia ardhi wengine wawekeze.
 
Wahaya wanabadilishana nafasi na wenzao waha mmoja mwaka huu anakua wa kwanza mwingine anakua wa pili kutoka mwisho
Nchi hii sisi waha/Wamanyema tunaongoza kuukimbia mkoa wetu adhimu wa Kigoma.
Waha wamehama maelfu kwa maelfu , kigoma yetu sasa hivi imeshikwa na warundi huwezi amini.
Familia nyingi zimehamia Dar Mwanza, Dodoma Tabora Katavi, Shinyanga,Moro nk.
CCM wanaweza kujikuta wanawaongoza warundi wanaojifanya waha.
Watu wa kigoma walianza kuhama tangu miaka ya 70_80,90,2000 mpaka sasa.
Robo tatu ya ukoo wangu pande zote mbili walihama kitambo huko kigoma.
Watu wa ujiji kwao kumegeuka Dar na mwanza.
Serikali lazima ihakikishe inaiokoa Kigoma ni bora hata watani zetu wahaya wanalima ndizi na maharage wanasafirisha mikoa ya kanda ya ziwa, sisi ukilima ndizi/maharage unauza kigoma tu hakuna usafiri wa uhakika .
Kigoma maharage huwa yanauzwa mpaka 700 kwa kilo huwezi amini. zaidi ni mawese tu nayo ni mashamba ya mababu hakuna mashamba mapya ya vijana.
Kigoma imetelekezwa na kila awamu, tunapambana tunavyojua sisi ila msaada wa serikali haupo au ni slow.
imagine kutoka mwanza mpaka Dar kwa basi sh50000 ila Kigoma to Dar sh70000+ kwa sababu barabara ni mbaya.
Ila tutafika tu kwa kujikongoja.
 
... sana! Ni ajabu kusikia mkoa wa Kagera ni mkoa masikini; ajabu mno! Mkoa ambao ni evergreen throughout the year kwanini uwe masikini? Dah!
Uvivu, Roho mbaya, ubinafsi, nankibaya zaidi sasa hivi wamekuwa washirikina....

Wizi...upo usemi kule eti ukilima vanilla, zao lenye pesa na linalostawi Sana huko wezi wanakupa chaguo AU UWAACHE WAIBE AU UJIFANYE KULINDA WAKUUE!
 
Kwanza aache kumuita “mama“ pili hana nia (kuhusu uwezo wake sijui) ya kufanya chochote kupunguza umaskini Tanzania vinginevyo Bwawa la kuzalisha umeme lingemaliziwa lkn linapotezewa, umeme hakuna umaskini ataushughulikia vipi ?
U profesa wake hauba faida naona
 
Huyu Mama kuitaja Kilimanjaro kuwa Ina maendele kuzidi Kagera atapingwa na wahaya wenzake wa JF
Hahaaaaaaa
Njombe ina maendeleo kuliko huko kwa akina nshomile[emoji2][emoji2][emoji3577]

Wahaya njoeni mbishe hapa
 
Sehemu yoyote ambayo wazawa hawataki kuchangamana na wageni hubaki duni hivyo hivyo

Hata mkoa wa Tanga nao kuna "usisi" hawataki wageni kabisa hasa handeni,kilindi,pangani,muheza,na mkinga na lushoto


Korogwe na tanga mjini at least mchangamano unaridhisha
 
Hao maengineer uchwara wamewasaidia nini? Kama wasomi mnao tokea uhuru lakini bado mnalialia hapa! Stend tu mmeshindwa kujenga!
 
Elimu ndiyo kila kitu, huoni msukuma mwemzenu aliyekuwa anaiponda elimu anavyotambia phd yake feki.
 
Wakati anasema kadiri unavopanua ndo watu wanazid kutaman ulikua wapi

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Jamani tuwe wakweli.Huyu mama ameandika ukweli.Mkoa umetelekezwa.Hakuna shughuri za vijana kujipatia kipato.Maeneo ya ardhi ambayo yalitumika kulima mazao Kama njugu mawe, ulezi,Karanga, mtama, hayapo tena.Yamenunuliwa na watu ambao wanaishi nje ya mkoa na kupanda miti. Kwakweli hili ni janga kubwa. Wahaya wamebakiza kwenda nyumbani wakati wa misiba na Christmas kwa kuwanunulia vijana waliochoka gongo.Nyumba za kifahari zilizojengwa vijijini wanaishi popo.
 
Waraka unaosemekana umeandikwa na Prof Msomi wa kihaya Anna Tibaijuka ukionesha Dunia jinsi mkoa wa Kagera unavyorudi nyumba kimaendeleo ni waraka ambao umebeba ujumbe ambao haukustaili kuandikwa na Anna Tibaijuka, au mtu kama Wilsoni Masilingi.

Watu hawa wekuwa viongozi wa wakubwa katika serikali za awamu tofauti, mathalani mtu kama Prof amekuwa mbunge wa huko huko mkoani kagera lakini unaambiwa hakuna Alichokifanya zaidi ya kusambaza maji pale Muleba.

Ukienda kwa ta Mwami Wilsoni Masilingi aliishia kuchonga ndevu na kupaka piko bungeni hakuna aliro lifanya ,leo hii wapo nje ya mfumo wanaanza kuropoka ovyo pasipo kuja na suluhisho.

Mali alizo Nazo Tibaijuka nusu na robo ya Mali zake ziko mikoa mingine kwa nininl hakuwekeza kwao? Ze same bushit to Masilingi na ndevu zake kama kamshungu shungu leo hii wako nje ya mfumo wanaona mkoa ukidorola wanaanza kelele.

Anna Tibaijuka akiwa mbunge alishindwa hata kuomba barabara ya lami leo hii barabara zinajengwa anaona wivu yeye aliishia kuongea lugha za ajabu ajabu bungeni mfano ile ya KUPANUA na nyingine atulie hata afanyeje Samia hawezi enda na kizee kama yeye apambane na Hali yake.
 
1. Nimesoma andiko la Prof. Anna Tibaijuka juu ya hali tete Mkoa wa Kagera tunapojikuta tuko mwisho kwa vigezo vya kiuchumi hususan GDP.

2. Ningeomba atupe namba ya mkoa katika quality of life/happiness index kutokana na household survey. Ni kwa kutazama vyote viwili ndio tunaweza kusema kama tupoteze imani kabisa au tupendekeze mikakati ya kutupandisha chati katika kipindi cha miaka 5 hadi 10.

3. Huko nyuma nimeshandika sababu ambazo zinaelezea kuanguka kwa uchumi wa Mkoa wa West Lake/ Kagera katika miaka 60 kutoka wa 2 hadi wa 26; kama mtu ambaye ameona haya yote yakitokea.

4. Sababu ya kwanza ni demographic na nategemea Prof. aielezee hii point. Kupiga hatua katika elimu bila kukua kwa viwanda au estate agriculture kuweza kuwaajiri wasomi wake huko kumesabaisha brain drain ya watu wetu walio kwenye productive age kuajiriwa nje ya mkoa wetu na kwa hiyo kuchangia kuendeleza mikoa mingine ya Tanzania.

Tumeacha watoto na wazee ambao mchango wao katika uzalishaji ni haba wakibaki kulima mashamba ya migomba na mibuni iliyopandwa miaka 100 iliyopia. Wachache walio na uwezo wa kuzalisha wamezembea kuhamia mahala ambako wangejiongeza kiuzalishaji na kuendekeza land fragmentation; mojawapo ya sababu ikiwa kuishi kwa invisible earnings kutoka kwenye mishahara ya jamaa zao walioko nje ya mkoa.

5. Sababu nyingine ni historical disruptions za

(a) Vita ya Tanzania na Uganda au na Idi Amin. Wengi huiona kama athari katika miaka ya 1978 mpaka 1980;
wanasahau kwamba uhusiano na Uganda ulififia kwa miaka zaidi ya 10 kuanzia 1971. Mathalan uwekezaji wa Serikali/NAFCO katika shamba la Ngano Kibanda, Murongo, lililokuwa mechanised ukiwa na matrekta hadi combine harvestor, ulisitishwa kwa kuhofia Amin asipate target ya kupiga mabomu. Prof. atafiti agundue kwa nini Serikali haikuendelea nao baada ya vita.

(b) Pili, ni Vita ya Kiuchumi ya Sokoine ambapo tofauti na mikoa mingine, wafanyabiashara wote muhimu katika mkoa waliswekwa ndani, na malori zaidi ya 400 yalikamatwa na kuteketea Kaitaba Stadium. Prof. na wasomi wengine watupe kiwango cha economic disruption iliyotokana na vita hiyo na fidia ambayo haikutolewa. Sheria maalumu kutaifisha malori yasiyozidi miaka 5 ambayo ilihusu Kagera tu ilikuwa ya kibaguzi na fidia ilikuwa kiduchu,ambayo kutokana na inflation,hawakuweza kununua lori nyingine. Nilishangaa sifa alizopewa Nsa Kaisi miaka ya karibuni, bila watu kukumbuka ukatili(sadism) alioufanyia mkoa wa Kagera. Serikali na CCM walipaswa kutengeneza Marshall Plan ya kuwekeza katika mkoa kuurudisha kwenye maendeleo iliyokuwa nayo.

(c) Mathalan,mwaka 1967 serikali ilipotaifisha mabenki na Viwanda, kampuni ya West Lake Bus Service iliyokuwa na mabasi ya routes zote mkoani ilifilisiwa na wamiliki wa Kihindi na kukomba hela yote na kumwacha Mzee Daniel K Rwiza, mtu aliyedhamini watu kujenga nyumba za bati Karagwe, kubaki masikini. Shida zote za usafiri mkoani tangu hapo mpaka miaka ya 1990s zinaanzia hapo,na ziliathiri mkoa sana.

Nadhani nimempa Prof. Anna na wapenda maendeleo wa Mkoa wa Kagera nafasi ya kuanzia. Sijataja athari za kuhujumu BCU,kuleta Mamlaka ya Kahawa na kuanzisha BCU (1990) Ltd na KDCU bila mali za Union zote kupatikana nyingine zikichukuliwa na RTC na CCM kuchukua kiwanja cha Union ambako kumejengwa makao makuu ya CCM ambayo ni gofu ambalo halikwisha na halitaisha.

Wakati yote hayo yanatokea viwanda vinajengwa Mbeya, Mwanza, Moshi, Arusha tulikuwa na viongozi wazawa. Nani tumlaumu?
 
Mali alizo Nazo Tibaijuka nusu na robo ya Mali zake ziko mikoa mingine kwa nininl hakuwekeza kwao? Ze same bushit to Masilingi na ndevu zake kama kamshungu shungu leo hii wako nje ya mfumo wanaona mkoa ukidorola wanaanza kelele.[emoji15][emoji3064]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…