Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba uitoe Simiyu mkuu! Wasukuma wa Ntuzu hawajawahi kuwa wazembe! Msikuruouke kuandika tu vitu humu!
Mamboengine ukisoma unatani kulia. Na mtu akikupa AK 47 hauchelewi kuwa-Hamza wapuuzi fulani huko ccm1. Nimesoma andiko la Prof. Anna Tibaijuka juu ya hali tete Mkoa wa Kagera tunapojikuta tuko mwisho kwa vigezo vya kiuchumi hususan GDP.
2. Ningeomba atupe namba ya mkoa katika quality of life/happiness index kutokana na household survey. Ni kwa kutazama vyote viwili ndio tunaweza kusema kama tupoteze imani kabisa au tupendekeze mikakati ya kutupandisha chati katika kipindi cha miaka 5 hadi 10.
3. Huko nyuma nimeshandika sababu ambazo zinaelezea kuanguka kwa uchumi wa Mkoa wa West Lake/ Kagera katika miaka 60 kutoka wa 2 hadi wa 26; kama mtu ambaye ameona haya yote yakitokea.
4. Sababu ya kwanza ni demographic na nategemea Prof. aielezee hii point. Kupiga hatua katika elimu bila kukua kwa viwanda au estate agriculture kuweza kuwaajiri wasomi wake huko kumesabaisha brain drain ya watu wetu walio kwenye productive age kuajiriwa nje ya mkoa wetu na kwa hiyo kuchangia kuendeleza mikoa mingine ya Tanzania.
Tumeacha watoto na wazee ambao mchango wao katika uzalishaji ni haba wakibaki kulima mashamba ya migomba na mibuni iliyopandwa miaka 100 iliyopia. Wachache walio na uwezo wa kuzalisha wamezembea kuhamia mahala ambako wangejiongeza kiuzalishaji na kuendekeza land fragmentation; mojawapo ya sababu ikiwa kuishi kwa invisible earnings kutoka kwenye mishahara ya jamaa zao walioko nje ya mkoa.
5. Sababu nyingine ni historical disruptions za
(a) Vita ya Tanzania na Uganda au na Idi Amin. Wengi huiona kama athari katika miaka ya 1978 mpaka 1980;
wanasahau kwamba uhusiano na Uganda ulififia kwa miaka zaidi ya 10 kuanzia 1971. Mathalan uwekezaji wa Serikali/NAFCO katika shamba la Ngano Kibanda, Murongo, lililokuwa mechanised ukiwa na matrekta hadi combine harvestor, ulisitishwa kwa kuhofia Amin asipate target ya kupiga mabomu. Prof. atafiti agundue kwa nini Serikali haikuendelea nao baada ya vita.
(b) Pili, ni Vita ya Kiuchumi ya Sokoine ambapo tofauti na mikoa mingine, wafanyabiashara wote muhimu katika mkoa waliswekwa ndani, na malori zaidi ya 400 yalikamatwa na kuteketea Kaitaba Stadium. Prof. na wasomi wengine watupe kiwango cha economic disruption iliyotokana na vita hiyo na fidia ambayo haikutolewa. Sheria maalumu kutaifisha malori yasiyozidi miaka 5 ambayo ilihusu Kagera tu ilikuwa ya kibaguzi na fidia ilikuwa kiduchu,ambayo kutokana na inflation,hawakuweza kununua lori nyingine. Nilishangaa sifa alizopewa Nsa Kaisi miaka ya karibuni, bila watu kukumbuka ukatili(sadism) alioufanyia mkoa wa Kagera. Serikali na CCM walipaswa kutengeneza Marshall Plan ya kuwekeza katika mkoa kuurudisha kwenye maendeleo iliyokuwa nayo.
(c) Mathalan,mwaka 1967 serikali ilipotaifisha mabenki na Viwanda, kampuni ya West Lake Bus Service iliyokuwa na mabasi ya routes zote mkoani ilifilisiwa na wamiliki wa Kihindi na kukomba hela yote na kumwacha Mzee Daniel K Rwiza, mtu aliyedhamini watu kujenga nyumba za bati Karagwe, kubaki masikini. Shida zote za usafiri mkoani tangu hapo mpaka miaka ya 1990s zinaanzia hapo,na ziliathiri mkoa sana.
Nadhani nimempa Prof. Anna na wapenda maendeleo wa Mkoa wa Kagera nafasi ya kuanzia. Sijataja athari za kuhujumu BCU,kuleta Mamlaka ya Kahawa na kuanzisha BCU (1990) Ltd na KDCU bila mali za Union zote kupatikana nyingine zikichukuliwa na RTC na CCM kuchukua kiwanja cha Union ambako kumejengwa makao makuu ya CCM ambayo ni gofu ambalo halikwisha na halitaisha.
Wakati yote hayo yanatokea viwanda vinajengwa Mbeya, Mwanza, Moshi, Arusha tulikuwa na viongozi wazawa. Nani tumlaumu?
Kwa hio mama yako anashindia mlo mmoja kijijini wewe uko dar gari yako unaoshea maji ya uhai.Kila mtu ana maisha yake lakin....
Maisha sio lazima yafanane Kila mtu ana vipaumbele vyake katika maisha ...
Kila mtu atafute maisha yake sio kuwa tegemezi ya watu walio mjini...
Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Jibu hoja. Prof. ama Masilingi hawana hela za kuendeleza maeneo wanakotoka. Kwa mujibu wa katiba yetu budget inapangwa na serikali chini ya uongozi wa rais. Yeye ndiye anaeamua kiasi gani kiende wapi. Ndiyo ya lugha iliyoanza kuzoeleka sasa ya kumpongeza na kumshukuru rais kwa kila jambo la maendeleo linalofanyika nchi nzima. Kwa mantiki hiyo Prof ana haki kabisa ya kuandika aliyoandika. Kama tutakubali kuwaruhusu viongozi wetu waelekeze mipango ya maendeleo sehemu wanazotoka na kusahau sehemu zingine tutafanya sehemu ambazo hazina viongozi wa kitaifa ziachwe nyuma kimaendeleo. Ndiyo maana tunataka katiba mpya itakayogawa keki ya taifa kiusawa.Waraka unaosemekana umeandikwa na Prof Msomi wa kihaya Anna Tibaijuka ukionesha Dunia jinsi mkoa wa Kagera unavyorudi nyumba kimaendeleo ni waraka ambao umebeba ujumbe ambao haukustaili kuandikwa na Anna Tibaijuka, au mtu kama Wilsoni Masilingi.
Watu hawa wekuwa viongozi wa wakubwa katika serikali za awamu tofauti, mathalani mtu kama Prof amekuwa mbunge wa huko huko mkoani kagera lakini unaambiwa hakuna Alichokifanya zaidi ya kusambaza maji pale Muleba.
Ukienda kwa ta Mwami Wilsoni Masilingi aliishia kuchonga ndevu na kupaka piko bungeni hakuna aliro lifanya ,leo hii wapo nje ya mfumo wanaanza kuropoka ovyo pasipo kuja na suluhisho.
Mali alizo Nazo Tibaijuka nusu na robo ya Mali zake ziko mikoa mingine kwa nininl hakuwekeza kwao? Ze same bushit to Masilingi na ndevu zake kama kamshungu shungu leo hii wako nje ya mfumo wanaona mkoa ukidorola wanaanza kelele.
Anna Tibaijuka akiwa mbunge alishindwa hata kuomba barabara ya lami leo hii barabara zinajengwa anaona wivu yeye aliishia kuongea lugha za ajabu ajabu bungeni mfano ile ya KUPANUA na nyingine atulie hata afanyeje Samia hawezi enda na kizee kama yeye apambane na Hali yake.
Nilitegemea kuona andiko/hoja mbadala wa hoja za Prof. Tibaijuka, lakini umeishia kufanya personal attack kwa Tibaijuka na Masilingi.Waraka unaosemekana umeandikwa na Prof Msomi wa kihaya Anna Tibaijuka ukionesha Dunia jinsi mkoa wa Kagera unavyorudi nyumba kimaendeleo ni waraka ambao umebeba ujumbe ambao haukustaili kuandikwa na Anna Tibaijuka, au mtu kama Wilsoni Masilingi.
Watu hawa wekuwa viongozi wa wakubwa katika serikali za awamu tofauti, mathalani mtu kama Prof amekuwa mbunge wa huko huko mkoani kagera lakini unaambiwa hakuna Alichokifanya zaidi ya kusambaza maji pale Muleba.
Ukienda kwa ta Mwami Wilsoni Masilingi aliishia kuchonga ndevu na kupaka piko bungeni hakuna aliro lifanya ,leo hii wapo nje ya mfumo wanaanza kuropoka ovyo pasipo kuja na suluhisho.
Mali alizo Nazo Tibaijuka nusu na robo ya Mali zake ziko mikoa mingine kwa nininl hakuwekeza kwao? Ze same bushit to Masilingi na ndevu zake kama kamshungu shungu leo hii wako nje ya mfumo wanaona mkoa ukidorola wanaanza kelele.
Anna Tibaijuka akiwa mbunge alishindwa hata kuomba barabara ya lami leo hii barabara zinajengwa anaona wivu yeye aliishia kuongea lugha za ajabu ajabu bungeni mfano ile ya KUPANUA na nyingine atulie hata afanyeje Samia hawezi enda na kizee kama yeye apambane na Hali yake.
Ukitoa Dar, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya na Kagera kwingine kote ni aibu tupuMingine niliacha muongezee wadau, ndio maana nikaweka kwenye mabano kwamba hiyo nimetaja ni michache kwa sababu niliona kama nakaribia kutaja mikoa ya Tanzania nzima 😂😂
Ile vita yako na mkoa wa Kilimanjaro naona imeisha rasmi.Sasa sisi tufanyeje kama mnafunga mipaka yote ya Uganda,Rwanda na Burundi...
Sijui hizi kuuza kahawa yako au vanilaa yako Uganda ni kama umeuza bangi???
Acha tu tukimbie huu mkoa na kubaki kujenga nyumba Kali vijijini za kufikia na kuzikwa
Hivi manyara huwa mnaitaja kwa kigezo gani? Wakati hata shinyanga tu haiifikii kwa kila kitu!Ukitoa Dar, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya na Kagera kwingine kote ni aibu tupu
Please mama yangu hausiki kwenye huu Uzi.......Kwa hio mama yako anashindia mlo mmoja kijijini wewe uko dar gari yako unaoshea maji ya uhai.
Huko wanakolewa mpaka wanasahau watoto wao?Ile vita yako na mkoa wa Kilimanjaro naona imeisha rasmi.
Kwanza aache kumuita “mama“ pili hana nia (kuhusu uwezo wake sijui) ya kufanya chochote kupunguza umaskini Tanzania vinginevyo Bwawa la kuzalisha umeme lingemaliziwa lkn linapotezewa, umeme hakuna umaskini ataushughulikia vipi ?
Nani kakwambia mama Samia anashughulika na kuondoa umasikini? pambaneni na hali yenu siku zote mnajisifia eti, Mtanzania wa kwanza kupanda ndege ni Muhaya, Profesa wa kwanza Tanzania ni Muhaya, sasa mnalialia nini, tumieni huo uprofesa wenu kuondoa dhiki Kagera
Kama hulijui hilo kwamba simiyu ni moja ya emerging giants basi huijui tanzania inabidi uongee na mkuu wa mkoa wa Simiyu Kafulila akupe siri. Wasukuma watu wa kazi jomba. Mkoa ule ni mpya ulianza miaka ya 20210 leo hii huwezi kulinganisha na makao makuu ya mkoa wa Kagera au PWANIMkuu, Simiyu unaweza iweka katika list ya mikoa iliyofanikiwa kimaendeleo? 🤔🤔
We mwenyew unajua system ya hii nchi..lkn wao wahaya wanajisibu kuwa mkoa wao wako vzr sasa hata wengine tulikuwa tunawashangaa wako vzr kwa lipi?ati kwamba wana makazi bora na wamesoma sana sasa si wautumie huo usomi kutatua matatizo yanayowakabili?kama mmesoma lkn hiyo elimu mliyoipata imeshindwa kutatua shida zenu basi mjitafakari ni wapi mlipodondokea.Kazi na Iendelee.
Kuna watu wakisikia simiyu au shinyanga anachukulia poa! Nakwambia pale bariadi Simiyu kuna wanaume wanapesa ni shida!Kama hulijui hilo kwamba simiyu ni moja ya emerging giants basi huijui tanzania inabidi uongee na mkuu wa mkoa wa Simiyu Kafulila akupe siri. Wasukuma watu wa kazi jomba. Mkoa ule ni mpya ulianza miaka ya 20210 leo hii huwezi kulinganisha na makao makuu ya mkoa wa Kagera au PWANI
Kama hulijui hilo kwamba simiyu ni moja ya emerging giants basi huijui tanzania inabidi uongee na mkuu wa mkoa wa Simiyu Kafulila akupe siri. Wasukuma watu wa kazi jomba. Mkoa ule ni mpya ulianza miaka ya 20210 leo hii huwezi kulinganisha na makao makuu ya mkoa wa Kagera au PWANI
nukta.co.tz