Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
Ummy Muya
KATIBU wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema waraka maalum utakaowaongoza waumini wa madhehebu hayo katika uchaguzi mkuu wa mwakani, umekamilika.
Sheikh Ponda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam ambapo alisema waraka huo umesheheni ujumbe mzito kwa ajili ya Waislamu.
Alisema waraka huo uko tayari kuanza kusambazwa kwa Waislamu wote nchini na huku ukitangazwa katika vyombo vya habari .
"Waraka huu utakuwa mzito sana ukilinganishwa na ule ambao tuliutoa mwaka jana,"alisema.
Kwa mujibu wa Sheikh Ponda waraka huo umeandaliwa na shura ya maimamu, inayojishughulisha na masuala ya siasa.
Tayari Kanisa Katoliki nchini, limetoa waraka wake unaowataka wananchi kuchagua viongozi, waadilifu na wacha Mungu katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa mwakani.
Hata hivyo, waraka huo umezua malumbano makali kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wakidai kuwa, unaweza kusababisha taifa kusarambaratika.
Akizungumzia maandamano, Sheikh Ponda alisema wanasubiri kumalizika kwa kikao cha Bunge, ili kujiridhisha na hatua zilizofikiwa na chombo hicho katika kushughulikia suala la Mahakama ya Kadhi. "Maandamano ambayo tumepanga yana ujumbe hivyo hatuwezi kuyafanya mpaka kikao cha Bunge kiishe na kufahamu suala hili lipo katika hatua gani,"alisema
SOURCE: MWANANCHI