CCM ina laana za wengi,ina laana za wazalendo walioijenga CCM yenyewe,ina laana za watanzania wanyonge wanaotaabika na maisha ya kila siku licha ya jasho lao halali wanalovuja kutafuta riziki zao za kila siku,ina laana za watanzania wa kila kada,kitendo cha wabunge wa CCm kusadiki na kupitisha kila kitu haijalishi kina madhara kwa watanznia au laa,hiki ni kitendo cha kulaaniwa na kila mzalendo wa nchi hii,hata hawa wanaokuja kulalamika leo wanalalamika kwa kuwa wamehujumiwa wao,ila CCM kuwahujumu watanzania haijaanza leo,haya ni malipo ya dhuluma chama inazozifanya kwa wazalendo wa nchi hii,Ukimuumiza sana mwingine mpaka ukaona kuwa unachokifanya ni halali basi hatua inayofuata ni kujidhulumu Mwenyewe,CCM ni ng'ombe Mweupe aliyeliwa siku alivyoliwa ng'ombe mweusi
KUNA SIKU SIMBA ALIWAENDEA NG'OMBE WATATU,MWEUPE,MWEUSI NA MWEKUNDU,SIMBA ALIVYOKWENDA KWA NG'OMBE MWEUPE ALIMWAMBIA KUWA ANA NJAA ANGETAKA AMLE NG'OMBE MMOJA,NG'OMBE MWEUPE AKASEMA KAMLE MWEUSI,NA KESHO KUTWA YAKE KAJA KAMWAMBIA KAMLE MWEKUNDU ASIJUE KUWA BAADA YA WALE WENGINE KULIWA ATAKAYEFUATIA NI YEYE,SIKU ALIVYOKUJA KUOMBWA RUHUSA YA YEYE KULIWA,NDIPO ALIPOKUJA KUSEMA ''NILILIWA SIKU ALIVYOLIWA NG'OMBE MWEUSI'' wana CCM walisahau kuwa baada ya wapinzani kuhujumiwa sasa kitafuata chama chao,ndio haya ya CCM ya akina Polepole