WARAKA WA WAZI KWA LADY JAY DEE kUHUSU WIMBO YAHAYA

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya watanzania ambao wana ji identify themselves kama mashabiki wako wakubwa. But kina kitu kimoja ambacho kwa maoni yangu ninaona hakipo sawa . Nacho ni kuhusu wmbo wako uitwao YAHAYA. Wimbo wako ni mzuri na unaelimisha jamii but kwa nini usingetumia jina tofauti na YAHAYA. Kwanini ninasema hivyo?

1. YAHAYA ni jina la kiislamu, na miongoni mwa majina ya kiislamu yenye maana kubwa kwa waislam.
2. Wewe ni mkristo wa madhehebu ya wasabato.
3. Hapa kwetu nchini Tanzania kuna vugu vugu la waislamu na wakristo. Waislamu wamekuwa makini sana kwa kila kitu kinacho fanywa na mtu yoyote yule mwenye jina la kikristo hususani pale maslahi ya dini ya kiislamu ama jina la kiislamu linapotajwa. Sihitaji kulizungumzia hili kwa kina kwa sababu naamini huwa unafuatilia taarifa mbalimbali za habari so am sure as hell unafahamu ni kitu gani kinaendelea kati ya wakristo na waislamu Tanzania wakati huu.

( KITU CHA MSINGI KUELEWA HAPA NI KWAMBA, KITU CHOCHOTE KILE KITAKACHO TAJWA NA MKRISTO DHIDI YA UISLAMU AMA MUISLAMU KWA NAMNA YOYOTE ILE KINAWEZA KUCHUKULIWA KAMA KASHFA DHIDI YA UISLAMU )

Hivyo basi wimbo wako wa YAHAYA ingawa una ujumbe mzuri, but unaweza kukuletea matatizo na waislamu wa Tanzania ambao wanaweza kuuchukulia kama kashfa dhidi yao. Maadui zako wanaweza kuitumia hiyo kama loop hole na ku dress beef lenu kulifanya lionekane kama beef kati yako waislamu.

MAPENDEKEZO: Nikiwa kama shabiki wako, ninakushauri ubadilishe haraka iwezekanavyo jina la wimbo YAHAYA na kutafuta jina lingine lolote lile. Katika kutafuta jina nakushauri utafute jina ambalo halihusiani na jina la dini yoyote kati ya ukristo na uislamu. Unaweza kutumia majina yanayo tumiwa na watu wa dini zote kama vile MAWAZO.
Ukibadilisha jina la wimbo wako, utajijengea heshima kubwa sana kwa mashabiki wako ambao ni waislamu na watachukulia hiyo kama heshima kwao.
Sina mengi ya kuongea zaidi ya hayo. Natumaini umenielewa.

NAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 13 YA LADYJAYDEE.
 
Wewe ndiyo umeanza kuchochea na uchochezi, mbona kwenye wimbo majina mengi yametumika tu mengine ya kikristu na mengine ya kiislam na wala hatujawi kuona tatizo?

Kaka angalia alama za nyakati, angalia upepo huu wa udini ambao Tanzania tunapitia kwa sasa. Ni kweli majina mengi yametumika mengine kwa ubaya mengine kwa uzuri, but kwa yaliyo tumika kwa ubaya ilikuwa enzi hizo wakati hakukuwa na sekeseke la udini kama lilivyo wakati huu
 
Kila kitu tukiendesha kwa itikadi ya iman hatuwezi kufika....hawezi kubadilisha badilisha mwenyewe kichwani mwako ukiwa unaimba..mbona haukulalamika kwenye wimbo wa Matonya Anitha au Vaileth?J.D akisema hana dini utasemaje maana kubadilisha dini ni kitu cha sekunde..
 
Wewe ndiyo umeanza kuchochea na uchochezi, mbona kwenye wimbo majina mengi yametumika tu mengine ya kikristu na mengine ya kiislam na wala hatujawi kuona tatizo?

Sorry Nyani Ngabu jibu halikuwa lako
 
Last edited by a moderator:
Na wewe Greti Thinka? Mbona majina kibao yameimbwa Idd (Eid) by Juma Nature, Masoud amekuwa jambazi

Nakuoongezea na mengine Kassim na Isihaka. But

Mtoto Iddy .............Juma Nature ni muislamu na umetoka kipindi hicho hakuna vuguvugu la udini Tz.

Masudi ..............Msondo Ngoma/Sikinde: Asilimia kubwa ya waimbaji wakuu kwenye hizo bendi ni waislamu, waimbaji viongozi kwenye hizo bend pia ni waislamu/ nyimbo hizo zimetoka kipindi hicho hakukuwa na upepo wa udini Tz kama uliopo hivi sasa. Sasa hivi udini umewaingia sana watz kiasi huko mashuleni mwalimu wa dini moja akimpa adhabu ya viboko mwanafunzi wa dini nyingine, inaweza kutafsiriwa kama udini. Naamini kama Jide angekuwa muislamu, beef yake na Ruge ingeweza kutazamwa katika sura ya udini
 
Mbona ahmada aliyekuwa amelewa haikuchukuliwa kuwa kashfa? Au side mnyamwezi aliekuwa na mabalaa kibao? Tunakoelekea siko.....

Ahmada imeimbwa na wazanzibari. Side mnyamwezi imeimbwa kipindi hiko hakukuwa na upepo mkali wa udini kama uliopo sasa hivi
 
tukihofu kila ki2 hatutafanya kazi bali tutatafutana kwa ubaya 2
 
acha uchochezi wewe,mbaguzi nini AU ume2mwa?acha kutuharibia nchi bana

Hapana kaka mimi sio mbaguzi na wala siwezi kuwa mbaguzi. Am an enligghtened person. Ubaguzi is for low lives
 
Hakuna chochote apa JD comando 2pe vi2,hawa ndo kina r,,,,,,,uuuu,,g'''''''e part 2
 

Hizo zilikuwa kipindi hicho, halafu Anitha and Vaileth hawakupewa bad image, zilikuwa ni nyimbo za mapenzi tu, but huu wa Yahaya anamzungumzia kijana aitwaye Yahaya ambaye anajihusisha na masuala yasiyo faa katika jamii kama vile utapeli nakadhalika, halafu mbaya zaidi huu wimbo umetoka kipindi hiki ambapo Tz tupo katika kipindi ambacho udini upo juu sana.
 
Hakuna chochote apa JD comando 2pe vi2,hawa ndo kina r,,,,,,,uuuu,,g'''''''e part 2

I cant say ur wrong but please Kimetah accord me some respect, u shall not put me in the same space as Ruge, i was just give my personal opinion. Didint u hear about what happened to JCB?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…