Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ahsate Mkuu!
Hizi ni dalili kuwa Koku aliniulizia....umenionea wapi TF? yuko mitaa gani?
Huyu mama ndugu yangu wa karibu akaendelea kunimaliza kabisaaahajaamka mataputapu aliyokunywa jana bado yamemkamata kichwa
Swahiba nikigeuza mgongo tu kumbe ni nyoka...tobaaaa...dawa yako inachemkaJana aliopoa kimwana akaenda nae kwenye zile G'house za bei chee, nahisi ameng'ang'aniwa huko, ngoja nimpigie kuwa pamekucha aamke... Atalijenga taifa sa ngapi jamani?
:shock::shock::shock:wala usikonde,ameonekana Namnani gest sinza na na mdada mmoja memba wa mmu,oooooops sorry i did'nt mean to tell you really!
Subiri tu Kongosho utaona matokeoTF anafanya EIA saa hizi, kaona umebana feasibility study.
Hakunaga zaidi yangu mimi na wewe...Swahiba nikigeuza mgongo tu kumbe ni nyoka...tobaaaa...dawa yako inachemka
Weee mwanamke kwa saundi sikuwezi...lolHakunaga zaidi yangu mimi na wewe...
Swahiba amini nakwambia hayo maneno sijaandika kwa mkono wangu, wanataka kutuchonganisha haswa Bishanga, eti umekutwa Namnani g'house..
Hakunaga zaidi yangu mimi na wewe...
Swahiba amini nakwambia hayo maneno sijaandika kwa mkono wangu, wanataka kutuchonganisha haswa Bishanga, eti umekutwa Namnani g'house..
acha hizo wewe kama wewe ulikuwa ushaanza mapenzi form 4 usidhani kila mtu...Form 4. atakuwa tayari ana boyfriend ni kheri ukawaisha huu ujumbe aweze kufanya maamuzi magumu
Mwanangu Koku,leo nakuandikia waraka huu nikiamini utakusaidia leo na siku za usoni hata kama sitakuwepo duniani.
Mwanangu,najua unatamani uwe mtu mzima ikiwezekana hata leo ili uondoke nyumbani uwe 'huru' kufanya unavyotaka na kupanga muda wako unavyotaka.Ni kawaida kwa mtoto kuwa na hamu ya kuwa mtu mzima.Kumbuka kipindi utakachokuwa mtu mzima ni kirefu kuliko kipindi cha utoto,hivyo haina haraka,inshallah mola akujalie uhai mrefu.Kumbuka maamuzi unayoyafanya leo ndiyo yatakuamulia maisha yako ya baadae.
Hakuna jipya chini ya jua hili,mbinu za kupata mafanikio zishajulikana,jifunze mbinu hizo,zitakusaidia.Usifanye jambo eti kwa kuwa wengine wanafanya hivyo,tenda jambo ambalo nafsi yako imekubaliana nalo,usifuate mkumbo,fuata dhamira yako.Kwepa vishawishi vinavyoweza kukutia aibu wewe,familia yako na jamii inayokuzunguka,miliki maisha yako.Kizazi chenu ni cha dot.com,kizazi cha facebook,twitter,bbm na kadhalika,kuwa macho katika ulimwengu wa cyber ,usiwe mwepesi wa kuzoeana na watu wala kutamani ukutane nao,inaweza kuwa hatari.Usijiruhusu kuwa 'addicted' na dunia hii ya mtandao,be real.Jifunze dunia inakwenda je na usitumbukie katika mtego wa kufuatilia maisha ya watu wengine.
Mwanangu,litakapokuja suala la kutafuta kipato,kazi kwanza starehe baadae.Osha vyombo kabla ya kuangalia TV,fanya homework kabla ya ku chat na marafiki zako,hii itakujengea nidhamu siku za usoni,ila usiache kujiburudisha ukipata muda,msongo wa mawazo(stress) ni mbaya.Shibisha moyo wako kwa dua.
Litakapokuja suala la kuchagua taaluma ,ikiwezekana chagua taaluma ambayo unaipenda,fuata moyo wako usijilazimishe kufuata mkumbo au kunifurahisha mimi mzazi wako.Katika taaluma yako fanya kazi kwa bidii na penda kazi yako.Hakuna mwajiri huwa anamlipa mwajiriwa stahiki yake,jifunze kudai unachostahili kulingana na uwezo na mchango wako kwa mwajiri.
Nimekufundisha kuweka akiba,endelea kutunza unachokipata,usitumie zaidi ya kipato chako.Pesa zako ni zako,usiruhusu mtu mwingine akupangie matumizi ya pesa zako,labda iwe ni kwa majadiliano lakini si kwa shurti.Usicheze kamari,kuiba wala kujiunga na mipango kama ya DECI.Hakuna pesa ya bwerere,pesa hutafutwa kwa jasho,na kwa maana hiyo kamwe usiuze utu wako kwa ajili ya pesa,una uwezo wa kutafuta pesa kama walizonazo hao wengine na kwa njia halali.
Utakapoingia kwenye mahusiano,usiangalie wengine wanasema nini,angalia wanafanya nini.Kuna siku utatumbukia kwenye lindi la mapenzi na utajiuliza 'hivi huyu ndo Mr Right?'.Ataweza kuwa ataweza asiwe.Akikuumiza usilie kupita kiasi ,jikusanye nyanyuka na usonge mbele.Muda ndo dawa ya machungu ya mapenzi,jipe muda utasahau,usijiue kwa sababu ya mtu mwingine mwenye baba yake na mama yake ambaye mmekutana ukubwani.Ukiolewa kumbuka mmeo kamwe hawezi kuwa baba yako,never.
Kuwa na marafiki wachache lakini wa ukweli,kuna siku watakusaidia.Epuka kuwa na watu wanaokusifia tu,anayekukosoa ndiye bora zaidi hata kama inauma.Ogopa marafiki wambeya na wasengenyaji,hata wewe watakusengenya.
Katika maisha yako utakutana na vikwazo vingi,jifunze kutokuwa na haraka ya kutoa maamuzi,tatizo lala nalo,litolee maamuzi ukiwa umetulia.Mwanangu,mdomo uliponza kichwa,chunga sana ulimi,neno likishatoka mdomoni ni kama cement ikisha kuwa zege hairudi kuwa cement.
Mwanangu nakutakia maisha mema yenye baraka tele,na siku zote ujue ninakupenda sana hata kama kuna wakati huwa unaona nakukwaza,yote huwa ni kwa nia njema tu.
Baba yako,
Bishanga Abashaija
Dar es salaam
29/11/2011
mjibie,si mmeo mtarajiwa?
Hebu msome Bishanga jamani, khaaa anatuchonganisha live bila chenga, kongosho keshathibitisha kuwa jf kuna wezi wa pasiwedi ati. Isijekuwa klorokwini aliiba p'word yangu.Weee mwanamke kwa saundi sikuwezi...lol
Bishanga unavyokazana kunichonganisha na TF,akigoma kunipeleka vekesheni utanipeleka wewe?SL sijui anakuogopa nini,una mipembe? Kukosa ukose wewe msamaha aombe SL,kha!!!!
ahsante mwanangu,i wish you a bright future.kwanza hongera sana bishanga kwa wosia mzuri kwa mwanao..umegusa kila sehemu ya maisha ya kila siku.wewe brain imetulia inaelekea sio mchezo.nadhani pia koku nae anaelewa ndio maana umeweza kumapatia wosia kama huu.mungu akujalie ukae na mwanmke ili utengenezie picha nzuri kwa mwanao kuwa maisha ni ndoa isiyovunjiak til death apart you.usiishi single parent. nakutakia malezi mema
you ve brighten my future as well maana me nko form 5