HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,567
Habari za leo wana MMU?
Kwanza, naomba msamaha kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wasingependa kuzisikia tena habari za The Great. Si nia yangu kuwatonesha kidonda bali kuwashirikisha yale ambayo nimeona tunawezakujifunza kama watanzania wenye nia na mapenzi mema, ili yakafanyike kuwa msaada kwetu na kwa wanajamii wenzetu.
Pili, kwa takriban wiki moja sasa, vyombo vya habari nchi Tanzania vikiwemo redio, magazeti na TV vimekuwa vikiripoti tukio la kumpoteza ndg yetu mpendwa the great! Binafsi, na mimi pia ni mmoja wa watanzania walioumizwa na kutoweka kwa ndg huyu. Naamini ni wengi ambao waliguswa sana na kifo hiki kutoka na ukaribu na ukarimu wa huyu ndg kwenye maisha yao ya kila siku. Wapo pia walioguswa na hili tukio ili kujipatia maslahi yao binafsi kwa kuuza habari na kuzusha mambo mengi yasiyo ya kweli ili kujipatia kipato cha udhalimu. Na pia wapo waliotumia msiba huu kama sehemu ya kwenda kufahamiana na wasanii na watu wengine mashuhuri. Kwa wote waliguswa kwa nia njema, nawapa pole sana na Mungu awafute machozi na kuziondoa huzuni zao!
Kwa nini nimeandika waraka huu?
Pengine ni kwa sababu ya kuguswa na hisia za maumivu ya mioyo ya watu juu ya tukio hili la kumpoteza ndugu yetu the great. Vyombo vya habari bado vinatukumbusha kila siku. Hotuba za viongozi wetu bado zinamtaja! Hata Juzi kwenye Kili Awards kauli za waliohojiwa bado wanashindwa kusema lolote bila kuacha kumtaja Kanumba. Nilikuwa kwenye sherehe moja Jana, nikamsikia binti mmoja akimwambia mwenzake kuwa siku hizi anaogopa kulala usiku pekee yake akihisi 'the great' anaweza kumtokea! Hizi ni dalili za wazi kuwa jeraha hili bado ni bichi na tunahitaji kufarijina ili tuweze kurudi katika hali ya kawaida.
Nini tumejifunza?
Tukiwa na maisha ya amani na watu, tukaondoa chuki na ubinafsi tukaacha tamaa pia, basi tunaweza kuishi maisha ya kuwa mfano.Kanumba kazikwa kishujaa kwa sababu ya aina ya maisha aliyochagua mwenyewe kuishi. Kwa sisi wana MMU tuliobaki, hatma ya maisha yetu ipo mikononi mwetu. Bado tuna nafasi ya kuishi maisha ambayo yanaweza kukumbukwa na vizazi vyetu vijazo badala ya kuwa na maisha ya kifisadi yatakayotuletea hukumu siku ya mwisho. Tubadilike!
Hitimisho
Nafikiri ifikie wakati sasa, watanzania wote tukubali kuwa huyu ndg hatuko naye tena duniani. Ni wakati wa kutambua kuwa yeye aliyetoa ndiyo huyo huyo pia aliyetwaa. Ni vizuri sasa kuukubali ukweli huu ili kuzinusuru akili na fahamu zetu ziweze kufikiria katika kuimarisha na kuenzi kazi zake badala ya kutumia muda mwingi kuendelea kulia na kuomboleza. Tukubali kuwa tumelia sana, tumeumia sana na pia tumehuzunika sana na sasa ni wakati wa kuyajaribu maisha bila ya kuwa na shujaa huyu wa tasnia ya filamu. Ningetamani vyombo vya habari visaidie kuwafariji watu na kuwaondoa majonzi badala ya kuendeleza hbr za huzuni, uchochezi na kujenga chuki baina ya wanajamii waliotuzunguka. Ni vigumu kumpata mtu kama huyu tena, ila yeye aliyemtwaa anafahamu ni kwa kiasi gani watanzania wameumia ni nini cha kutufanyia ili kuweza kuikabili hii hali.
Nawaombea Mungu wa amani awafariji kwa faraja na baraka zake kuu. Tuamini kuwa sisi ni binadamu, na hii dunia si sehemu yetu ya kudumu na hivyo tujitahidi kutenda mema na kuishi na watu vizuri kujiwekea thawabu kwa maisha yetu baada ya haya ya duniani na kuacha kumbukumbu kama ya the great. Tupinge na kusaidiana kukemea maovu. Tuamini ya kuwa kazi ya Mungu haina makosa. Tudumu kutenda mema.
RIP the Great na wengine wote ambao bado mioyo yetu inawakumbuka kama Sokoine, JK Nyerere, Fanueli Sedekia, Angela Chibalonza, Rehema Mwakangare, Damian Kanuti, James Dandu, na wengineo wengi.
Poleni Watanzania,