meona maandishi mengi nikadhani nitapata jambo la maana humo lkn nilichoambulia ni kichefuchefu cha kumfananisha Kanumba na Sokoine. Wewe huna tofauti na yule mchungaji aliyeongoza ibada ya kumuombea marehemu iliyoandaliwa na wasanii wenzake ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa mtumishi wa Mungu.
Mtanisamehe Pro-Kanumba, mimi huwa sipendi unafiki. Huyu mtu ndio kafa na anastahili heshima kwa mazuri ambayo mimi BINAFSI siyajui. Lkn inapofikia sasa tuanze kuaminishwa kuwa alikuwa mtakatifu kwa kuwa tu mliishi kwa kumsujudia, mimi sioni mantiki. Rejea maandishi yako mtoa mada Mimi si Mungu wa kuwahukumu watu, lkn na wewe ni nani wa kuwasafisha tena bila hata aibu?
Wote tumesikia mazingira ya kifo cha Kanumba. Sasa unaupata wapi ujasiri wa kujaribu kutuaminisha na kututamanisha kuomba kifo kama cha Kanumba? Lets stop this illusions. Hakuna mazito ya kulisaidia hili taifa kutoka kwa Kanumba (kwa mtizamo wangu), makubwa katika kazi zake (na wenzake) ni uharibifu wa jamii yetu. Bongo muvies na wanachama wake ni taswira mbaya kwa Taifa lkn kwa kuwa sisi tunaathiriwa na utandawazi kwa namna mbaya, basi Kanumba kwetu ni nabii na tunaamua kumuabudu. Tena mbaya zaidi, tunapofuka macho na kushindwa hata kuona kuwa mwisho wake kimaadili haukuwa mzuri.
Mimi simkatazi mtu kuamini anachoamini, lkn punguzeni kauli mjumuisho. Kusema Taifa limepoteza mtu muhimu, maana yake ni kunilazimisha hata mimi ambaye ninaamini kuwa Kanumba na wenzake ni wapotoshaji wa jamii yetu tuamini mnavyoamini nyinyi msiojua zamani tuliishije na sasa tunaumiaje.
Juzi (kama sio jana), kwenye JAMII PHOTOZ, kuna mtu alipost picha ya watu wawili wakiwa kitandani wanapapasana mapaja. Kilikuwa kipande cha picha kutoka kwenye moja ya maigizo yetu ya Bongo. Je hicho ndio tunachokililia kwa Kanumba kufa? Haya ya Lulu, umri wake, jinsia yake na uhalisia wa mazingira ya yeye kuhusika na kifo cha Kanumba uliyazingatia kabla hujaandika huu waraka wa kumtuza marehemu?
Binafsi nafikiri umefikia wakati sasa tuishi kwa malengo. BONGO MUVIES na waigizaji wake ni uchafu. Haya mabadiliko yanayotukumba tukiwa hatuna elimu ni sumu kwa taifa. Watoto wetu wako bize na Kanumba na Shigongo kiasi hawana muda wa kusoma vitabu bora na magazeti yenye msaada kwao na hilo linachangia yale tuliyoyaona kwenye matokeo ya kidato cha 4 na kujifanya tunajali na tumeumia. Hivi kwa akili tu ya kawaida, wapi kwenye gazeti la Uwazi unaweza kusoma makala ya uchumi au historia zaidi ya Ray kampa mimba Amina, Lulu kabakwa kolabo, Anti seche katoa mimba ya kigogo, wema sepeku abamizwa makofi na mke wa buzi lake,.....n.k?!
Najua haya maoni yangu yatawakera wooote wanaoishi kwa hisia. Lakini mimi ni Mtanzania kama ulivyo wewe na haya ndio maoni yangu. Huu unabii wa Kanumba mimi naukataa. Wote tutakufa lkn hicho sio kigezo cha kukienzi kifo kichafu cha Kanumba kwa wewe kutuasa tuepuke ufisadi na tufe vizuri na kwa amani kama Kanumba. Tafakari mwisho wake halafu jiulize kama kweli upo sahihi