Waraka wa wazi kwa wana MMU kumhusu “The Great”!

mtaandika mengi haya bado hayatoshi,anayeweza kuhukumu ni mungu tu na si vinginevyo.nachukia mijitu inayokalia na kukomalia kanumba alikua mzinzi.mnajuaje alizini na yule lulu wakati hata set aliambiwa wajiandae watoke.kanumba alisema yuko single mnajuaje ndo walikua anaanza kurusha nyavu mtoto akaonyesha ucharuko.tusubiri anaehukumu afanye kazi yake sio kuropoka yawatu wakati mifuko yetu imeoza.
R.I.P the great
 

Well said mkuu...kula like 3!! mkuu...ulichosema ndo uhalisia,kuna ***** alisema kilicho baki tumuombee nikamjibu ILI IWEJE? aka ni block
 

Na tusubiri anayetoa haki afanye kazi yake. Ukiwa na akili angalau kidogo, utagundua kuwa kuna biashara chache sana ambazo hufanywa usiku wa manane. Kwa umri wa Lulu, kama kweli unataka kumsaidia na si kumharibu, basi mchana utamfundisha kuigiza na ikifika saa 12 jioni utamrudisha kwa mama yake.

Nashukuru kwa kuwa muwazi kuwa unawachukia watu wengine. Na hizi hasira zako nazo ni dalili ya kutokomaa kiuelewa, ndio maana umeshindwa kutofautisha uhalali wa chuki yangu dhidi ya upotofu wa chuki yako. Mimi simchukii Kanumba wala wewe, nachukia tabia alizozionesha Kanumba na nachukia tabia za watu wenye kuhalalisha maovu kwa kuwa tu yamefanywa na watu wanaowapenda.

Kuonesha jinsi usivyoweza kuuona ubaya tazama matamshi yako mwenyewe:
kanumba alisema yuko single mnajuaje ndo walikua anaanza kurusha nyavu mtoto akaonyesha ucharuko
Kwa hiyo kwa sababu Kanumba ni "The Great" basi ana ruhusa ya kutongoza vitoto kwa kisingizio cha kuvisaidia, eti eeh?

I never sweet-talk porn stars just because they died.

Labda nikuombe Mkuu, usinichukie mimi, zichukie tabia zangu za kukosoa bila woga hata kama Jamii nzima ikisimama upande tofauti. Kanifundisha mjomba wangu, aliniambia siku zote nisimamie ninachoamini hata kama kitanigharimu.
 
Cha muhimu kujifunza ni kuwa tayari wakati wowote kwani hatujui siku wala saa. Hakuwa fisadi wa mali lakini alikuwa fisadi wa mapenzi so huwezi kumsafisha namna hiyo. All in all Mungu ndo mwenye kutoa hukumu ya mwisho.
 
Akili za Watanzania walio wengi sidhani kama ziko sawa sawa.........kuna tatizo somewhere!!
 
Kuna watu humu wako tayari wazazi wao wangekufa kuliko mzinzi mwenzetu Kanumba..... Mitanzania bana. Mizembe kama kikojoleo cha jogoo. Badala ya kumwonea huruma mtoto Lulu kuingia katika matatizo ya wakubwa, wao wanamlilia mzinzi mwenzetu. Nami nikifa afu msinililie ntamwomba Mungu ahamishie vikojoleo vyenu usoni. *****!
 

Mzee mwenzangu,

Yaani wengine tunashangaa hadi hatuelewi au kuelewaki, inawezekanaje Kanumba alinganishe alinganishwe na Nyerere au Sokoine?

Babu DC!!
 
Mzee mwenzangu,

Yaani wengine tunashangaa hadi hatuelewi au kuelewaki, inawezekanaje Kanumba alinganishe alinganishwe na Nyerere au Sokoine?

Babu DC!!
Mzee mwenzangu,
Miafrika Ndivyo Ilivyo... Source NN.
 
Tulichojifunza ni namna gani taifa letu halina vipaumbele, wakati taifa zima na viongozi wa kitaifa wakijipanga kwa kutumia pesa za walipa kodi eti to pay tribute to Kanumba na kumshutumu mtoto wa miaka 16 kwa kuua, aliyekua mkuu wa majeshi na mpiganaji aliyeshiriki kuongoza vita ya kumg'oa Iddi Amin dada anazikwa kama mbuzi. Hii ndio Tanzania yenu. Katika mazishi ya jenerali Kiaro nasikia serikali hii iliwakilishwa na mkuu wa mkoa, waandishi wa habari pia hawakua mbali katika kubariki udhalimu na unyang'anyi wa utu wa kiaro maana hata tukikusanya maandiko yao hayatajaa kiganja, ila wahariri wako busy kugombana na RPC wa kinondoni maana hakumuacha lulu wazi ili wampige picha na kelezea kwa akili zao kile anachdhani ni hisia za mtoto huyu waliye m label malaya. Nchi, viongozi na waandishi walioweka ngono kama kipaumbele cha taifa letu, Kiaro hauzi hana story hata katika miaka 50 yake ya kulitumikia jeshi, na nchi hii kwa kutukuka, waandishi hawana mambo ya kutosha ya kulielezea taifa hili na vizazi vyake juu ya kile alichofanya Jenerali Kiaro katika miaka yake 50, sawa na uhuru wa nchi hii. Ndiyo maana mtoa maada bado anataka tumshabikie mwana maigizo asiye mtunzi, aliyeishia kucheza sinema za kubadilisha zile za nollywood leo tunamuita mtu aliyeitangaza Tanzania kuliko wapiganaji waliolirudisha Taifa letu toka kwa dhalimu Iddi Amin, ambaye pengine kama asingezuiwa, angetugeuza watanzania mishikaki kama walivyofanywa warwanda, hili kwa watanzania na viongozi wetu na wake zao sio la muhimu kama mapenzi anayoonyesha Kanumba kwenye sinema za ki nigeria zilizo tafsiriwa kwa kiswahili. Ndio maana mtaishia kutembea kwa miguu eti mnaenda Kilioni lakini watoto wenu mnataka msomeshewa, mifereji ya maji machafu mzibiwe na serikali. kalagabaho
 
Hatimaye watu wenye akili nao wamejitokeza kuchangia


Ndugu yangu,

Watu waliamua kukaa kimya ila sasa uchokozi na upotoshaji unataka kuvuka mipaka.....


Kwa mtu mwenye akili na anayeilewa hii Tanzania katika awamu zote tatu, haweza kukaa kimya akiona viongozi waliotumikia nchi hii kwa utumishi uliotukuka na uadilifu wa hali ya juu wakiwekwa kwenye kundi/mzani mmoja na wasanii. Tena wasanii ambao utendaji wao hauwezi kuchujwa na kupita kwenye chekecheo lolote!

Anyway, wengine tumefikia hatua ya kukubaliana na matusi ya Mkapa kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikirii na JK aliyesema kuwa Watanzania wanafuata upepo.

Hata kama hayo matusi ni ya kweli, hivi hakuna hata watu 10 katika ya watu mil.40 wa nchi hii ambao walau bado wa akili???

Babu DC!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…