Yah,mi ni msomi mzuri sana wa hadithi,na mpaka sasa kuna watunzi ambao nimekuwa nikiwaheshimu sana kwa riwaya zao kama BEN MTOBWA(R.I.P) na vitabu vyake kama tutarudi na roho zetu,najisikia kuua tena,nyuma ya pazia,mtambo wa mauti,Salamu kutoka kuzimu;MUSIBA na kisasi,hofu,gongo la chuma,njama,HUSSEIN TUWA na mkimbizi,mtuhumiwa,mdunguaji.Hao jamaa ukisoma vitabu vyao lazima mwili usisimke,vinatia hari ya mapinduzi,moyo wa uzalendo,moyo wa kuipenda nchi yako.Niliumia sana alivyofariki Mtobwa maana nilijua wanaisha na hawaibuki wengine,lakini nilifarijika nilivyoanza kuviona vitabu vya Hussein Tuwa.Ukiangali makala nyingi sana za MWANAKIJIJI utaona ni jinsi gani alivyo na moyo wa kizalendo,nimesoma hadithi yake hiyo juu pamoja ni ya mapenzi lakini waweza kuona utaalamu na umahili wake unaopelekea kumfanya msomaji asikiweke chini kitabu na asahau mambo mengine.Mi nadhani kwa Ushauri wangu kwa Mwanakijiji atunge vitabu vingi vitakavyolenga kumpa hari kijana yeyote wa kitanzania achukie Rushwa,apende nchi yake,Awe tayari kufa kwa nchi yake na aviingize sokono kwa wingi.Nasema hivi cuz mimi ni zao la vitabu hivi vya akina Mtobwa,namshukuru uncle wangu kwa kuniletea vitabu hivi tangu nikiwa la kwanza(cuz they made me who i am now).