Warioba afichua siri nzito

kwani warioba kala shilingi ngapi? si keshasema hesabu zote ziko safi?
 
Alikuwa wapi siku zote mpaka aje na kusema baada ya kubanwa, sisi tutasema siku zote na yeye pia atasema na pengine vyombo kama mahakama ndio zinaweza kuwasafisha na sio vyombo vya habari
 
Ni wizi mtupu serikali ambayo iko busy kuuza mashirika ya umma kwa upande mmoja, upande mwingine inayaanzisha bila hata kufuata taratibu. Mwisho wa yote ni kuwa haikuwa serikali bali ni janja ya watu wachache kutaka namna rahisi ya kuchota fedha za walipa kodi.Ila ntacheka sana kama hata hili nalo litawekwa kwenye lile kablasha lisiloguswa wala kuruhusiwa kulitamka hadharani.....usalama wa Taifa.Tuwaeshimu hawa jamaa wajameni.
 
Hapana shaka kuwa huyu mzee naye Fisadi na tena kwa siku za karibuni amekuwa haeleweki kuwa yupo upande gani
 

Hapo nashangaa kuona unasema makini....yah umakini tuliou fabricate katika nchi yetu au? Maana kama ni umakini basi hayo yaliyofanyika yasinge raise a lot of questions ila kwasababu tumekua na attitude ya kubariki makosa ya 'washika hatamu' na kukuza makosa ya 'washikwa hatamu' no wonder hata wewe badala ya kuona chongo ukaona kengeza.

Kama anafuata kanuni ya 'kuinama na kuchora chini' akumbuke alienzisha hiyo kanuni yeye pekee kati ya wote waliokuwapo hapo (mshitakiwa na washitaki) ndo hakua na tone la doa and if that is the case hata mimi namwombea kwa mola asiwepo wakumpeleka ila kama ni kwa mtindo wa kosa ni kwa wale tu nje ya 'kushika hatamu' hapo naomba na roho mtakatifu asaidie washitaki katika kudevelop kesi itakayoshinda ku tokomeza hii kansa ya ufisadi kwani ni mbaya kuliko ugonjwa wa ukoma and masses are falling victim of it na kupoteza maisha every hour kwa kukosa dawa, elimu, furaha, amani, upendo na mbaya zaidi kupoteza uzalendo na ari ya kufanya kazi.
 
Sisi tulisema mapema kuwa anaweza kusaidia mahakama kama alishiriki vipi na mipango ya wizi kama ile ya kuanzisha makampuni ya ajabu na yanakuja kufa katika mazingira ya kutatanisha kama haya
 

Naona hii style ni nzuri sana na itasaidia kutupeleka kwenye rule of law na baadhi wanaopenda shortcut za maisha kuwa makini kama endapo watakubali kutumiwa dont you think so? I think we will ultimately agree kuunda system itakayolinda maslahi ya nchi na siyo inayolinda individual interest. NAIPENDA HII STYLE na naomba idumu mpaka hapo tutakapo nyooka na kukubali rule of law.
 

Dada siyo kutaka to shortcut ya maisha kwa sababu pesa wanazo tengeneza katika uongozi ni nyingi sana na wanaweza kuzitumia kuwa na biashara kubwa tu za kihalali. Tatizo ni tamaa na kutokuridhika. Pesa mbunge anazo pata kwa mwaka tu ukijumlisha base salary na incentives zinigine zinatosha tu kuwa na maisha mazuri na akikaa miaka mitano inatosha kabisa kuwa tajiri tena kihalali. Tatizo viongozi wetu wamekua kama mbu ambao wana tunnyonya damu mpaka wahakikishe wamevimbiwa.
 
Kwanza yeye alikuwa wa kwanza katika kupinga List ya Mafisadi wakati ule mwaka 2007 sasa yeye atasema
 
UPEPO WA ufisadi ulishampitia huyo mzee ni kama kingunge tu alivyouacha ujamaa na kuanza ufisadi uzeeni,
tungemuelewa huyu mzee kama kweli anataka maslahi ya taifa muda mrefu kama angekuwa anapigania uwepo wa kampuni hii, lakini sasa kila siku ni mbio kwenye vyombo vya habari ili ajisafishe ufisadi wake, magazeti, radio, tv aviwezi kumsafisha fisadi, ni mahakama pekee ndio inaweza kukusafishan kwa maji safi
 
Huyu jamaa alitumika katika mipango ya kishetani ya ajabu kama haya na leo baada ya mtandao kufa ameachwa pekee yake
 
Hapa ndipo unaweza kugundua maovu na vificho na nia na roho mbaya za viongozi wetu wa Kitanzania. Hili ni bomu katoa huyu mzee..!Viwanda vingi Tanzania vimekufa kutokana na nia na malengo mabaya ya viongozi wakitanzania kwa faida zao binafsi,

Tumekuwa na viwanda vingi muhimu, mfano kiwanda cha mbolea Tanga, Canvas, Morogoro na sehemu zingine..viwanda vile vimekufa pasipo sababu za msingi..Hapa Mzee Warioba anataka kutueleza jambo ambalo ni lazima tuwe makini na ni msaada ameutoa kwa watanzania ...Huu ni ufisadi unaoendeshwa na viongozi wetu kwa faida zao binafsi.
Mzee Warioba Kama anamakosa yake,sawa tusikatae.Tuyajadirini baadae mara baada ya kufichua hiki kitendawili alicho kileta mbele yetu .Hii ni siri anayo itoa leo mbele ya watanzania jamani , Hii si ni kashfa kubwa kwa Taifa ? Je inatofauti gani na ile ya kule kwenye mbuga za wanyama walikokuwa wanasafirisha wale Twiga kwenye midege kuelekea Uarabuni ?
Haya madini yalikuwa yanapelekwa kusafishwa na kuuzwa nje kinyemela, wamepata kilo 100 za Gold waka kwambia tumepata kilo 10 tu , Hii issue imekaa kienyeji , ..! Jamani tupo wapi watanzania .Hili tunatakiwa kulifanyia kazi..ni kwa faida gani Tanzania iliona itapata endapo itafunga kiwanda chake na kwenda kusafisha madini nje ya nchi ?

Hata huyo mzungu atakucheka..! Unachupi yenye kukuenea na kukutosha nyumbani kwako kwanini watembea uchi kwenda kuvaa chupi ndogo yenye kukubana kwa jirani yako ...mtindo gani huu..!!

Waandishi wa Habari kama mwaweza mwomba mzee mkutane nae awaeleze zaidi issue hii..!! Lipo jambo hapa..!
 
Mfa maji aachi kutapatapa,huo ndio mwisho wao mafisadi.Wakishadhulumiana mambo yote huwa kweupeee.
 
Mode, hiyo rangi nyekundu inaumiza macho please! Otherwise the story is interesting!!
 
Nadhani walimuambia atulie watampa Kitengo Nyeti cha Kihistoria akamezea kumwaga Siri...

Nchi watu wengi Wanakufa na Siri zao Mioyoni.... Wanamugopa zaidi Binadamu kuliko Mungu Wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…