Hofu ya ccm katika hili ni mbili:
1.CCM kupasuka kuliko muungano kuvunjika, na hii ilikwa ni msingi kwa serikali na kamati ya wabunge wa ccm kuuusu hoja ya G55 bungeni wakati ule. Uamuzi ule ulilenga kuizuia ccm isipasuke kuliko kuzuia muungano usivunjike. Ni nyerere ndiye aliyekuja na uamuzi ambao ukaiokoa ccm, huku kuokoa muungano likiwa ni suala secondary (primary kwa nyerere). Lakini kwa vile suala la kuiua Tanganyika ni suala lililokiuka mkataba wa muungao, solution za kuliweka tatizo hili chini ya carpet kamwe haitazaa matunda na ndio maana limerudi tena. Hadhi ya kweli ya znz katika muungano haiwezi kupatikana bila ya kuzinduliwa kwa Tanganyika ambayo imekuwa kwenye coma kwa miaka 46 (1967-2014). Na kadri wazanzibari wanavyoendelea kurudi kwenye yaliyokubaliwa kwenye mkataba wa muungano (1964) ndivyo watanganyika wanavyozidi kuamka kujua ukweli wa historia na pia umuhimu wa kuzindua Tanganyika yao. Katika suala la Tanganyika, hakuna kurudi nyuma, na hii agenda itaigharimu sana ccm uchaguzi 2015.
2. Hofu ya pili kwa ccm ni kwamba tangia muungano uzaliwe, CCM imekuwa iki focus zaidi katika controlling people (kudhibiti watu) kuliko controlling territory (kudhibiti eneo lake la asili la utawala), kwani chama kina amini kwamba mtaji wake wa kutawala ni kwa kudhibiti watu zaidi ya eneo lake la utawala (Tanganyika), na kwa mantiki hii, ikawa tayari na bado ipo tayari kuisaliti Tanganyika ili mradi tu himaya yake isambae hadi zanzibar kupitia mfumo wa serikali mbili. Lakini kweli unabakia wazi kwamba nguvu ya ccm znz haijawahi kuwa ni nguvu ya TANU bali ndoa yake na ASP. Serikali tatu itapelekea mgogoro wa ndoa hii hivyo legitimacy ya ccm znz kuwa mashakani. Ccm ilifanya kosa kubwa kuchakachua mkataba wa muungao kupitia TANU pale ilipoingiza suala la vyama vya siasa kama ni suala la muungano nje ya mkataba ule kwani mkataba haukutaja vyama vya siasa. Iwapo TANU isingefanya hivyo kupitia sheria za muungano 1965, sheria ambazo hazikuishirikisha znz, leo ccm isingekuwa na wanachoita "changamoto za muungano" kwani siasa chini ya federation zingeendelea bila matatizo unlike under the current forced unitary structure.
CCM itaendelea kupigania masuala mengi ya katiba ya jmt 1977 yaendelee kwa vile katiba hii ilijengwa juu ya nguzo kuu zifuatazo:
1. One party state (CCM) ambapo baada ya muungano kuishi chini ya katiba ya muda kwa miaka 12 (1965-1977), ikadhaniwa kwamba solution ni kuunganisha vyama vya siasa, hence kuishia kuufanya muungano kuwa ni wa kisiasa huku uchumi ukitumikia siasa husika. Katika kipindi hiki CCM ika transform kutoka a political party into a state party controlling all politics. Leo tunaishi chini ya mfumo wa vyama vingi lakini multipartism sio sawa na democracy. Hakuna demokrasia Tanzania. Na isitoshe, chini ya katiba ya sasa, what we have is the rule of the registrar rather than the rule of law.
Serikali tatu will destroy mfumo wote hapo juu, lakini muhimu zaidi, legitimacy ya ccm zanzibar itapungua kwani maana nzima ya TANU + ASP itakuwa haipo tena. Legitimacy ya ccm Tanganyika ndio itakwisha kabisa kwa vile ccm ilishaukataa utanganyika, kwanza kwa kukifuta TANU lakini pia kwa TANU kuifuta Tanganyika kwa mujibu wa sheria namba 24 ya 1967.
2.Nguzo ya pili ya katiba ya sasa ni the Two governmet union structure kama nilivyojadili hapo awali.
Mwisho - nazungumza haya kama mwana ccm ninayeamini katika ccm kuanza upya na kurekebisha makosa ya huko nyuma kwani hivyo ndivyo sisi vijana tutaweza endeleza chama hiki na kurudisha imani kwa wananchi hata kama itabidi kuwa chama cha upinzani kwa muda. Siasa za kpokezana vijiti ndio demokrasia, tunahitaji ccm ambayo itakuwa inashinda au kushindwa on an equal playing field. Ushindani wa aina hii ndio wa maana na sustainable, sio ushindani wa ujanja ujanja.
Kinachosikitisha sana tena sana ni vijana waliopo ndai ya NEC, CC kwenye chama kutoona haya. Badala ya kupigania ccmm mabadiliko ili mbeleni waendelee kwa na legitimacy kwa umma hasa ikizingatiwa kwamba bado waa umri mdogo na safari ndefu kisiasa, wao wanaegemea kwa wazee ambao wanaja walishaharibu suala zima la muungano na kwa vile muda wao madarakani hauzidi miaka 20 kutokana na umri, wazee hawa wanapigania kuendeleza mfumo wenye makosa kwani ndio umewafikisha hapo. Kweli vijana mpo tayari kurithi chama chenye migogoro hii ambayo mnaibatiza jina la "changamoto za muungano"? Ni kweli hamuelewi maana ya Tanganyika ndani ya muungano?
Tunashukuru angalau wazee kama warioba, na wengine wameona kasoro zilizopo na wana nia nzuri sana ya kukiokoa ccm ya vijana wa sasa (sio wazee), kuokoa muungano, na pia kokoa machafuko kwa kuifufua Tanganyika kwani bila ya Tanganyika, zanzibar wanayoitaka wazanzibari kihadhi na kihali haiwezekani, na bila ya Tanganyika, kwa vijana wengi sasa, Tanzania haiwezekani kwani wamengudua kwamba Tanganyika kumbe haikutoweka bali imekuwepo kwa miaka 50 ikiwa imevaa koti la muungano ikiitwa Tanzania bara.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums