Warioba amewasilisha rasimu ya katiba au rasimu ya serikali tatu?

Warioba amewasilisha rasimu ya katiba au rasimu ya serikali tatu?

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,570
Takribani zaidi ya masaa matatu aliyotumia Mwenyekiti wa Mchakato wa Katiba Mpya, Jaji Joseph Sinde Waryoba kuwasilisha kile kinachoitwa(nasema ni kile kinachoitwa kwa vile sasa maana halisi ya Katiba Mpya haipo tena) Rasimu ya Katiba Mpya alitetea (na siyo kuwasilisha maoni ya wananchi) muundo wa Serikali tatu.

Watanzania wengi kutoka makundi mbali mbali wakiwemo Wakulima, Wafugaji, Walemavu, Watoto, Vijana, Wanawake, Wazee na mengine mengi wamebaki wameduwaa na kujiuliza maswali mengi kama kilichowasilishwa jana bungeni ni Rasimu ya Katiba Mpya au ni Rasimu ya namna gani ya Muundo wa Muungano unawafaa watanzania, hoja ambayo pasi na shaka ni kwa manufaa ya wanasiasa.

Jmbo kubwa ambalo watu wamebaki wakijiuliza ni namana ambavyo Waryoba alitumia nguvu nyingi kutetea hoja ya serikali tatu huku akijua kabisa katika mchakato mzima wapo watanzania tena wengi tu ambao ni waumini wa Serikali mbili na wengine akiwemo yeye mwenyewe ni auminini wa serikali moja.

Watu wanajiuliza Waryoba ambaye ni muumini wa serikali moja alishikwa na nini au kuna nini kimejificha juu ya msimamo wake katika serikali tatu na kusahau kabisa kugusia hata serikali moja ambayo yeye anaaamini ni nguzo imara ya Muungano?

Lakini kubwa ambalo Makungi ambayo jana yamesaulika kwenye hotuba ya Jaji waryoba yanajiuliza ni wapi watasimama kuhoji haki zao kwenye Katiba itakayopatikana wakati tangu mwanzo wameonekana kusahaulika?

Mytake: Iko haja kubwa kabisa ya Wabunge wa Bunge maalum la Katiba kujitazama upya kuhusiana na rasimu hiyo la sivyo kuna kila dalili kuwa Katiba inayokwenda kuandikwa ni kwa ajili ya Wanasiasa na watu kama akina Waryoba ambayo yawezekana kabisa kuna kitu wameahidiwa na kufumba macho yao bila kujali athari ambzo zianweza kujitokeza ikwamo kuvunjika kwa Muungano ulioasisiwa na Wazee wtu Julius Kmabarage Nyerere na Abeid Aman Karume.
 
Aeleza mizengwe ya kimkakati kuzima hoja za madai ya serikali 3, asema ofisi ya waziri mkuu,Makamu wa Rais walipendekeza serikali 3.

Jaji Warioba amewatoa watanzania ukakasi juu ya muungano wa serikali mbili waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa. Umebadirishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya kufanya mabadiliko kwenye katiba.

Waasisi walituachia muungano wa nchi moja yenye serikali mbili na siyo nchi mbili zenye serikali mbili.
Karibuni kwa kuchangia.
 
Rasimu nzima ya katiba imeandaliwa kwa msingi wa serikali tatu.

Yani mambo yote ya kwenye rasimu ya katiba yamewekwa kwa kuzingatia serikali tatu.

Sasa sijui Warioba amepatwa na maswaibu gani!?

Maana ni wazi kuwa kuna Watanzania wengi wanahitaji muundo wa sasa wa muungano, tena wengi sana. Sasa 'sample' yake aliyoitumia sijui ameipataje kufikia maamuzi ya kuandaa rasimu ya wale wa serikali tatu?

Basi kama Warioba ameamua kuandaa rasimu kwa misingi ya serikali tatu, angefanya vyema pia kuandaa na nyingine ya serikali mbili pamoja na ile ya mkataba ambayo CUF wanaitaka.
 
Kuna kitu Waryoba ameahidiwa siyo bure, tusubiri tu tuone, haiwezekani asione haya hata kidogo kuliingiza taifa katika hatari ya aina hii. Huyu ni sawa Rais Pourtine wa Urusi anayelimega taifa la Ukraine bila hata haya.
 
Muzimu wa Karume na Nyerere lazima utamwandama tu Waryoba asicheze na kilio cha marehemu.
 
Amesahau kabisa hata Serikali moja ambayo yeye alijipambanua kuwa ni muumini wake.
 
Kuna kitu Waryoba ameahidiwa siyo bure, tusubiri tu tuone, haiwezekani asione haya hata kidogo kuliingiza taifa katika hatari ya aina hii. Huyu ni sawa Rais Pourtine wa Urusi anayelimega taifa la Ukraine bila hata haya.

Who is "Pourtine"? Hivi nyinyi magamba zaidi ya ufisadi kuna kitu kingine mnakijua?UDHAIFU mwanzo mwisho.
 
pombavu zenu mazezeta ndiyo mmejipanga kumchafua, warioba kawapiga chini ya mkanda..
 
Rasimu nzima ya katiba imeandaliwa kwa msingi wa serikali tatu.

Yani mambo yote ya kwenye rasimu ya katiba yamewekwa kwa kuzingatia serikali tatu.

Sasa sijui Warioba amepatwa na maswaibu gani!?

Maana ni wazi kuwa kuna Watanzania wengi wanahitaji muundo wa sasa wa muungano
, tena wengi sana. Sasa 'sample' yake aliyoitumia sijui ameipataje kufikia maamuzi ya kuandaa rasimu ya wale wa serikali tatu?

Basi kama Warioba ameamua kuandaa rasimu kwa misingi ya serikali tatu, angefanya vyema pia kuandaa na nyingine ya serikali mbili pamoja na ile ya mkataba ambayo CUF wanaitaka.

Hiyo hoja yako ya Watanzania wengi kuhitaji muundo wa sasa wa Muungano umeitoa wapi. Tume iliyokusanya maoni imekuja na data inayoelezea maoni ya wananchi wangapi wanasema nini, hii ya kwako ni ya kuupotoshaji. Muundo wa Muungano wa sasa nani alikuambia kuwa watu wengi wanaupenda wakati hoja ni kuwa huu muundo ulioopo siyo ule tuliachiwa na waasisi. Muundo wa Muungano tuliachiwa na waasisi ulikuwa wa nchi moja serikali mbili lakini huu wa sasa ni wa nchi mbili (moja ikiwa imevaa koti la muungano) na serikali mbili.

Wanaotetea Muundo huu wa sasa wa Muugano ni wanafiki na wazandiki kwa sababu wanataja tu kwamba Warioba anavunja muungano, oooh, muungano wa serikali mbili ukifanyiwa marekebisho utafaa. Wanapotaja muundo wa serikali mbili hawataji suala la nchi mbili ambalo ni ukinzani wa katiba ya muungano na katiba ya Zanzibar.
 
Amesahau kabisa hata Serikali moja ambayo yeye alijipambanua kuwa ni muumini wake.

Ondoa upuuzi wako huo, Warioba hajawakilisha maoni yake bali ya wananchi. kama maoni aliyowasilisha ni ya kwake basi angesema anachokiamini. Uwe mwepesi wa kutofautisha mambo
 
kwa nini mnamsakazia waryoba kutetea serikali moja, wakati ninyi ccm mnaogopa wazanzibar kuwaambia juu ya kuvunja serikali yao na kuwa na serikali moja?
 
Rasimu nzima ya katiba imeandaliwa kwa msingi wa serikali tatu.

Yani mambo yote ya kwenye rasimu ya katiba yamewekwa kwa kuzingatia serikali tatu.

Sasa sijui Warioba amepatwa na maswaibu gani!?

Maana ni wazi kuwa kuna Watanzania wengi wanahitaji muundo wa sasa wa muungano, tena wengi sana. Sasa 'sample' yake aliyoitumia sijui ameipataje kufikia maamuzi ya kuandaa rasimu ya wale wa serikali tatu?

Basi kama Warioba ameamua kuandaa rasimu kwa misingi ya serikali tatu, angefanya vyema pia kuandaa na nyingine ya serikali mbili pamoja na ile ya mkataba ambayo CUF wanaitaka.

Hivi nyinyi mijitu ya chama cha majuha (CCM) mna matatizo gani ya uelewa?Ndio kila mtu anajua ili uwe mshabiki wa ccm lazima ufahamu wako uwe chini ya wastani lakini hii imezidi. Yaani jana jaji Warioba amesema na jaji Augustine Ramadhani akakazia kuwa hakuna jambo lililoamuliwa kwa kura na hakuna mjumbe wa kamati aliyewakilisha mawazo au misimamo ya chama chake ila mawazo ya wananchi ndio yaliyotengeneza rasimu aliyoisoma jana. Dada Hamida tafuta mume uolewe labda utabadilika.
 
Kinashangaza. Tume ya Jaji Nyalali, Tume ya Jaji Robert Kisanga, Tume ya Jaji Waryoba, zote zinaona kuwa wananchi wanataka mfumo wa serikali tatu. Je wote hawa hawana akili? Je wote wamepotoka? Je wote wameahidiwa kifuta jasho? Ni kweli kuwa hatuoni sababu nzito alizotoa Jaji Waryoba jana kuhusu malalamiko ya pande mbili za Muungano kutoukubali mfumo wa serikali mbili? Anayebisha aende akafanye survey kule Zanzbar. Sample yako iwe ni random selected, watu unaokutana nao barabarani. Waulize kuwa wanataka muundo gani wa Muungano! Tusiwe washabiki wa chama chetu hadi kupuuza ukweli kama ule uliosemwa jana.
 
Back
Top Bottom