Warioba amewasilisha rasimu ya katiba au rasimu ya serikali tatu?


Mtatoka sana povu; lakini judge kawafunika kwa hoja zenye nguvu; mwenyekiti wenu atafungua bunge kwa mipasho na maneno ya kwenye kanga; CCM mnaweza kushinda kubadili rasimu kwa wingi wenu lakini si kwa hoja za maana!!!
 
Nilishawahi kuandika humu kuwa, kuna tofauti kubwa sana pale CCM wanapotamka neno "Mwananchi" na pale watu wengine wapotamka "Mwananchi". Mwanachi kwa wana CCM ni wale ambao ni WANACHAMA WA CCM.THE RESTS ARE NOT CITIZENS.Hili ndilo litakaloiua CCM.Hii nchi ni ya Watanzania wote, kama wapo wananchi waliosema wanataka serikali tatu unategemea Warioba angewakatalia tu kwa sababu inapingana na wanaCCM?Mliunda mabaraza ya Katiba na mkajaza wanaccm huku mkiwakaririsha waseme serikali mbili, walipotakiwa kutoa hoja kutetea point zao wakawa Tabularassa, ulitaka Warioba afumbe macho na kuafikiana nao?Zanzibar ni nchi, na imetamka hivyo katika katiba yao kuwa yenyewe ni nchi, nini hatma ya Tanganyika katika Muungano?Mna point gani ya kutetea hoja yenu ya Serikali tatu?Alichowasilisha Warioba kinapaswa kujibiwa kwa hoja nzito na Si mipasho mliyoianza na mnayotegemea kuhitimishwa na Mwenyekiti wenu Taifa. Think Beyond your Nose!
 
Hahahaaaaaaa no wonder mlikuwa mnataka atumie dkk 120 ili asimalize!!!!!
 
mtu na akili timamu kabisa anakuja hoja ya mizimu? hii nchi ina watu wagonjwa sana. warioba hawasilisha maoni yake. hili wengi hawalijui.warioba kawasilisha maon ya watanzania ambao walikuwa sample kuwakilisha maoni ya wengi. ufumbuzi ni kuwa na Serikali moja au Serikali tatu. kwa mnaoleta hoja za kulinda Muungano kwa nin hamsemi kuwe na Serikali moja? huu Muungano wa sasa ni Muungano gan fafanue. ni nchi gan ma nchi gan zimeungana?
 
kuna mambo mengi sana muhimu yanatakiwa kujadiliwa kwenye hii katiba, lakini cha kushangaza baada ya kujadili haya muhimu tumejikita katika hili oooh mara serikali 2 mara serikali 3, wanasiasa wameshaiteka katiba tayari, muda unakwenda, hili la serikali 2 au 3 linatusaidia nini sisi wananchi, kwani hata muungano ukivunjika kuna shida gani? tuna kero nyingi sana Za kujadiri kwenye katiba ili itusaidie sisi wananchi,, baadala ya sisi kuishinikiza katiba iwe yenye msaada kwetu, tunawasaidia wanasiasa kupiga domo, au ndio kila mtanzania mwanasiasa sasa??? watanzania tuache Kuwa mashabiki wa wanasiasa hebu tuwe kitu kimoja kuwakemea Hawa wanasiasa kwa manufaa ya sisi wengi,,, ili isaidie maendeleo ya kizazi kijacho.
tuache ushabiki wa kisiasa, tuamke tuwe kitu kimoja.
 

Hayo mawazo yaliyotolewa ni ya wale waliohojiwa tu kijana, hata kama wapo wengi wasiotaka huo mfumo wa serikali tatu na hawajatoa mawazo yao hayawezi kuingizwa. Kama unataka yawekwe basi na wewe andaa rasimu yako na mi-CCM wenzio.
 
Tunapojadili hoja ya serikali tatu au mbili, au muundo wa Muungano tunatakiwa kuja na vielelezo ambavyo vitang'amua ukweli na kuthibitisha hoja zetu, vinginevyo tunakuwa tunaongelea ushabiki tu usiokuwa na vithibitisho. Binafsi nampongeza sana Warioba, kwani kathubutu kuweka historia kwa kuacha kumumunya maneno kwa kuangalia nini wanasiasa wanataka kaamua kuweka wazi juu ya historia na muungano uliopo sasa na nn wananchi wanahitaji. Kimsingi yawezekana serikali tatu usiwe mwarobaini wa matatizo yaliyopo, lakini ukachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo na changamoto zilizopo kuliko mfumo wa sasa wa serikali mbili nchi mbili.
 
Kuna Raha , Catsnet , Ctv Na Satcom

Serikali 2 nchi 2, maana yake hapo hamna Muungano, yaani kila nchi inaserikali yake! Serikali 3 au 1 ndo Muungano!
 

Mkuu jipMbnue katika kusolve kiakili big and overiding issue first.
Unapoongelea mfugaji kama kipaumbele atahudumiwa na serikali ipi?
Na fungu lake la kodi ni kutokka kwa watu wepi?

Soma ujiridhishe na mada kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…