Warioba amshangaa Kikwete kusema mpasuko ndani ya CCM ni kidogo


......TAYARI ANASHUTUMIWA KUWA KAMBI YA SALMIN HAWEZI SIKILIZWA TENA KWA NAMNA UNAYOSHAURI,ENZI ZA MKAPA ALIPEWA TUME ILIYOKUJA NA MAPENDEKEZO YANAYOAMINIWA KUWA MAZURI KTK KUPAMBANA NA RUSHWA LAKINI HAIKUFANYIWA KAZI.

Mwisho kulalamika ndio imeshakuwa utaratibu kwani tumeona na kusikia WAZIRI MKUU ALIYEPO MADARAKANI AKILALAMI NA HATA RAIS SIMBUSE YEYE MTAAFU TENA AMBAYE HAYUPO "KUNDI" LA MTAWALA?
Warioba endelea kulalamika na kuwaeleza viongozi udhaifu wao hadharani ili na sisi wananchi tujionee serikali yetu ilivyo KIBURI na hatimaye tuweze kuamua vinginevyo.
 


Hana lolote anazeeka vibaya kafulia siasa
 
Msidanganyike kuwa Amos Makalla ndiye aliyemjibu Warioba; huyo ni mouthpiece too mwenyewe mkulu ndio amemwambia aseme hayo , kwani ndio staili zake kutumia decoys kama Makalla, Makamba etc. Naona ajabu watu wanasema Warioba angeweza kumshauri Jakaya badala ya kusemea magazetini, hilo haliwezekani kwasababu Jakaya ni mtu wa visasi,wale wote ambao hawakumuunga mkono kwenye mchakato wa kugombea urais 2005 kwake ni maadui, hajawasamehe na anawaona kama vile sio watanzania!! Juu ya yote Jakaya hashauriki na watu professionals kwani ana washauri wake wasio rasmi anaowaconsult kabla hajafanya maamuzi ya nchi!! Kama ni hivyo watu kama Warioba watapata wapi nafasi ya kumshauri?
 


Mimi nashauri ujumbe huu usomwe kwa makini maana mkuu you have said it all na hakuna la kuongeza wala kupunguza asante sana kwa muda wako
 


Kamati kuu ya CCM imejaa wajumbe wenye kila aina ufisadi.Kamati kuu ni chombo cha juu kabisa cha CCM na kinategemewa kutoa mwongozo na maamuzi makubwa kwaajili ya maendeleo ya Tanzania.Kamati kuu inapokuwa na wajumbe kama Makalla,Lowassa,Chenge,Kinana,Kingunge na wengineo kibao tegemea ubabaishaji kama majibu ya Makalla kwa Jaji Warioba.


100%
 

Bubu Ataka Kusema,
Wewe ni Bubu kweli?
Mbona ni mwenye maneno matamu?????
 
wafuasi wa salim tupo wengi ...na wala hatuoni aibu kusema!!!!....makala na jk na wanamtandao wakubwa lazima ipo siku wataabika mchana kweupeeeeeeeeeeeeee!!!.kwa kampeni chafu za kuchafua walizoendesha mwaka 2005'''''

jk ni muasisi wa siasa za MAJI TAKA!!!!...
 

UMEPATIA HASAA..JK NDIO HURATIBU MASHAMBULIZI YOTE ......na kwa kisasi alichonacho jk....na unafiki anaweza kufanya usanii wowote....

makalla is just in a bunch of fools...as the big fool out there...kwa kampeni zake za kibaguzi walizotumia mtandawoo...ndio anazotumia kule anakotaka ubunge ...naarifiwa kuwa anamfanyia murad ...kampeni za kibaguzi sana!!!...kisa kaahidiwa uwaziri nyeti mwaka 2010.......
 
Tena wa kutisha!

Hawana wanalolijua zaidi ya kupitisha siku wakijilimbikizia mali. Hakuna mwenye nia thabiti miongoni mwao ya kuendeleza nchi.

Ni mpaka pale Tutakapokuwa na tume huru ya uchaguzi ili uchaguzi uwe "Huru na Haki" ndiyo aliyepo madarakani atakuwa na pressure ya kuonekana kwa wananchi kuwa anawaletea maendeleo hivyo wampe kura za halali. Hiki kiburi chote cha CCM ni kwa sababu wanajua kuwa hata wananchi wawa-vote out wao wataji-vote in kwa kujitangaza washindi kwa kutumia Jeshi la polisi, na UWT kuwatisha watu.

"Unapofanya maandamano badala ya kuwafanya watu wakauze nyanya zao ili wajipatie mahitaji yao ya siku ni kupoteza muda"-Chiligati akiongelea maandamano ya CUF kudai katiba

Haya ndiyo mawazo yao halisi kuhusu watanzania.
 
Tusisahau lakini kuna majira ya kila kitu. Mtandao una nguvu leo, hatuji ya kesho. Ni vizuri kusimama ukweli ulipo maana hata miaka ikipita bado ukweli utatuweka huru.Malumbano haya ya wakubwa ndani ya chama ni ishara tosha kuwa lipo tatizo. panapofuka moshi, pana moto.
 
Wana-Jamii,
Nafikiri wote tunapenda kupata mawazo yanayojenga na si kubomoa. Nadhani viongozi wote wanajuana vyema na inawezekana "mchezo mchafu" upo na haiondoi ukweli kusema "mbona sikuiba mwenyewe" cha muhimu kila aliyekula vingi bila kupewa ruhusa na wananchi awajibike.
Labda Warioba alikuwa anajua sehemu ya kuweka mrija ili kupata kinyaji ki-urahisi na sasa anaona wenzake wanafaidi na hawampi mrija naye akavuta kidogo. Hii kama ndo ilivyo, ni vyema wananchi wakajua mrija huo ulipochomekwa na baadhi ya viongozi ili wasiendelee kunyonya bila ridhaa yao.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Bubu Ataka Kusema,
Wewe ni Bubu kweli?
Mbona ni mwenye maneno matamu?????


Ha ha ha ha ha Mkuu Ngida nitaanzisha thread kuhusu hili jina BAK muda ukiruhusu.
 
Makalla, Warioba wazidi kukabana koo Saturday, 03 October 2009 11:39
Na Mwandishi Wetu
Majira

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Uchumi na Fedha, ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Amos Makalla amezidi kumshambulia Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba na kudai kiongozi huyo hapendi kupingwa wala kukosolewa bali anapenda hoja zake zionekane ndio fikra sahihi.

Bw. Makalla ametoa hoja hiyo jana kufuatia kauli za Jaji Warioba kupitia gazeti moja la kila siku nchini, kudai kuwa amemtukana na anajipendekeza kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, baada ya kujibu hoja zake za hivi karibu alipokosoa masuala mbalimbali ya chama na utendaji wa Serikali.

Katika taarifa yake aliyoituma kwa gazeti hili jana, Bw. Makalla alisisitiza kuwa anamheshimu sana Jaji Warioba na hajawahi kumtukana bali alimlaumu mwanasiasa huyo kuwa hapendi kukosolewa wala kupingwa hoja zake.

"Nimesoma majibu ya Mzee Warioba katika gazeti (alilitaja jina ) leo (jana) . Katika utetezi wake anadai nimemtukana, najipendekeza kwa Kikwete, naendekeza mtandao na pia amesema yeye aliongelea matatizo yaliopo sasa ya udini na matabaka yanayohatarisha amani na alitumia fursa hiyo kuishauri Serikali.

"Naomba niseme tena namheshimu sana Mzee Warioba, na si kweli kama mimi nimemtukana ila Mzee Warioba ni miongoni mwa wazee wasiopenda kupingwa wala kukosolea na anapenda hoja yake ichukuliwe ni fikra sahihi ambayo kila Mtanzania anapaswa kuiheshimu.

"Ninamwomba kama kweli yeye ni mwana CCM thabiti tena Waziri Mkuu mstaafu, anashindwaje kutumia uzoefu wake kutoa ushauri kwa viongozi wa chama na Serikali katika vikao vyao, au kuwaona moja kwa moja maofisini, awe Rais , Waziri Mkuu na viongozi wa juu katika chama?

" Je fursa hizo kwake yeye anaona zimeshindikana na anaona ni vema ashauri kupitia vyombo vya habari? Au ni busasra gani ya kushauri Serikali kwa kuita waandishi wa habari? Kwanini yeye anapenda kukosoa kupitia vyombo vya habari? " Alihoji Bw. Makalla.

Bw. Makalla alisema kama Jaji Warioba anataka kuendelea kuheshimika akubali ushauri wake na akitumia staili hii, ajiandae pia kupokea changamoto kama hizi za kupingwa hadharani.

"Mimi sijajipendekeza kwa Kikwete kama anavyodai yeye mimi ni wajibu wangu kama mwana CCM na kiongozi kutetea chama changu na Serikali ya CCM . Yeye mwenzangu ameamua kutafuta umaarufu wa kuikosoa Serikali ya chama chake hadharani kwa maslahi binafsi, " alidai Bw. Makalla .

Alikana madai ya kuendekeza mtandao na kudai kuwa Jaji Warioba anapaza sauti kwa hoja dhaifu na kueleza kwamba kilichomkera ni kuambiwa ukweli kuwa kasoro anazotoa na kulaumu, zinasababishwa na kinyongo cha kushindwa mgombea aliyemuunga mkono mwaka 2005 , Dkt. Salim Ahmed Salim .

" Namshukuru amekiri kwa mara ya kwanza wazi wazi kuwa alikuwa kwa Salim 2005. Hivi kama inajulikana hivyo, sasa tutegemee nini unapolaumu Serikali hata jambo moja la kusifia hana kwanini nisiamini kuwa anaendekeza makundi.?

"Mimi sina kinyongo na Salim, namheshimu sana ila nina tatizo na wapambe kama anavyofanya mzee wangu Warioba, hayaishi tu?

"Hivi anataka nimkumbushe kuwa siku ya mkutano wa kupata mgombea urais 2005 yeye tayari alishavaa shati lake safi la CCM lenye nembo ya Bendera ya Taifa huku akiiamini kuwa Salim akishinda anakuwa mgombea mwenza! Kwanini nisiamini kuwa Salim alishakubali kushindwa lakini yeye akikumbuka umakamu basi hasira zake ndiyo kushambulia Serikali, tukimkosoa anasema ametukanwa! alilalamika Bw. Makalla.

Alimtaka Jaji Warioba kutafakari upya namna bora ya kutoa ushauri kwa Serikali na chama pasipo kuingia katika njia ambazo zitawaingiza Watanzania katika malumbano.

" Nachelea kuamini kama uzee ni dawa, lakini si kila mzizi ni dawa ipo mizizi mingine ni sumu. Mimi niliamini kuwa Mzee Warioba alimwelewa Rais alipoongea na wananchi juu ya udini, akalieleza vizuri sana. Sasa kama mkuu alishaliongelea hakuwa na sababu tena ya kuitisha mkutano. Suala la tabaka la walionacho na wasionacho ni changamoto kwetu sote kushirikiana na Serikali kutafuta majawabu.

"Nimemlaumu kwa kulaamu pasipo kutoa majawabu. Namtaka Mzee Warioba na Watanzania wote tushirikiane na Serikali kujenga nchi yetu, tuache siasa zitakazobomoa umoja wetu na amani tuliyonayo," alisema Bw. Makalla .
 
Warioba is also part of the problem (mnafiki)...anaendeleza makundi vilevile jino kwa jino wacha walumbane tunawaita walewale (agenda zao zinafanana) wamejificha kwenye nyasi fupi.
 
Ndugu you are damn right!
Wenye akili tunajua agenda zao ...wanaopiga kelele sana ukifanya dotting utakuta "the point of intersection" yaani kambi yao ya makutano ni ipi angalia hao wapiga kelele wote makutano yao ya "SIRI" ni wapi??? hakuna asiyejua "Too late" wana jificha kwenye nyasi fupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…