Shaycas
JF-Expert Member
- Feb 13, 2009
- 906
- 112
Hio ni kweli kabisa.
Warioba japokuwa sio mtendaji tena serikalini, lakini kama ni mwenye ushauri anaweza moja kwa moja akautoa huo ushauri wake kwa hao wanaohusika na hatua zikachukuliwa. Warioba sio mimi na wewe, ni mtu anaeheshimika mpaka leo, kwahivyo, sio mtu wa kupiga kelele magazetini. Kama anaona kuna ubaya fulani unatendeka anaweza kumuona hata Rais JK at any time. Kwanini hafanyi hivyo na anabakia kupiga kelele pembeni tu kama vile ni mlalahoi? Au anataka sisi wananchi tumsikie na tusahau juu ya Mwananchi Gold?
Kama wapinzani wanapiga kelele magazetini tunafahamu, lakini sio yeye. Japokuwa kastaafu bado heshima yake ipo pale pale. Ikiwa sote siku zote tutakuwa tunalaumu tu, sasa nani atatusaidia kutatua haya matatizo? Kwani hao watendaji serikali ni wenye ufumbuzi wa kila kero hata tunawasukumia wao kila kitu?
Kila mtu anajua kuwa udini, ukabila, utajiri, ufisadi, etc etc ndio kero zetu leo katika serikali hii ya awamau ya 4. Kwahivyo, kusema tena na tena juu ya mambo ambayo kila Mtanzania anayajua haisaidii kitu! Mimi na wewe tunaweza kupiga kelele kila siku lakini sio Warioba. Tukitaka kusaidia ni lazima tutowe mbinu za kutatua matatizo. Ni nchi yetu sote sasa kwanini hatutaki kutatua matatizo yetu kwa pamoja na tunajiweka pembenei kila wakati? Mimi na wewe hatutofika mbali, lakini Warioba atafika na atasikilizwa!
In fact, some of these problems that we are facing today in Tanzania have been created during his reign. Haya sio mambo yalioanza jana na leo - hasa huo udini. Au hajui hilo? Wakiwafanyia nini waisalamu katika utawala wao? Is it not right now kwa awamu hii to undo those wrongs?
I hope Warioba will realize that he is doing more harm to this nation by talking to the press than good - this is from the bottom of my heart. Hatutaki afungiwe uhuru wake wa kusema, lakini yeye ni mtu ambae kama angekuenda mbele na kusema basi angelisikilizwa and this nation would have benefited, lakini kama ataendelea kuropokwa kwenye magazeti tu basi hakuna atakae mchukulia kuwa yupo serious!
Au nitaulizwa ninajuaje kama hajawahi kutoa ushauri huko nyuma bila ya kusikilizwa? Kama ni hivyo atueleze!
Kwanini hafuati nyayo za Sh. Ali Hassan Mwinyi? Juzi alikuwa katika Kata ya Ndungu, jimbo la Same Mashariki, mkoani Kilimanjaro, akiengezea nguvu juu ya kile kinachoweza kuitwa mapigano dhidi ya ufisadi. Yeye sio mwenye kulalamika tu from the corridors of his house in Upanga kuwa nchi imechukuliwa na mafisadi bali anapigana nao huko huko kwenye Kata zao. Please, Warioba, follow his example. Tunataka ukumbukwe kama ni shujaa wa awamu ile na sio mropokwaje wa awamu ile!!!
......TAYARI ANASHUTUMIWA KUWA KAMBI YA SALMIN HAWEZI SIKILIZWA TENA KWA NAMNA UNAYOSHAURI,ENZI ZA MKAPA ALIPEWA TUME ILIYOKUJA NA MAPENDEKEZO YANAYOAMINIWA KUWA MAZURI KTK KUPAMBANA NA RUSHWA LAKINI HAIKUFANYIWA KAZI.
Mwisho kulalamika ndio imeshakuwa utaratibu kwani tumeona na kusikia WAZIRI MKUU ALIYEPO MADARAKANI AKILALAMI NA HATA RAIS SIMBUSE YEYE MTAAFU TENA AMBAYE HAYUPO "KUNDI" LA MTAWALA?
Warioba endelea kulalamika na kuwaeleza viongozi udhaifu wao hadharani ili na sisi wananchi tujionee serikali yetu ilivyo KIBURI na hatimaye tuweze kuamua vinginevyo.